Kovu la kufinywa shavuni mpaka leo lipo

Kovu la kufinywa shavuni mpaka leo lipo

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
376,454
Reaction score
872,070
Ni ule umri wa under 20, full utundu nikawa nakanyemelea kabinti nyumba ya jirani, kila wakienda kulala mimi nanyata mpaka dirisha la chumba chake nalisukuma nazama ndani kimyakimya tunamaliza yetu nachomokea dirishani naenda kwetu kulala mwepesiiiii

Kumbe bwana ule mchezo ukashtukiwa na mamaake bila sisi kujua, basi siku usiku kama kawa nikajivuta mpaka dirishani nikalisukuma likafunguka nikazama ndani mpaka kitandani! Ile kuinama tu nimguse nikajikuta mashavu yote mawili yamepigwa vitasa kisawasawa na mikono yenye nguvu
Sikuchelewa kugundua yule ni nani na nimenasa mtegoni, kipigo kilikuwa kimyakimya mama yule alikuwa haongei bali kufinya tu,halafu akaniburuza hivyohivyo mpaka dirishani akaniacha kupata tu ule mwanya nikaparamia dirisha huku nyuma nikasindikizwa na bonge la bao mgongoni
Niliugulia maumivu usiku kucha lakini mbaya zaidi nitasemaje asubuhi kwa wazazi? kufika asubuhi najiandaa kutoka nje nikawapige skonyo wazazi namwona yule mama keshafika mlangoni kwetu niligeuka na kutokea mlango wa nyuma kwa kasi ya supersonic,tangu siku ile Ilikuwa nikimwona yule mama popote mimi ni mbio tu
 
mshana jr una mikasa mingi kweli ila mingine huwa unasimulia ya marafiki na majirani
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom