Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 359,882
- 828,446
By Malisa GJ,
Mwaka 1965 aliyekuwa Rais wa Romania Gheorghe Gheorghiu-Dej, alifariki dunia akiwa madarakani. Kwa mujibu wa Katiba yao, Rais akifia madarakani, Katibu mkuu wa chama cha kikomunisti (PCR) anarithi kiti chake. Hivyo ndivyo Nicolae Ceaușescu alivyopata bahati ya kuwa Rais wa Romania bila kutarajia. Urais wa mirathi.
Alipoingia alijaribu kuonesha yeye ni tofauti na mtangulizi wake. Aliachilia huru baadhi ya wafungwa wa kisiasa, kuanzisha maridhiano na wapinzani, kuendeleza miradi ya mtangulizi wake, hasa ujenzi wa nyumba za bei nafuu (affordable housing).
Alitekeleza miradi mingi ya ujenzi kiasi kwamba hakuona hatari ya kukopa fedha nyingi nje ya nchi ili kujenga. Lakini kumbe alifanya ufisadi mkubwa kupitia miradi hiyo. Sehemu kubwa ya fedha zilirudi kupitia kampuni zake au za ndugu zake. Alipandisha deni la Romania kutoka dola bilioni 1 mwaka 1965 hadi dola bilioni 5 mwaka 1970. Yani deni la taifa liliongezeka mara 5 ndani ya miaka mitano tu.
Madeni hayo yalitokana na kukopa pesa nje ya nchi zenye riba kubwa. Kwahiyo alilazimika kuanzisha tozo na kodi mbalimbali ili serikali ipate pesa za kulipa madeni. Wananchi wa Romania walinuka kodi na tozo, kiasi kwamba baadhi walikimbilia nchi jirani kama Serbia na Hungary. Alianzisha kodi hadi kwenye mazao ya chakula kiasi kwamba gharama za chakula ziliongezeka maradufu na watu wengi walishindwa kumudu hata mlo mmoja. Lakini alifanya hivyo ili kupata fedha za kulipa madeni.
Polepole Ceaușescu alianza kubadilika kutoka kiongozi wa maridhiano na kuongoza nchi kwa mkono wa chuma. Hakutaka kukosolewa wala kupingwa. Wale waliojaribu kufanya hivyo walipotea, kutekwa, kuuawa kikatili na miili yao kuokotwa ufukweni, na wengine walifungwa jela kwa makosa ya uhaini.
Kwa mujibu wa taarifa ya CIA iliyoachiliwa mwaka 2010 “Romania: A Situation Report” ilionesha kuwa hadi mwaka 1980 Rais Ceaușescu alikuwa na kikosi cha siri cha zaidi ya watu elfu 70 (wasiojulikana) ambao walihusika kuua, kuteka na kufungulia watu mashtaka ya uongo. Kikosi hicho hakikuwa katika mfumo rasmi unaotambulika, kwa hiyo kiliweza kufanya ukatili wa aina yoyote bila kuwajibishwa.
Miili ya watu waliomkosoa Rais Ceaușescu iliokotwa katika fukwe za bahari nyeusi (The Black Sea) ikiwa na majeraha. Polisi walisema uhalifu huo ulifanywa na watu wasiojulikana na kuahidi kuwatafuta lakini hakuna muuaji aliyewahi kukamatwa.
Matukio hayo yaliendelea kushamiri, watu walikamatwa mchana kweupe wakiwa maofisini, kwenye biashara zao, au kwenye vyombo vya usafiri na kwenda kuuawa. Rais Ceaușescu hakuwahi kukemea wala kuonesha kusikitishwa na vitendo hivyo.
Katika kuimarisha utawala wake wa kiimla Rais Ceaușescu alihakikisha amezicontrol mahakama na bunge vikawa vyombo vya kutekeleza maagizo yake badala ya mihimili inayojitegemea. Bunge likageuka mwanasesere wa kumsifia Rais na mahakama ikapoteza uhuru wake na kuwa chombo cha kufanya maamuzi kwa kumfurahisha Rais.
Katika giza hilo totoro, makanisa nayo yakageuka kasuku wa kuisifia serikali badala ya kusimamia haki. Kanisa la Orthodox la Mashariki lenye waumini wengi zaidi nchini humo (zaidi ya 80%) likawa linatoa nyaraka za kumsifia Rais na kuwataka wananchi kutii mamlaka maana mamlaka zote zinatoka kwa Mungu.
Ili kulicontrol bunge vizuri, Ceaușescu alijenga bunge kubwa la kifahari (pichani), ambalo ni bunge la pili kwa ukubwa duniani baada ya Pentagon, likiwa kwenye eneo la kilomita za mraba 365 ambalo ni kubwa zaidi ya nchi yote ya Malta.
Lakini kaskazini magharibi mwa nchi hiyo katika mji wa Timișoara kulikuwa na Kanisa la Kilutheri lililokuwa likiongozwa na Mchungaji Laszlo Tokes. Alikuwa mmoja wa watu wachache waliothubutu kuikosoa serikali ya dikteta Ceaușescu hadharani. Alikosoa kukithiri kwa vitendo vya ufisadi, kukosekana kwa uhuru wa kuabudu (makanisa kufungwa), wapinzani kutekwa, kupotea, kuuawa na wengine kupewa kesi za uhaini.
Pia Mchungaji Tokes alipinga mauaji ya kabila la Wamagyar yaliyoendeshwa na kikosi cha siri cha Rais Ceaușescu. Katikati ya mamilioni ya wananchi waliokuwa wakimsifu Ceaușescu na kumnyenyekea, Mchungaji Tokes alisimama imara kumkosoa. Alipewa onyo na mamlaka kuwa aache kuchanganya dini na siasa, lakini hakutii. Aliendelea kukosoa na kupinga vitendo vya utekaji, kufunga makanisa, ufisadi etc.
Tar 15 Disemba 1989 Serikali ilifunga Kanisa la Mchungaji Tokes. Rais Ceaușescu akamuita wakala wa Shetani na akaagiza akamatwe. Baada ya amri hiyo, waumini na majirani zake walizingira nyumba yake ili kuzuia askari kumkamata.
Hadi Disemba 16, polisi walikuwa hawajafanikiwa kumkamata Mchungaji Tokes. Rais Ceaușescu akatoa amri ya kuua mtu yeyote aliyekwamisha zoezi hilo.
Polisi wakamimina risasi kama njia ya kuwatawanya wananchi. Siku ya kwanza wakaua watu 106 na kutishia kuua zaidi kama hawatatawanyika kwa hiyari. Lakini kadri polisi walivyotumia nguvu ndivyo waandamanaji walivyoongezeka.
Maandamano yakashika kasi na kuhamia miji ya Cluj-Napoca, Brașov, Constanța, Galați na hatimaye yakafika mji mkuu Bucharest.
Hayakuwa tena maandamano ya kuzuia Mchungaji Tokes kukamatwa bali kupinga utawala dhalimu wa Rais Ceaușescu. Kile kilichoanza kama maandamano ya kidini kilibadilika kuwa maandamano ya kupinga serikali.
Rais Ceaușescu akaamuru waandamanaji wadhibitiwe kwa nguvu na ikibidi wauawe. Polisi na jeshi wakatumia risasi na mabomu. Vifaru vya jeshi vikaingia mtaani kukabiliana na waandamanaji. Watu 1,300 waliuawa ndani ya siku 3. Mauaji hayo yalichochea hasira zaidi kwa wananchi na kuingia barabarani.
Jeshi lilianza kukataa amri za kupiga raia, lakini Polisi waliendelea kupiga. Jeshi likabadilika na kuanza kulinda raia na kuzuia polisi kutumia nguvu. Disemba 21, maandamano yalifika Ikulu ya Bucharest, ambapo Rais Ceaușescu alijaribu kuhutubia lakini hotuba yake ilivurugwa na kelele za upinzani. Ilikuwa mara ya kwanza hotuba ya Rais kuingiliwa moja kwa moja hadharani.
Tar 22 Disemba 1989, Rais Ceaușescu na mkewe Elena walijaribu kutoroka lakini walikamatwa na kuletwa mbele ya umati wa watu wakizomewa kuwa ni wauaji na mafisadi.
Walishtakiwa katika mahakama ya kijeshi (military tribunal) ambapo kesi ilisikilizwa kwa siku 3 tu. Walipatikana na hatia na kuhukumiwa kifo.
Tar 25 Desemba 1989 Rais Nicolae Ceaușescu na mkewe Elena waliuawa kwa kupigwa risasi hadharani huku wananchi wakishuhudia na kushangilia. Na huo ukawa mwisho wa utawala wa dikteta Nicolae Ceaușescu. Siku hiyo ikapewa jina Krismasi ya Uhuru (Crăciunul Revoluționar).!
Umejifunza nini?