Naomba kujua kama naweza kumpeleka mtoto kuanza kidato cha tano shule ya serikali. Alishinda lakini kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu sikuweza kumpeleka. Naweza kumpeleka sasa?
Jaribu kuwasiliana na shule husika kujua kama nafasi yake bado ipo ama laa, kama nafasi bado ipo mpeleke kijana na awe tayari kupambana kweli ili kufidia wenzake walichokwisha kukisoma
Itatokana na sababu zako Kama zina msingi mkuu atakuelewa. Jaribu kwenda kuongea. Pamoja kuwa muda umepita ila mkuu wa shule ni binadamu anaweza kukusaidia Akampa nafasi