Kubebana kabla ya ndoa ni suluhisho la wanandoa?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kubebana kabla ya ndoa ni suluhisho la wanandoa??

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Aug 9, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  [h=3]Kubebana![/h]

  [​IMG]
  Kwa nini jamii nyingi za vijana wa leo huchukua uamuzi wa kuanza kuishi pamoja kinyumba kabla ya kuoana rasmi na ndipo kuanza maisha?
  Wengi hutoa sababu nyingi mojawapo ni kuokoa fedha za kutumia kwani badala ya nyumba mbili huwa nyumba moja, kutumia muda mwingi pamoja, kuwa karibu kihisia (feelings and emotions), kuzoeana kimapenzi (sexual intimate) pia ni kitu rahisi ambacho hakina gharama.
  Zaidi wengi hutoa sababu kwamba wanaishi pamoja kabla ya kuoana rasmi kwa sababu wanajitahidi kuangalia namna wanafanana na kufahamiana ka undani zaidi na kujaribu kama itawezekana (testing) kuishi pamoja na kuridhika kwamba waoane (wanaogopa kununua mbuzi kwenye gunia) kwa kuchunguzana mazingira ya masaa 24 siku 7.
  Je, ni kweli wachumba kuishi pamoja kwanza hupelekea kuoana na ndoa kuwa imara baada ya kuoana?
  Ukweli ni kinyume chake, tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu ambao huamua kuishi pamoja (Cohabitation, common law, kuvutana, kuishi katika dhambi, kuchukuana nk) kwanza huongeza uwezekano wa kuachana baada ya kuoana na mara nyingi wengi hata kuoana huwa inashindikana huku kila mmoja akiwa amejeruhiwa vibaya kwa kupoteza muda wake na mali zake.
  Kubwa zaidi wapo ambao hufikia hatua hata ya kuzalishana watoto na hata kabla ya kuoana huachana huku mwanamke akipelekeshwa na maisha ya kutunza watoto wakati baba anaenda kuona mke mpya.
  Hii style ya kuishi pamoja kabla ya kuoana si lolote wala chochote zaidi ya kupotezeana muda na kuharibiana maisha na kuweka rekodi ambazo huwa gharama kubwa kwa maisha yote ya mtu kwamba aliwahi kuishi na mwanaume au mwanamke a hakuoana naye, unakuwa umejiwekea kibandiko (label) kwamba wewe ni moja ya failures na itaku cost kujisafisha katika ile jamii.
  Kwa nini ni muhimu sana kuoana kwanza na ndipo kuishi pamoja?
  Pamoja na kwamba kuoana kwanza ndiyo utaratibu wenye Baraka wa ndoa zote, kuingia kwenye ndoa si mchezo au jambo dogo (kids game) bali ni agano kati ya wawili wanaoana na Mungu kwa maana hiyo lazima kuwepo kiapo (commitment) kit ambacho hufunga wawili wanaoana kuishi maisha yao pamoja bila kujali nini kinatokea mbele “No matter what”
  Kiapo ambacho unaapa kwa mwenzi wako siku ya kuona ni kukubali kuishi naye maisha yako yote yanayobaki hapa duniani na ni msingi wa ndoa na kwamba hiki kiapo ni unconditional kwamba utaishi naye hata kama ni matajiri au maskini, afya njema au ugonjwa, katika shida au raha, kuwa na watoto au kutokuwa na watoto hadi kifo kitakapowatenganisha.
  Wanaochukuana au kubebana na kuanza kuishi huwa katika risk ya kuachana muda wowote kwa kuwa hakuna kiapo, hakuna ahadi (covenant) hakuna commitment, hakuna furaha ya kweli, hakuna amani ya kweli kwa kuwa si utaratibu wa ndoa na ni njia nzuri ya kuachana na kuharibiana maisha na mara nyingi anayeumizwa zaidi ni mwanamke.
  Jambo la msingi na la kukumbuka ni kwamba unapofahamu kwamba mwenzako yupo fully committed kwako hii husababisha ujisikie vizuri (security) na huweza kuimarisha kujisikia kitu kimoja na wewe ni mali yake na zaidi mnaimarisha ile bond ya kuzoeana na kuwa karibu kimapenzi kwa kuwa unafahamu mwenzangu amejitoa na kunikubali maisha yake yote.
  Kubebana na kuchukuana na kuanza kuishi pamoja kabla ya ndoa ni njia nzuri ya kufanyia mazoezi ya kuachana.
   
 2. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kule kwetu inaitwa nzogwi twigashe
   
 3. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Big up kaka umemaliza pande zote!
   
 4. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  makubaliano tu
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Sipendi kubeba wala kubebwa. Mambo mengine hata hayahitaji haraka.
   
 6. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #6
  Aug 10, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kazi kwenu
   
 7. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #7
  Aug 10, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kani mnabebana ili nini? na kwanini wapenzi waishi pamoja au wafunge ndoa?
   
 8. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #8
  Aug 10, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Eti ni kutesti zari.... Kuona kama ni right candidate au Kimeo!
   
 9. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #9
  Aug 10, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi kwani ndoa ni nini??
   
 10. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #10
  Aug 10, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,672
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  Kama vile ulikua unajua ninachowaza,hebu atujibu halafu tumwage hoja!
   
 11. mimyv

  mimyv Member

  #11
  Aug 10, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi cfkiri ivyo...
  watu wangapi wameoana kwa ndoa na mambo mabovu tu? nimeshtuka kuona unaniambia uchunguzi mdogo uliofanyika ..." umefanyika wapi na takwim zinasemaje...???? izi mambo hazina formula, japo kimaadili ya kitanzania yale yalowekewa misingi yanataka ndoa kwanza...itategemea tu mtu unafata nn? kama maadili subiry ndoa au kama unafata upepo basi ufaate vema...
  ni maoni
   
 12. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #12
  Aug 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Ina raha yake ..
  Usiniulize raha yake ni nini??
   
 13. mimyv

  mimyv Member

  #13
  Aug 10, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mi cfkiri ivyo...
  watu wangapi wameoana kwa ndoa na mambo mabovu tu? nimeshtuka kuona unaniambia uchunguzi mdogo uliofanyika ..." umefanyika wapi na takwim zinasemaje...???? izi mambo hazina formula, japo kimaadili ya kitanzania yale yalowekewa misingi yanataka ndoa kwanza...itategemea tu mtu unafata nn? kama maadili subiry ndoa au kama unafata upepo basi ufaate vema...
  ni maoni
   
Loading...