Kuanzisha Biashara Mpya (ofa ya serikali)

Ichwampaka

Senior Member
Nov 19, 2018
107
225
Katika kuongeza ajira katika sekta binafsi na serikali kuwekeza ili kupata kodi baadaye, napenda kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli kusaidia watanzania kukuza uchumi wao kwa kupendekeza mambo yafuatayo:

1. Serikali iruhusu mtu yoyote kuanzisha biashara yoyote halali na kupewa tax break kwa muda wa miezi mitatu. Kuanzia 1st July 2020 hutalipa kodi, leseni, ushuru wa tozo yoyote hadi 30/09/2020. Kuanzia 1st October 2020 ndio utaanza kukadiriwa kodi na kulipa tozo na ushuru kuanzia hapo kwenda mbele.

2. Biashara ni zile mpya kabisa (TIN number mpya) ndio zinaingia kwenye huu utaratibu.

Serikali haipotezi chochote ila inakuwa ''imepanda mbegu'' ya kuvuna kodi hapo baadaye. Lazima kuwa na njia za kuvutia watu kuanzisha biashara. Katika mpango huu kwa nchi nzima inatarajiwa biashara mpya (walipa kodi wapya) 875,000.

Rejea ushauri wangu mwingine:

Business development unit ndani ya Serikali
 

Koffi Annan

JF-Expert Member
Dec 23, 2018
645
1,000
Si mpaka wakuelewe
Anyway nahisi kwa government kuna intellectual wanaowaza hii vitu so itakua kuna obstacles zinazowafanya wasitekeleze ushauri kama huu
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
7,337
2,000
Wangesamehe kwa miezi sita, na baada ya hapo hawana haja ya kukadiria kodi, iwekwe (kujulikana kisheria) asilimia kadhaa ya mauzo (mapato) iende kwenye kodi.

Hii dhana ya kukadiria tena bila ya ukizingatia uhalisia wa hali ya biashara husika inawafilisi wafanyabiashara.
 

Nicklaus

JF-Expert Member
Sep 24, 2014
292
250
Nachojua kwenye budget iliyopita waliweka hiko kipengelea cha tax break ya miezi sita. Sina uhakika kama kilipitishwa au la
 

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,481
2,000
Watanzania watafungua Biashara kisha watafunga baada ya miezi 6! Kisha pale pale Atafungua mkewe! Miezi 6 atafunga afu atafungua Mjomba! Baadae Baba mdogo! Miaka mi3 biashara imemilikiwa na 6 lkn ni mtu yule yule
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom