Kuandikisha mtoto darasa la kwanza 55,000/=

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,844
Reaction score
10,768
Wakuu ndiyo hali halisi. Nina ndugu yangu anayeishi Morogoro mjini. Kwa kiasi cha wiki mbili sasa amekuwa akihangaika kutafuta 55,000/= ili aweze kumwandikisha mtata wake darasa la kwanza katika shule ya msingi Maghorofani. Basi jana nikampigia kwa lengo la kutaka kumjulia hali, katika maongezi yetu ndio akanigusia kuwa ameamua kuachana na wazo la kumsomesha huyo mwanae kwa vile hawezi kupata hizo hela. Kwa kweli nimesikitika sana na kesho nimepanga kufika wizarani kupata ufafanuzi. Jamani kuna watanzania wangapi wanashindwa kuwapeleka watoto wao shuleni kwa mambo kama haya???
 
Fuatilia kwanza ndiyo uje hapa we unaandika kama unauhakika mbona mie nimemwandikisha bure
 
Kweli wewe ni aspen
27ad49839b8c2a418b91469f2816a075.jpg

party_cigarettes.jpg
 
Last edited by a moderator:
hiyo fedha ni kwa ajili ya nini? waulize pata ufafanuzi, usimnyime mtoto haki yake. si umesema anakaa morogoro mjini, anao uwezo wa kutoa hiyo fedha cha msingi ajue anatoa kwa ajili ya nini?
 
Kwani kila anayeishi mjini anaweza kutoa kiasi hicho cha pesa?
 
mkuu, maelezo ni mengi lkn umechukua eneo dogo tu, lisilo na ufumbuzi, naomba fuatilia na uwajuze wana jf, anatakiwa atoe hiyo fedha kama rushwa, ada ya kuandikishwa , kwa ajili ya unifomu, dawati, ujenzi wa madarasa/choo au kwa ajili gani? kwa kujibu swali lako mkaazi wa mjini kama morogoro mjini ana uwelewa wa kutosha kujua mahitaji ya mwanae kwa tukio kubwa kama hilo la kuanza shule.
 
Mkuu kwa ufahamu wangu mdogo michango ya aina hii ishapigwa marufuku. Sijui unaongelea Tanzania ipi.
 
ni kweli michango mbalimbali imekatazwa ktk shule hizi za umma, lkn uongozi wa shule kwa kushirikiana na kamati za wazazi, hupanga mikakati kwa ajili ya kutunisha mifuko ya shule zao, likiwemo suala la unifomu kwa maana ya kaptura , shati na t-shirt, vyote vikiwa na nembo ya shule husika. tatizo pia wazazi wengi au wananchi wengi hawapendi kuhudhuria vikao halali vya shule zilizo ktk maeneo yao, vikao husaidia, kuelekeza, kukosoana na kufahamiana lengo likiwa shule yetu, waalimu wetu, wazazi wetu.
 
Mkuu, ulifika wizarani as promised? Tunaomba feedback basi tujue pa kuanzia.
 
ni kweli michango mbalimbali imekatazwa ktk shule hizi za umma, lkn uongozi wa shule kwa kushirikiana na kamati za wazazi, hupanga mikakati kwa ajili ya kutunisha mifuko ya shule zao, likiwemo suala la unifomu kwa maana ya kaptura , shati na t-shirt, vyote vikiwa na nembo ya shule husika. tatizo pia wazazi wengi au wananchi wengi hawapendi kuhudhuria vikao halali vya shule zilizo ktk maeneo yao, vikao husaidia, kuelekeza, kukosoana na kufahamiana lengo likiwa shule yetu, waalimu wetu, wazazi wetu.

Sijakuelewa unachozungumza. Mzazi ndo anakwenda kuandikisha mwanawe, anaambiwa bila 55,000/= hakuna nafasi, unasema shule zinapanga? Tangu lini kuna mwongozo kama huu? Nchi hii inayumba si kwa sababu ya akina Rostam tu, ni pamoja na mitazamo kama hii ambayo haipo katika taratibu za kiserikali. ADA YA KUANDIKISHA WATOTO!!! Tunaandaa taifa la mambumbumbu. Kama wewe unaona 55,000/= ni pesa ya chai wengine amount hiyo ni muujiza. Hebu toka "Masaki" uingie uswazi kidogo, huku kwetu watu hutoana roho kwa ugomvi wa shilingi 200 tu, sembusse 55,000? TUSIJISAHAU kwamba kuna watu wanasota na kudhani kila mtu anaishi paradiso.
 
sijakukatalia mkuu yote ,unayosema ni sahihi kabisa, lkn muulize amehoji hiyo pesa ni ya nini? anatoa hiyo fedha ifanyie nini? tujiulize tunapenda kuudhuria vikao vya wazazi? sehemu ambayo tunafursa nzuri ya kuhoji hayo yote na kutoka na maazimio ya kuwapongeza au kuwaadabisha watendaji au tubaki tunalalamika kwa majungu jiulize Rostam unamuingizaje hapa, UNASEMA hujanielewa kwa sababu HUJANIAMBIA ; ameambiwa hiyo fedha ni kwa ajili ya kufanyia nini? mimi nimejaribu kujifikirisha labda , RUSHWA. MCHANGO WA MAJENGO,UNIFORM baada ya hapo ndo nichague upande lkn mkuu yale ninayojifikirisha ili nipate moja ww unaona ndo maamuzi. mf; kama ni hilo la rushwa jiulize halina tiba hapo moro.
 
Aleyesoma tu hiyo amount ashaelewa. Mchango wa uniform? Unadhani hii ni St..... primary school mpaka iwepo ada ya uniform? Umesoma shule gani wewe, St. Madalena eeeh! Madawati? Majengo? Usinshangaze, yaani wazazi wabanwe kwenye kuandikisha? Kwamba bila kutoa pesa, hakuna kuandikishwa? Kwa vikao vipi? Haki ya kupata elimu iko wapi? Kama unadhani ni majungu well and good, ila nimeshakusoma vizuri tu tangu post yako ya kwanza. Hizi shule huzijui wewe, ndo maana unaleta experience za international, mnakonunua shati jeupe na kaptula ya khaki kwa 55,000/=.
 
Wakuu ndiyo hali halisi. Nina ndugu yangu anayeishi Morogoro mjini. Kwa kiasi cha wiki mbili sasa amekuwa akihangaika kutafuta 55,000/= ili aweze kumwandikisha mtata wake darasa la kwanza katika shule ya msingi Maghorofani. Basi jana nikampigia kwa lengo la kutaka kumjulia hali, katika maongezi yetu ndio akanigusia kuwa ameamua kuachana na wazo la kumsomesha huyo mwanae kwa vile hawezi kupata hizo hela. Kwa kweli nimesikitika sana na kesho nimepanga kufika wizarani kupata ufafanuzi. Jamani kuna watanzania wangapi wanashindwa kuwapeleka watoto wao shuleni kwa mambo kama haya???

Watanzania lazima tubadilike na kwenda na wakati.
Kama jamaa yako alijua hana uwezo wa kumtunza mtoto kwa nini alimzaa?
Kwani mtoto slipatikana kwa bahati mbaya au alipangwa kuzaliwa.
Tuanze kuondokana na dhana kwamba mtoto ni kudra ya Mungu tusnze kupanga uzazi.
Halafu utasikia mtu kama huyo a,baye mtoto mmoja tu anamshinda anazaa watoto sita jumla.

Huo ni umsikini wa kujitakia na kurithisha vizazi vingine umasikini huo huo.
 
Poor me! Kwa hiyo ni wazazi tu wako ndo waliostahili kuzaa kwa kuwa wanauwezo? Very illogical, watu hutoka katika utajiri hadi umaskini and vice versa. Ukidhani wewe leo ni mjanja kumbuka kwamba kuna kesho. Ndiposa ajidhaniye amesimama aangalie asije akaanguka. Halafu kwa upeo finyu umemiss point nzima ya thread hii, suala la huyu ndugu siyo exceptional case, hivyo litazamwe kwa mapana yake. But mind you, ni kwa wale wanaotambua hali ya watanzania wengi zaidi nchini na si wale waliokulia Masaki wakijua kila mtanzania ana hali sawa ya maisha. Be a bit logical.
 
Mkuu hizo ndio realities of life.
Huko China baada ya kuona watu wao ni wagumu kuelewa ilitungwa sheria ya kuzaa mtoto mmoja tu!

Mafanikio yao tunayaona na swala si la matajiri wala masikini.
Simple logic ni kuwa midomo mitatu ni ghali zaidi kuilisha kuliko mdomo mmoja.
Katika dunia ya leo ya watu wanaoishi mijini, ni mtu mwenyewe anayeweza kupanga mafanikio yake, uwe masikini au tajiri.Hata tajiri akijizalia watoto kumi na uwezo wake ukiwa ni wa mtoto mmoja tu, yeye vile vile anaukaribisha ufukara.

And thats very logical.
 
Katafiti tena sababu ya wachina kupanga idadi ya watoto. Halafu uelimike ni kwa nini wanakijiji waruhusiwe kuzaa watoto wawili ilhali matajiri wa mjini kama wewe wazae mtoto mmoja tu. Usikariri tu. Otherwise kushupalia kuwa eti ada za kuandikisha watoto kwenye shule za awali za public ni akili za kifisadi, nothing less. Wakati mawaziri wenye mtazamo mpana wanadai elimu bure inawezekana, mtoto wa fisadi anahoji sababu ya raia mmoja kuzaa mtoto mmoja tu. Sijui alipaswa kufunga uzazi!? Na kesho wewe ndo unakuwa waziri, maana nchi hii haiishiwi na maajabu!
 
Mh Mulugo akiongea na ITV alitoa ruksa kwa michango kutozwa mashuleni ikiwa tu imeithinishwa na KAMATI YA SHULE HUSIKA.
 
Back
Top Bottom