Willy Johnson
JF-Expert Member
- Aug 29, 2016
- 316
- 156
Habari wana jf. Mimi ni mfanyabiashara wa duka la rejareja Mbezi kimara, sasa nilichokiona kwa sasa katika biashara ni kila mteja akija anakuja na elfu kumi au elfu tano wanaokuja na hela ndogondogo ni wachache kiasi ambacho ukichukua hizi hela ndogo ukiwapa hawa wa elfu kumi au tano, wateja wanaofuatia wa elfu kumi au tano wanakosa sasa hii tuiteje ni kwamba hela ndogondogo zimebanwa katika mzunguko zimeachwa kubwa au ndio hali ya uchumi imekuwa ngumu, naomba niwasilishe watalaamu wa uchumi watueleze hili limekaaje?