Kuanzia leo sitaki kuona ujumbe wako wala simu yako kwenye simu yangu

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
Kauli hii ni kauli inayonichanganya sana. Mimi ni msichana, nimekuwa na mahusiano na mpenzi wangu sasa inapata miaka miwili na hakuna siku ambayo ameshawahi nikataza kushika simu yake na wala kunitenga kwa namna moja ama nyingine.

Nimeshangaa na ninaumia leo ni siku ya nane, tangu siku niliyoamka asubuhi na kuangalia simu yangu na kukutana na ujumbe wa mpenzi wangu akisema hataki nimtumie ujumbe wala kupigia simu.

Sikuwa tayari kuipokea hii kauli, nilipompigia simu yangu pia ilikata bila kuita ikiandika “User busy” ikimaanisha ni wazi pia 'ameniblok', nimejaribu kutuma ujumbe ila hata moja sijajibiwa.

Ninaumia sana kwakuwa sijui lipi ni kosa langu mpaka yeye kufikia kufanya maamuzi haya, ni bora basi angeniambia nina kosa hili na lile nami ningekuwa tayari kuishi atakavyo.

Hivi kweli kwa kuishi vyema mimi naye na ghafla tu anabadilika kama mimi ni adui kwake, vipi kuhusu ahadi yake kwangu na vipi maisha yangu niliyomuamini na kumtambulisha kwa baadhi ya ndugu zangu na marafiki zangu ooh Mungu nipe nguvu ya kuikabili hii hali.

Nilijaribu kuazima simu ya rafiki yangu na kumpigia lakini aliposikia tu sauti yangu alikata na kuzuia namba ile pia. Kwanini asiniweke wazi mimi nilichomkosea nikawa huru katika hii Dunia? Ni ipi kasoro yangu katika mapenzi ikiwa alinisifia kuwa mimi ni bora kwake kuliko X zake wanne?

Natamanai kuyaanza maisha mapya lakini nakosa amani ninapowaza kwanini ameniacha bila kuniambia makosa yangu. Kwanini ? Kwanini mpenzi?

20221031_095948.jpg
 
Sijasoma kitabu chote lakini ngoja niandike jibu nililopata automaticaly kabla sijalisahau, alafu niendelee kosoma.
iko hivi;-
kuna sehemu alikukuta/ alikuona ukifanya kitu m-bad, wewe mwenyewe wajua.

huenda ni mtu mwenye hasira kama mimi hapa, so hajaona sababu ya kugombana na wewe.
ushauri:
jitafakari, muache hvyo wala usmtafute ipo siku yeye atakutafuta hasira zikipoa (kama bado anakupenda)
 
Naomba niongee kama nabii:
1. kuna sehemu ulijisahau, ukavuka mipaka, ukatenda asiyoyapenda tena ya kumuumiza..
2. Kuna siri zako ambazo hakuzijua na sasa zmevujishwa.

mtu wako ni mkimya, ili uweze kujua yaliyo kichwani kwake nawewe kuwa mkimya.
 
Unaumia wakati hujaachwa na mimba? Ni muda mwafaka wa kuachana nae na kufanya shughuli zako za kuinua kipato. Tafuta shamba lima tikiti maji. Heka moja inakodiwa kwa 50,000 kwa msimu. Heka moja yanatasha mashina 1,500. Yakiota kila shina linakuwa na matunda mawili hadi matatu. Bei ya sokoni ni 1,000 hadi 1,500 so mashina 1500 × matunda 3 kila shina × 1000 bei ya kila tunda sokoni utakuwa tajiri ndani ya miezi 4 tu na huyo mpenzi ataanza kujipendekeza tena kwako
😀😀😀😀
 
wewe umejuaje kuwa yeye sio tajiri?
umejuaje kwamba hana pesa?

mshauri kimahusiano sio kiuchumi.
huyo dada anaweza kuwa anakuzidi pesa ujue!
 
Jbu mswali Yangu Ili tunzie hapo.

1. Je tangia mumenza uhusiano. Uli mcheat mara ngapi.

2. Sema Siri ya mahusiano ambayo hukuwahi kumwambia. Jarib kukumbuka.

3. Una shughul gani ya kukuingizia kipato, au kama unamtegemea yeye sema
 
Kauli hii ni kauli inayonichanganya sana. Mimi ni msichana, nimekuwa na mahusiano na mpenzi wangu sasa inapata miaka miwili na hakuna siku ambayo ameshawahi nikataza kushika simu yake na wala kunitenga kwa namna moja ama nyingine.

Nimeshangaa na ninaumia leo ni siku ya nane, tangu siku niliyoamka asubuhi na kuangalia simu yangu na kukutana na ujumbe wa mpenzi wangu akisema hataki nimtumie ujumbe wala kupigia simu.

Sikuwa tayari kuipokea hii kauli, nilipompigia simu yangu pia ilikata bila kuita ikiandika “User busy” ikimaanisha ni wazi pia 'ameniblok', nimejaribu kutuma ujumbe ila hata moja sijajibiwa.

Ninaumia sana kwakuwa sijui lipi ni kosa langu mpaka yeye kufikia kufanya maamuzi haya, ni bora basi angeniambia nina kosa hili na lile nami ningekuwa tayari kuishi atakavyo.

Hivi kweli kwa kuishi vyema mimi naye na ghafla tu anabadilika kama mimi ni adui kwake, vipi kuhusu ahadi yake kwangu na vipi maisha yangu niliyomuamini na kumtambulisha kwa baadhi ya ndugu zangu na marafiki zangu ooh Mungu nipe nguvu ya kuikabili hii hali.

Nilijaribu kuazima simu ya rafiki yangu na kumpigia lakini aliposikia tu sauti yangu alikata na kuzuia namba ile pia. Kwanini asiniweke wazi mimi nilichomkosea nikawa huru katika hii Dunia? Ni ipi kasoro yangu katika mapenzi ikiwa alinisifia kuwa mimi ni bora kwake kuliko X zake wanne?

Natamanai kuyaanza maisha mapya lakini nakosa amani ninapowaza kwanini ameniacha bila kuniambia makosa yangu. Kwanini ? Kwanini mpenzi?View attachment 2427130
Pole, ila usiwe mbinafsi kujiangalia wewe tu… maana naona unajiulza “kwanini mimi, Kanionaje, vipi ahadi zake kwangu n.k” fikiria what if he’s a dumb selfish moron?, vipi kama si mtu wa kuridhika wa kutangatanga kas na kus, vipi kama hakustahili msichana mzuri kama wewe?

Hiko unachokipitia ni suala la kisaikolojia, that is a fear of unknown, naelewa ni hali ngumu sana ila ushauri wangu if u have to cry find a place with your trusted buddies then liiia hamu yako, if you want someone to talk to find someone you trust (u can contact me) kisha ongea yote nyongo ikuishe.

Ni suala la muda sumu ikiisha utajisikia vizuri tena, ila never forgive that Dick, ni wazi he don’t deserve u.

(Kwa asilimia 80 ninajua huwezi msahau, na atakukaa sana kichwani)
 
Mkuu ..wewe ni mnasihi au mshauri
 
Back
Top Bottom