Kuanzia leo chochote nitakachonunua nitadai risiti

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,701
71,035
Kwa kweli mh. Rais amenipa hamasa ya kurudisha uzalendo na utaifa wangu baada ya kuonyesha jinsi anavyotaka kwa dhati kabisa kuijenga nchi yetu, kwa hiyo naapa kwamba kuanzia sasa hata nikinunua soda dukani lazima nidai na nipewe risiti, na kama sintopewa risiti naripoti TRA.
 
Ina maana sisi wauza michicha hatupati wateja tena ili hali tunalipa mia mbili kila siku na risit wanatupa za 2007?
 
Hivi ni risit gani zinaongelewa hapa? Ni EFD au za kuandika na mkono? Kama ni EFD mbona sehemu nyingi za biashara hazina EFD machine? Naombeni ufafanuzi tafadhali ili nijue ni wapi natakiwa kudai risit na ya aina gani.... kwa kweli lazima tuwe wazalendo kumuunga mkono Rais wetu.
 
Wema Sepetu mbona hana EFD Machine? Muulize Idrissa kama kishawahi kupewa risiti?
 
Hivi ni risit gani zinaongelewa hapa? Ni EFD au za kuandika na mkono? Kama ni EFD mbona sehemu nyingi za biashara hazina EFD machine? Naombeni ufafanuzi tafadhali ili nijue ni wapi natakiwa kudai risit na ya aina gani.... kwa kweli lazima tuwe wazalendo kumuunga mkono Rais wetu.
EFD znaenda kwa awamu... na kuna level ya biashara ndo wameanza nazo.
 
Inaonekana wewe unahemea supermarket maana kama ni kama sisi wa huku uswazi kuna vitu vinauzwa bei yake ndogo kuliko gharama ya kutengeneza hiyo risiti, sasa sio rahisi kupewa
 
Kwa kweli mh. Rais amenipa hamasa ya kurudisha uzalendo na utaifa wangu baada ya kuonyesha jinsi anavyotaka kwa dhati kabisa kuijenga nchi yetu, kwa hiyo naapa kwamba kuanzia sasa hata nikinunua soda dukani lazima nidai na nipewe risiti, na kama sintopewa risiti naripoti TRA.
Unaonaje ukabadilisha na Avatar yako Mkuu kuhamasisha!
 
Kwa kweli mh. Rais amenipa hamasa ya kurudisha uzalendo na utaifa wangu baada ya kuonyesha jinsi anavyotaka kwa dhati kabisa kuijenga nchi yetu, kwa hiyo naapa kwamba kuanzia sasa hata nikinunua soda dukani lazima nidai na nipewe risiti, na kama sintopewa risiti naripoti TRA.

Naunga mkono hoja, nami kuanzia sasa manunuzi yoyote nahitaji risiti.
 
Back
Top Bottom