Kuagiza gari japani

Kaitaba

JF-Expert Member
Jun 30, 2009
916
52
Habari za leo,

Kama kichwa cha habari kinavyosema .Mimi natafuta wakala ambaye anahusika na uwakala wa kutuma magari Japani kuyaleta hapa nchini.
 
Nimejaribu kufuata taratibu nikaambiwa niwaone jamaa wa makunganya, nikaskuta, iweje nawasiliana na japani halafu niwasiliane na makunganya.
 
It is easy siku hizi. Unaingia kwenye mtandao unafanya search ya gari unayotaka then mnakubaliana price na muuzaji. Mkishakubaliana atakutumia proforma invoice kwa ajili ya kufanya malipo benki.
Wakishapokea pesa yako wataanza inspection then wata-book usafiri wa meli kuileta bongo.
Mchakato unaweza kusubiri hata 5 weeks.
Watakutumia bill of lading na documents zingine baada ya kusafirisha af wewe utatakiwa kusubiri.
Ikifika, utatafuta wakala wa kukusaidia kutoa gari na kufanya registration. Then the car is yours

Angalizo:
Kuna mitandao mingine ina matapeli so ni muhimu kupata reference kutoka kwa watu waliowahi kuagiza.
Kwenye clearance hapo bandarini kuna matapeli pia wanaweza kukutolea gari lako kama kontena la maziwa. Utakuwa unaendesha gari kama transit siku una-renew road licence tra wanakudaka.
 
Mkuu maelezo yako yanaeleweka vizuri na yanatia moyo kwani nilidhani ni kazi sana kuagiza gari. Napenda pia kujua njia nzuri ya ku-deal na hao clearing and forwarding agents ni ipi,ku-address bill of landing ifikie kwa agent ama muagizaji kuipokea na kumpelekea agent?
 
Usiangaike sana, nenda katika ofisi za beforward tanzania pale karibu na hospital ya ocean road, utachagua gari, kulipia na wao wenyewe watakutolea likifika nchini kwa gharama ya 250,000 tu kwa gari dogo. Una weza cheki magari yao online www.beforward.jp na hii kampuni ndio yenye magari ya bei nafuu na usalama wa pesa zako kuliko kampuni zote jaman.
 
Usiangaike sana, nenda katika ofisi za beforward tanzania pale karibu na hospital ya ocean road, utachagua gari, kulipia na wao wenyewe watakutolea likifika nchini kwa gharama ya 250,000 tu kwa gari dogo. Una weza cheki magari yao online Japanese Used Cars | BE FORWARD na hii kampuni ndio yenye magari ya bei nafuu na usalama wa pesa zako kuliko kampuni zote jaman.

Bei nafuu sawa maana magari mengi(sio yote) ya be forward Ni mabovu ndio maana yanauzwa bei rahisi kama sio mabovu basi Ni magari yaliyopata ajali either ndogo au kubwa..kuhusu usalama sio kweli kwamba be forward pekee ndio wapo salama 100%, hata baadhi ya makampuni mengine kama sbt Japan, na PIA ukinunulia tradecarview PIA carview corporation pia wapo salama, so kapuni salama Ni nyingi na zina magari mazuri tu
 
Ni kweli Nokla usemacho, ila kwa mtu anayeanza kutaka kuagiza gari nje ni vizuri akapata feedback kutokana na uzoefu wa mtu fulani. Beforward na kampuni nyingine wote wana magari tofauti tofauti ktk ubora na ndio maana wanaweka picha ili mteja mwenyewe achague. Kwa huyu ndugu anayetaka kuanza kuagiza nafikili kwa ushauri niliompa unaweza kuwa mzuri kwake.
 
Back
Top Bottom