Kova: Maandamano ya DOWANS kesho marufuku!

Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!!

Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns.....

Eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM.....

Najisikia kuanza kulia.....
Hili tishio la dowans hajawahi kuliona hata kidogo?
 
Reactions: Nzi
Kwa hiyo anataka kuthibitishia kwamba al shabab wapo ndani ya nchi yetu?

Nini chanzo cha tishio lao?

Tumevamia nchi yao?

Na leo baada ya nyoka kuingia ndani ndio wanaamkaa?
 
Tatizo hawa maitelijensia wetu wanafikiria kwa masaburi! Vitu vya muhimu kwa Taifa kwao havina umuhimu...
 
Kuna uhusiano gani wa kulipwa doainzi na Al Shabaab?!!

Ifike muda watawawala wetu wawe wanafikiri kwa kutumia bongo zao badala ya kuendelea kutumia nyayo zao kufikiri!!!!!

Shwine kabisa
 
Kama hii ni kweli basi itakuwa ni kichekesho kikubwa!

Mbona watu wanakusanyika kwenye mikutano ya vyama inayoendelea ila kwenye hili la maandamano ya kupinga DOWANS ndiyo kunakuwa na tishio la Al shabab!
 
Kova unataka kutuambia Al shabab wapo nchini tayari,na je kama hivyo nvdivyo polisi wamechukua hatua gani?

Hivi anawajua Alshabab au anawaangalia kwenye TV na kuwasoma kwenye gazeti?akawaulize Uganda watampa jibu,na kama iko hivyo hatua gani zimechukuliwa kuzuia mikusanyiko?je ligi ya vodacom itasimama?je mechi ya simba na yanga nayo itaahirishwa?

Hapo wamechemka, je kwenye night club amabazo zinakuwa na watu wengi wamefanya nini kuzuia mashambulio yasitokee?makanisani na misikitini hali ya usalama ikoje?

Hapana hapo naona wanaibeba serikali kwa kuwa wao ni vibaraka wa sisiemu-magamba basi wametafuta mbinu ya kuzuia,kwani naamini ccm lingewashuka.

Jamani wa JF tutafanyaje kuonyesha hisia zetu juu ya DOWANS
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....

kwa hiyo anataka kuthibitishia kwamba al shabab wapo ndani ya nchi yetu? na nini chanzo cha tishio lao? tume vamia nchi yao? na leo baada ya nyoka kuingia ndani ndio wana amkaa?

Si jana tu bosi wake kasema kwamba wamejidhatiti kukabiliana na Al-shabab?!
Tatizo Kova anapenda sana kucheza na jukwaa; huyu mjomba toka yuko Mbeya alikua anapenda sana kucheza na media..sasa kwa vile anajua kila mTZ ana habari ya hayo maandamano anataka apate airtime kidogo hapo..
 
Pilipili shambani huyu mzee inamuwashia nini??huku TZ tunatishwaje??zaid ya kuzuia maandamano katangaza strategies gani nyingine za kujihadhari na hao al shabaab??Hao al shabaab wameanza leo???

Mbona kwenye maadhimisho ya miaka 34 ya CCM hakuzuia kusanyiko au Al Shabaab hawakuwepo??viongoz wanaofkiria kwa matumbo utawajua tu, siku zote hawakosagi sababu. Jana ilitoka taarifa kuwa maandamano hayana kibali, leo tishio la al shabaab, lipi ni lipi??

Mi nadhani atuache tu tukusanyike mana ni bora kufa kwa mashambulio ya al shabaab kuliko kufanyiwa haya tunayofanyiwa na watawala wetu mafisadi. Wangekuwa na uchungu na maisha yetu si wangefanya the needful???unafki mtupu.
 
kumbe hela zinazolipwa na dowans ni za al shabaab..!!sasa kwanini wasiseme dowans ni al shabaab moja kwa moja?.mia
 
Na wanaharakati wanaoandaa maandamano wameamuaje baada ya kova kuongea upuuzi huo??
 
Tatizo hawa maitelijensia wetu wanafikiria kwa masaburi! Vitu vya muhimu kwa Taifa kwao havina umuhimu...
Wanaona havina umuhimu kwa vile wote wanashiriki katika kulihujumu taifa kwa namna moja au nyingine. kama na wao wangekuwa wanapata shida wanazopata ordinary citizens nadhan wote tunge dance kwa tune moja.

Siku zote wanaosababisha shida kwa ordinary citizens ni wale walio kwenye system. Nadhani tusonge mbele tu mana haitakaa itokee siku watawala wakawa willing kukubali mabadiliko.
 
Tanzania tuna viongozi wa ajabu...!!! Kova kapiga marufuku maandamano ya kupinga Dowans kulipwa 111bns..... eti kwa ajili ya tishio la Al Shabab...

Source Radio Wapo FM..... Najisikia kuanza kulia.....

Haya maandamano ni ya CDM kutaka kutuvurugia amani yetu ya Tz na si lingile lolote !
 
Afadhali kama hao mababu wapo nchini ili wakatuue tu kuliko kulipa ujinga, huo upendo wake kwetu umeaanza lini? na kwanini wasiwadhibiti kimya kimya? hata hivyo tuna kitu gani sie hadi waje?

Hiyo sababu ni ya kijinga na kipuuzi maana kuna mikusanyiko mingi tu mikubwa kama kariakoo na kwingineko wanaweza kufanya tu wakitaka, mbona Tanzania inaruhusu wageni kibao na hata polisi wenyewe hawana taarifa? I will be there nimeshaomba ruhusa ya kusafiri kuja Dar kesho japo last week tu nilikua hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…