Kuambatana! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuambatana!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Apr 17, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Kuambatana!  Wanahitaji kuongea uso kwa uso!
  [​IMG]
  Tumeona kwamba mwanamke anatakiwa (lazima) amheshimu mume ili mume naye ampende na matokeo yake kila mmoja aridhike na mwenzake na hatimaye kuwa na uhusiano mzuri idara zote.
  (Efeso 5:33)
  Mke anahitaji mume anayempenda na kumuonesha upendo kuanzia asubuhi, mchana na jioni wakikutana mume anahitaji kuwa karibu na mke wake ili mke ajisikia anapendwa na hatimaye ajisikie relaxed na kuwa tayari hata kwa activities zingine usiku.
  Je, mume kuwa karibu na mke wake ina maana gani?
  Maana ya kuwa karibu kwa mke na mume ni kuambatana, shikamana, kushikana, ng’ang’aniana, fungamana, kaa jirani jirani, songamana, karibiana, kuwa pamoja (cleaving, cling or intimate)
  Kuwa karibu ni kuungana uso kwa uso na kuwa mwili mmoja.
  “Kwa sababu hii mwanaume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja”.
  (Mwanzo 2:24)
  Katika uimbaji wa Mungu ni Binadamu peke yao ambao huweza kuwa karibu kimapenzi (sexual intimate) uso kwa uso.
  Kuambatana kati ya mke na mume ni zaidi ya kuwa mwili mmoja.
  Kuambata kwa mke na mume ni kuwa karibu au mwili mmoja kiroho na kimwili.
  Kama wewe ni mwanaume inakupasa ufahamu kwamba mke wako hufurahia na kujiona anapendwa na wewe pale unapomkaribia na kufanya ajione unataka kuwa karibu kwa namna unavyomtazama, unavyomgusa, unavyomkumbatia, unavyotabasamu na kumbusu na kumwambia NAKUPENDA.
  Katika ulimwengu wa sasa (modern world) ni rahisi sana kwa mke na mume kuchukuliwa na kuwa busy na kujisahau kujenga ukaribu ambao ndiyo msingi wa mwanamke kujisikia anapendwa na mume wake.
  Wanandoa wenye busara huchukua dakika si chini ya 15 kila siku wakikutana jioni baada ya kazi; huhakikisha kila mmoja anajihusisha na mwenzake kwa ukaribu wa kimaongezi na sharing ya information za namna siku ilikuwa kwao wote na matokeo yao jioni na usiku vinakuwa exciting.
  Mke akirudi anataka connections, anataka involvement na mume, anataka face to face talks na Mume akirudi kazini anataka kwenda pangoni hata hivyo jambo la msingi ni mwanaume kuhakikisha anapata muda wa kutosha ili kufanya connection na mke na hasa kama unataka mambo yawe safi kuanzia jikoni, sebuleni hadi chumbani huo usiku pia usigande kwa TV au Gazeti au pangoni bila kuongea na mke na kusaidia kazi ndogondogo hapo nyumbani.
  Kuna ubaya gani kama utakuwa unapiga story na yeye anaandaa dinner au na wewe unasaidia kupika (kama hamna wafanyakazi wa ndani)
  KUMBUKA KUWA KARIBU NA MKE SI GHARAMA BALI MUDA:
  Mke atafurahi kama mara kwa mara:
  Utamshika tu mikono,
  Utamkumbatia na kumbusu wakati wowote,
  Unapokuwa affectionate bila wazo la sex,
  Kufanya kitu kinachosaidia kuwa na “togetherness”
  Pale unapomwambia unampenda, yeye ni mwanamke mzuri (mrembo).
  Kumbusu mke kwa sababu unataka sex tu ni turn off.
  Pale mnapoangaliana na kupeana story zinazowafanya kuwa na kicheko.
  Unapotumia muda wa kutosha kuwa na yeye katika kazi ndogondogo kama kupika, kufua nguo, kuogesha watoto, kusafisha nyumba nk.
  Pale unapomfanya ajisikie unafurahia kujadili vitu mbalimbali na yeye.
  Pale unapoendelea kuongea naye, au mkumbatia na mbusu baada ya tendo la ndoa.
  Tutaendelea......
   
 2. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #2
  Apr 17, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Daa Pdidy leo umetuamulia.ni shule kwa kwenda mbele,asante sana.
   
 3. kitalolo

  kitalolo JF-Expert Member

  #3
  Apr 17, 2010
  Joined: Dec 4, 2006
  Messages: 1,846
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135


  lakwangu nilimelifanyia yote lakini ndio likaanza kuniona ngombe, kondoo, mbuzi, yaani hata kitandani namwona kama maiti tu
   
 4. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #4
  Apr 17, 2010
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnh pole kitalolo
   
Loading...