TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Gazeti la leo la MAWIO kwenye ukurasa wake wa Mbele lina KIKARAGOSI kinachowaonesha Waziri wa Nishati na Madini, Sospeter Muhongo na Mbunge wa Kigoma mjini kupitia ACT-WAZALENDO, Zitto Kabwe. Kwenye kikaragosi hicho Zitto anaonekana kumuita mwizi Waziri Muhongo kipindi fulani huko nyuma, lakini kwa sasa anaonekana kupiga magoti mbele ya Waziri Muhongo kama ishara ya kunyenyekea kwake.
MAWIO ni gazeti la Mbunge wa Ubungo kwa tiketi ya CHADEMA, SAID KUBENEA mtu ambaye kwa takribani miaka mitatu aliandika makala kuhusu UFISADI WA LOWASSA.
Pamoja na vyanzo vingine, makala hizi za KUBENEA nazo zilitoa mchango mkubwa sana kwa watanzania kujua madudu ya LOWASSA na washirika wake katika nchi hii.
Hata kushindwa kwa LOWASSA kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka jana katika ngazi ya urais kulitokana na CCM kutumia vema AGENDA ya UFISADI, agenda iliyokipa umaarufu mkubwa chama cha CHADEMA kutokana na kuhubiri UFISADI wa watu mbalimbali huku viongozi wa CHADEMA kwa nyakati tofauti wakionesha kuwa LOWASSA ndiye aliyekuwa KINARA wa MAFISADI nchini kwa kutoa kauli mbalimbali, moja ya kauli hizo ni ile ya Mch. Peter Msigwa kuwa "ANAYEMSHABIKIA LOWASSA ANAPASWA KUPIMWA AKILI" na ile ya MBOWE kuwa "ANASHANGAA KUONA SERIKALI IKIHANGAIKA NA VIBAKA HUKU IKIMUACHA LOWASSA ANAKULA BATA MTAANI"
Leo hii KUBENEA KAPIGA MAGOTI NA YUKO CHINI YA MIGUU YA LOWASSA akimnyenyekea.
Hiki KIKARAGOSI, KUBENEA amejichorea mwenyewe akijifanya kuwa amesahau historia yake na LOWASSA.
HUKU NI KUJIDHALILISHA.