Kubenea anawakilisha tatizo jipya la Uongo katika jamii!

Kubenea anawakilisha tatizo jipya la Uongo katika jamii!

meningitis

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2010
Posts
8,464
Reaction score
4,832
Kwa miaka mingi nchi yetu imekabiliwa na maadui wanne yakitajwa kama elimu,maradhi,umasikini na rushwa(ufisadi).

Matatizo haya yameshindikana na sasa yanaonekana kama ni laana ya Mungu kwa watanzania.

Tukiwa bado tunajadili jinsi ya kuondokana na matatizo hayo sasa tunajionea tatizo jingine hatari sana likiibuka na kurasimishwa kama ni jambo na tabia ya kawaida ya watanzania.

Tatizo la kutokusema ukweli ni changamoto mpya nayoikabili jamii yetu kwa sasa.

Uongo unakuwa ni jambo la kushabikiwa na wananchi kiasi cha kufanya wale walioonekana kutaka kusema ukweli waamue kuwa waongo.

Saidi kubenea alijizolea umaarufu mkubwa sana kupitia kalamu yake kwa kianika ukweli kiasi cha kuonewa huruma na wananchi na kuaminiwa kuwa ni msema ukweli.

Leo hii Saidi kubenea anaibuka na kuamua kuukataa ukweli uliotikisa taifa tena yeye akiwa mwanahabari pekee aliyeamua kuusema.

leo hii kubenea anatudanganya kwa kuanzisha uongo mwingine kuhusu ripoti ya richmond.

Sikushangaa kumuona Mbowe akiukana ukweli kwani imesemwa amefanya hivyo kwa kuchukua chochote.

Simshangai Sumaye au lowassa kutuaminisha uongo kwani wao ndio walikuwa mfumo wa uwongo tulioukataa.

Simshangai lissu kusema uongo baada ya tetesi za kununuliwa.

Simshangai Mnyika kuutetea uongo kwa kuwa kuna tetesi ya kupewa chochote na bado kama kijana yuko katika sintofahamu.

Sishangai Mbatia kuwa muongo kwa kuwa tulimshitumu mara kadhaa kuwa muongo ndani ya upinzani.

Siwashangai wanasiasa wengi kuusema uongo kwani walitumia ujinga wa watanzania ili wapatenafasi za kuuishi uongo wao.

Ninamshangaa sana kubenea ambaye kidogo apoteze jicho kwa kuusema ukweli.

Leo hii kubenea anataka watanzania kuwa waongo kwa kuwa hakuna adhabu iliyowahi kuwakumba waongo kwenye ardhi ya watanzania ukiacha kusutwa tu!

HIVI KUBENEA ALIICHAPISHA STORY YA UONGO WA MWAKYEMBE KUHUSU RICHMOND?

KAMA ALIICHAPA ALIKUSUDIA NINI KWA WATANZANIA?

Huu ni mwanzo mbaya kwa Taifa linaloanza kuchomoza kiuchumi.

Siwezi kuwa tayari kutumia uongo ili kuondoa uongo.

Inabidi aje shujaa mpya wa kuanzisha mapambano mapya dhidi ya uongo.
 
meningitis

Kupitia kalamu yake Kubenea amewahabarisha watz mambo mengi ya kweli, na ndiyo maana akapoteza jicho lake. Hebu tusaidie ni kipi wewe umechangia katika kuwapa ukweli watanzania?
 
Last edited by a moderator:
hahahahaaa magamba mnadanganyana.subirini kichapo kunako 25 oct.

masaburi hata robo ya kura hapati.
 
Hahaha mkuu si ulianzisha mwenyewe sasa ngoja tulianzishe hili swala kisawasawa ili tujue na ni mwizi wa RICHMOND. na Lowassa bado anasubilia tu SIKU ukkiropoka tu yeye anamaliza.

VIVA ROMA VIVA.

swissme
 
Tuàmbie aliposema uongo ili tuamuwe mashiko ya hoja yako. Hadithi nyingi siyo muda wake. Kumbuja hansard za bunge zinajibu kwa usahihi hoja ya Kubenea kuhusu ripoti ya Richmond.
 
WanaJF waliyoyumbishwa na blog ya kubenea na kuhama JF watakuwa wametambua nia ya kubenea kutaka kukivuruga chombo hiki kinachosimamia ukweli.
 
CCM imechokwa,haikubaliki na haichaguliki.Weka mbali na watanzania.Kamwe mbu hawezi kutibu malaria!
 
Kupitia kalamu yake Kubenea amewahabarisha watz mambo mengi ya kweli, na ndiyo maana akapoteza jicho lake. Hebu tusaidie ni kipi wewe umechangia katika kuwapa ukweli watanzania?
Uuuwii. Waacheni wadanganyane eeh. Wajinga haoo.
Kubenea alivamiwa kwa kuwa na tabia ya kumendea wake za watu huku akilelewa nao
 
Bora muongo mmoja kuliko mamilioni ya waongo UGAMBANI.
 
Kebenea kisha hongwa pumbavu tu
Mfungwa ni vizuri ukifunguka ili ufunguliwe, neno hili alilitumia rais mstaafu likapokelewa kwa mtazamo hasi. Kwa nini nawe umependa kulitumia dhidi ya Kubenea? Upumbavu wake ni upi? Agenda yako ni nini juu ya kubenea? Ni vema ukijenga hoja yenye msingi wa maendeleo ya umma!!
 
Wanasiasa wengi ni waongo tu, wameishiwa hoja sana na hakuna jolts wanalosema zaidi ya kupigana vijembe majukwaani badala ya kuleta hoja na jinsi gani watawakilisha wananchi huko bungeni.

Wananchi wengi nao majuha tu, kazi kushangilia ujinga bila kuchuja hoja na sera. Ndio maana tuna taifa ovyo tu....

Hakuna la maana Kubenea alilosema zaidi ya vijembe vya wanywa kahawa wa pale Karume.
 
Kubenea amegusia vitu, kama :-
A) ubinafsishwaji wa uda
B) Mkataba wa Richmond
C) N.K
Naomba tujadiliane A~B
Je? Kwa nia thabiti ya taifa hili letu, ni kigezo kipi serikali ilikiona cha kubinafsisha UDA?
 
Inasemekana hao anaowasafisha sasa ndio kidogo wampofushe macho leo hii kasahau. Je kafungashiwa furushi la fedha? Kapewa rushwa?
 
Back
Top Bottom