Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,582
- 6,627
Wakuu,
Huenda Kabendera akawa huru leo baada ya Hati ya Mashtaka kufanyiwa marekebisho.
Baada ya Erick Kabendera kukubali makosa, Upande wa Serikali wamemsomea Mashtaka Rasmi.
Mashtaka hayo ni pamoja na Uhujumu Uchumi pamoja na Kukwepa Kodi baada ya kosa la kuongoza Genge la Uhalifu kuondolewa Rasmi na Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).
UPDATE:
Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP) ameridhia maombi ya mwandishi wa habari, Erick Kabendera kukiri mashtaka yake na kuomba msamaha. Alikuwa anakabiliwa na mashtaka 3 likiwemo la kutakatisha fedha, TSh. Milioni 173.
Aidha, DPP amewasilisha hati ya kuiruhusu Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu kusikiliza kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi huyo.
=====
FINAL UPDATE:
Kabendera aachiwa huru
Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imemuachia huru mwandishi wa Habari za Uchunguzi Erick Kabendera.
Katika hukumu iliyosomwa na Hakimu Janeth Mtega imemtaka mtuhumiwa Erick Kabendera kulipa kiasi cha pesa za kitanzania shilingi laki mbili na elfu 50 (250000) au kutumikia kifungo cha Miezi mitatu jela. Adhabu hiyo inaambatanana fidia ya Shilingi za kitanzania Milioni 172, hii ni kwa kosa la kushindwa kulipa kodi.
Kosa la pili limemtaka Erick Kabendera kulipa faini ya shilingi za kitanzania Milioni mia Moja (Mil 100) hii ikiwa ni adhabu kwa kosa la Utakatishaji fedha katika kesi ya Uhujumu uchumi inayomkabili.
======
Agreeement
=====
Pia, soma:
1). Kisutu: Erick Kabendera afikishwa mahakamani, upelelezi dhidi yake haujakamilika
2). Kisutu: Erick Kabendera ashtakiwa kwa Kujihusisha na mtandao wa uhalifu, ukwepaji kodi na kutakatisha fedha haramu
3). Mwandishi wa Habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera aomba msamaha kwa Rais Magufuli
4). Rais Magufuli: Waliopo mahabusu kwa kesi za uhujumu uchumi, kama wapo tayari kuomba msamaha na kurejesha pesa, kama Sheria inaruhusu nashauri waachiwe