Kubenea na UDA: Upele uliompata mkunaji. Mafisadi wakae chonjo

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,278
25,846
Mbunge wa Ubungo,Saed Kubenea,anajulikana kwa uthubutu wa kusema na kutenda pamoja na kufuatilia jambo. Suala la kurejesha UDA mikononi mwa Serikali ni moja ya ahadi zake za kuupata Ubunge wa Ubungo. Ahadi nyingine ni kuifutilia mbali Mahakama ya Jiji na kutaja waliochota mabilioni ya Escrow kupitia Stanbic Bank bungeni.

Kubenea ameanza na UDA. Ameshakusanya lundo la nyaraka kuhusu UDA kwa ajili ya kujengea,kutetea na kufuatilia jambo hilo. Saed Kubenea amedhamiria kweli na wala habeep. Hataachia njiani suala hilo la UDA kwakuwa anatekeleza moja ya ahadi zake. CAG amempa nguvu ya kuendelea na mapambano yake kuhusu UDA. Mafisadi wakae chonjo kwani Kubenea hatanii katika sakata la UDA.
 
Bado upo CHADEMA tu, wewe si ulisema Lowasa akihamia CHADEMA na wewe unatoka kwa mlango mwingine, aibu kabisa.
 
...naona anakomaa na simon group waliouziwa UDA kimagumashi...anajua wamiliki wa simon group na anataka kuwaumbua....ameanza kwa ku engineer kukamata mapesa yao (5bil kwenye halmashauri ya jiji)....hii kitu inaweza kutuletea hadithi nzito kuliko ile escrow.....ngoja tusubiri.....
 
Lini nilikuwa CHADEMA? Mimi nazungumza mambo ya kitaifa mkuu. Weka ushahidi hapa juu ya unachodai.
Kuna masuala mengine itikadi za vyama ni vyema zikawekwa kando, tuache uzalendo utamalaki. Hili la UDA suala linatia kichefuchefu sana hasa ukiangalia jinsi wahusika wanavyolichulia poa. Tunamuomba Bwana Kubenea akianzisha jambo lifike mwisho na liwe na hatma inayoeweleka.
Hili jambo nakumbuka jinsi waliokuwa wabunge wa Dar es Salaam bila kujali vyama vyao walikuwa wakilikemea sana na kuna wakati aliyekuwa Meya alidiriki kuwatukana na kuwaambia wanafikiri kwa kutumia makalio yao. La haulah, watu wazima na fikra zao walitukanwa na Bwana Masaburi na wakaufyata. Sasa ni wakati wa kuuthibitishia watanzania kwamba wao wanafikiri kwa kutumia ubongo kama binaadamu wa kawaida, la sivyo..............
 
Back
Top Bottom