Kubenea kugombea ubunge kwa ticket ya CCM - Mafia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kubenea kugombea ubunge kwa ticket ya CCM - Mafia

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Ex Spy, Aug 29, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Ex Spy

  Ex Spy Senior Member

  #1
  Aug 29, 2009
  Joined: Jan 15, 2007
  Messages: 139
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Katika hali ya kustaajabisha kuna taarifa kuwa yule mwandishi wa habari na mmoja kati ya wamiliki wawili wa gazeti la mwanahalisi amekuwa katikajuhudi kubwa ya kutengeneza mazingira ya kugombea ubunge kupitia CCM.

  Saidi Kubenea ambaye ana asili ya kisiwa cha Mafia amekuwa katika harakati za kujenga mtandao wa ushindi miongoni mwa vigogo wa CCM wa makamdi mbalimbali ambao anaamini kuwa wataweza kumpatia ushwawishi na fedha za kuukwaa uheshimiwa.

  Tofauti na hapo mwanzoni, Kubenea ambaye aliwahi kuwa kada maarufu wa CUF na kuendesha moja ya magazeti ya chama hicho na baadaye kushirikiana na vigogo wa CHADEMA kuanzisha na kuliendesha gazeti la Mwanahalisi, siku hizi amekuwa karibu sana na makundi yote ya CCM yakiwemo yale ya wapiganao na ufisadi na pia mtandao ambao umekuwa mtetezi mkubwa wa mafisadi na maslahi ya CCM.

  Kubenea amekuwa akilalamikiwa sana na watu ambao alikuwa nao karibu hapo kabla katika kuendesha kampeni za kuanika ufisadi unapofanywa na vigogo wa CCM wakiwemo wanamtandao ambao hivi sasa wamegeuka kuwa masahiba wake.

  Baadhi ya wanaolalamika wamo waandishi wenzake ambao mara kadhaa ndio wamekuwa ama chanzo cha habari zilizokuwa zikitoka Mwanahalisi ama hata kumuandikia nyingi ya habari hizo na kumpa kubenea kutumia jina lake.

  Wengi wamekuwa wakilalamika na tabia ya Kubenea ya kuendesha fitina dhidi yao ili yeye ndiye aonekane wa muhimu na wengine wote ni wabaya.
  Baadhi ya majeruhi wa majungu na fitina za Kubenea ni pamoja na waandishi kadhaa wa habari na wanasiasa vijana ambao yeye kwa kutumia fitina ameweza kujenga uaminifu mkubwa kwake kwa staili hiyo ya kuwafitini wenzake na kuwafanya wanasiasa muhimu na wapambanaji kuchukiwa na wengine kupoteza nafasi zao.

  Miaka kadhaa tangia kuanzishwa kwa Mwanahalisi amekuwa akipata misaada mbalimbali ikiwemo matangazo ya matoleo yake ya kila wiki katika TV na pia baadhi ya habari kutumia Mwanahalisi kuepuka kuyaingiza magazeti mengine katika matatizo ya Kisheria.

  Kubenea pia kwa kutumia mbinu zake hizo hizo za fitina na majungu ameweza kujijengea ukaribu mkubwa na wanasiasa wa makundi yote yanayopingana ndani ya kundi la Mtandao.

  Baadhi ya watu wamekuwa wakihoji uhusiano huu wa Kubenea na wale ambao mara nyingi amekuwa akionekana kuwapiga vita kutokana na machafu yao. Wapo wanaosema kuwa Kubenea alianza mahusiano haya ya karibu na vigogo wa CCM mara baada ya kumwagiwa tindikali na kutembelewa hospitalini na Rais Kikwete na vigogo wengine wa CCM ambao kwa pamoja walimchangia fedha kwenda kutibiwa India.

  Yapo madai kuwa hata suala zima la kumwagiwa Tindikali lina siri kubwa linalohusiana na tabia yake ya fitina na dhuluma ingawa waandishi wenzake na wanasiasa kadhaa waliweza kulifanya lionekane kama lilihusiana na uandishi wake kuhusiana na habari za mafisadi.

  Mafisadi ambao sasa wamekuwa marafiki zake kiasi cha kumhakikishia kuwa pamoja na misaada ya kifedha na ahadi za kumhakikishia anaukwaa uheshimiwa ndani ya CCM pia gazeti lake linaongoza katika kupata matangazo mengi kutoka wizara na mashirika ya serikali kama ilivyokuwa katika miezi ya hivi karibuni.

  Hii ikiwa ni tafauti na kawaida ambapo magazeti yanayoonekana kukosoa serikali, chama tawala na viongozi wake yamekuwa yakinyimwa matangazo kutoka serikali ambayo ni msingi mkubwa wa kuendesha biashara ya magaeti hapa nchini.

  Baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya naye kazi ikiwemo hata kumuandikia makala na yeye kupachika jina lake wameanza kumkwepa. Wapo wanoalalamikia kuwa amekuwa akiendesha gazeti kwa staili ya kuwalaghai watu kumsaidia uchapishaji wakati ambapo kama angelikuwa na mfumo wa kudhibiti mapato na matumizi yake asingekuwa akilazimika kujitembeza kwa wafadhili wake ambao anapaswa kuwakosoa maovu yao serikalini na katika chama.

  Lakini wengine wameshtushwa sana na mpango wake wa kugombea ubunge kupitia CCM wakati wote kwa pamoja wanaamini kuwa CCM ndio msingi mkuu wa ufisadi nchini ambao yeye alipaswa kuwa mfano wa kuigwa katika kupiga vita.

  Yangu machache mengi yanakuja siku za hivi karibu ambayo mkiaangalia na kupima mtaona ni jinsi gani tuliyekuwa tukimuona hero wetu amekuwa compromised na karibuni ataishia kama Mtikila na mashujaa wetu wengine…
  Habari ndiyo hiyo watanzania….sijui tumemkosea nini bwana wetu aliye mbinguni…

  Hii si tetesi, ndio ukweli wa mambo!

  UPDATE 1:
  Majibu ya Said Kubea

   
  Last edited by a moderator: Aug 30, 2009
 2. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #2
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160

  Habari yako ingekuwa nzuri kama ungeweka wazi vyanzo vyako vya habari na pia kuachana na uandishi wa ki-machale. Hakuna hata sehemu moja umetaja jina au majina ya watu unawaongelewa. The whole story is floating!
  Pia tupe data basi, Mwanahilisi ni gazeti la CHADEMA?
   
 3. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kama madai haya yana ukweli basi Tanzania si salama hata kwa wale wapiga makelele ya mageuzi Tanzania. Una maana Said Kubenea ninaye mjua mimi ?
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Aug 29, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Biased, one sided story. Halafu story yenyewe ni tetesi lakini with full of conclusions!!
   
 5. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Hizi shutuma na tuhuma Kubenea aambiwe aje aseme hapa si ana uwezo wa kuutumia mtandao huu? karibu Kubenea
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Is not concluded, nilisema na kutukanwa almost katika post nyingi kuwa huyu jamani si mnavyo mfahamu.

  Ukinipa habari yeyoteya mwanahalisi iliyowahi kumuandika JK vibaya, basi nitamuona Kubenea mwanamapinduzi.

  JF kutokana na mapenzi kuwa huyu Bwana mko tayari kutukuna hata kupigana pale watu walio serious katika mapinduzi wakianza kuwasema mamluki wanaoonekana nao kama vile wapiganaji.

  JK is highly organised never underestimate him!!!!!!!! NEVER!

  tutasema tu mika nenda rudi without positive and remarkable developments, au tangu tulipoanza kupigana habari za ufisadi, nani kaenda jela, nani karudisha hela zetu KAMA WAPIGANAJI TUSIPOKAA CHINI NA KUONGALIA STRATEGY ZETU KAMA ZIKO SAHIHI, NITAONEKANA M'BAYA KWA KUANZA KU-POINT WATU WANAORUDHISHA HAYA MAPAMBANO NYUMA?

  NIKIOGOPA KUSEMA NDANI YA JF, NITASEMA WAPI NIMUOGOPE NANI?

  TIME WILL TELL, i will retriev all my post na matusi, will then ask them YAKO WAPI??

  MWANAHALISI NI LA JK HILO LINAJULIKANA, hata kubenea anajua watu wanajua hivyo, kumwagiwa tindikali kwa sababu ya tuhuma za wanawake was good move to twist as political issues!


  why talk about CCM, they are everywhere, within us and we real think they are ours.
   
 7. M

  Masatu JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mbona tunakuwa waoga sana ikitajwa tu fulani anagombea sehemu fulani? si ndio demokrasia? kama kupinga ufisadi Sitta, Kilango, Kimaro, Shulukindo( Mr & Mrs ), Sendeka, Mpendazoe, Mkumba, Selelii na Eng Manyanya hawa wote si wapo CCM? mbona wameweza? kwanini Kubenea asiweze akiwa CCM? au ndio mpaka uwe Chadema?

  Acheni hizo ndio maana mnamsakama Zitto...
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Wote wasanii. Hakuna mtu anaweza kupinga ufisadi akiwa bado yuko ndani ya CCM. Ndiyo maana nilisema na nitasema kuwa kama kweli Sitta anapinga ufisadi basi angeacha kadi yao pale DOM. You are either with them or against them. Hakuna neutral kwa CCM!
   
 9. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #9
  Aug 29, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Labda kaona akienda Chadema hatapewa nafasi kama anavyobaniwa Zitto.ataambiwa kijana.
   
 10. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #10
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bodi ya wakurugenzi wa mwanahalisi ina vigogo wa chadema kadhaa, hii haina maana gazeti ni la chadema. Chadema kama chama hawana mamlaka yeyote kwenye hilo gazeti.

  Nijuavyo mimi Kubenea amepania kugombea Rufiji kupitia chadema.
   
 11. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #11
  Aug 29, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kubenea, Kubenea, Kubenea....

  I have never trusted this fella, never from the first day I saw him...

  Jembe Ulaya na "post zako tatu" acha upotoshaji.....Haya ya kubenea kugombea CCM hata mimi nimeyapata kutoka kwa haohao waheshimiwa wake nikadhani ni propaganda hadi nilipofuatilia zaidi nikayakuta mengi zaidi ya haya....angalieni huko kwenu mna virusi vya kutosha msiongezee vingine tena wakati huu wa UCHAGUZI "wenu"

  omarilyas

   
 12. Jembe Ulaya

  Jembe Ulaya JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2009
  Joined: Oct 27, 2008
  Messages: 456
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wapotoshaji ni "vijana wajinga" aliyewataja kibanda. Nafikiri bwana Omar Ilyas unawafahamu vizuri saaana...

  Time will tell.
   
 13. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Naona umekimbilia REFA. Usidhani kuwa sikutambui kaka. Nimeanza mapambano wakati wewe hata majengo ya mlimani huyajui.

  Hata ukitumia majina 100 nitakung'amua tu kaka, wewe kwangu utabaki kuwa mwanafunzi tu na sio zaidi.

  Nipo karibu hapa, mkithubutu kuvua gloves, naamini unanitambua katika sekta hiyo....

  omarilyas
   
 14. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  jamani vueni gloves, na sisi tupate mengi
   
 15. Z

  Zurich Member

  #15
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wewe jembe ulaya,

  Umetumwa na akina lowasa nini?, hata siku moja Kubenea hawezi kufanya hivyo. Kasome makala ya mwanahalisi ya wiki hii kwanza. Kubenea ni mzalendo hawezi kwenda CCM.
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Huwa mnakuwa kimya kama ndege aliyelowana mambo yakiisha wekwa hadharani! ona sasa kama bado uko gizani pole,

  swala ni kuwa mafisadi wako well organised kiasi cha kuwateka wale unaowaona ni wapambanaji, muda umefika wa mimi na wewe kutokuwasubiria wengine!

  CCM has to go, kuanzia waliopo na vizazi vyao vyote , sumu hiii!
   
 17. Z

  Zurich Member

  #17
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Niliishasema, CCM imefikia kikomo hivyo katika hilo sina wasiwasi kabisa, wao wenyewe watajimaliza, na kama kubenea ameshawishika pia siwezi kusikitika maana, tutamuheshimu kwa kipigo alichokipata kwa kutetea watanzani kupitia kazi yake katika gazeti la mwanahalisi, ila ingawa atajuta kwa uamuzi huo wa kuhamia CCM maana hatapata ubunge. Tuko pamoja mkuu wala sikupingi ila tu nilistuka kidogo kusikia hivyo,,,,,,,,
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Aug 29, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Kila mtu anayeiponda ccm mwisho hujiunga nao,nyerere alisema kigumu chama cha mapinduzi,,,,,,,,,ha ha ha,,,,,,,,
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  Aug 29, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Aliandika njama za kumuangusha JK na gazeti lake likafungiwa miezi 3.
   
 20. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,438
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Wagombea ubunge watarajiwa Mafia kwa tiketi ya CCM ni Omari Kimbau (keshapeleka gari ya kampeni), Abdulkarim Sham mbunge wa sasa, Carlos na dada mmoja daktari. Hao ndio wenye pilikapilika za Ubunge Mafia. Kubenea hayumo!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...