Kosa langu li-wapi?

Nyakwaratony

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2011
Posts
573
Reaction score
140
Hali zenu wanaMMU?

Miaka kadhaa iliyopita nilikuwa nafanya kazi katika Ofisi fulani hapa DODOMA alitokea baba mmoja akawa mteja wetu mzuri kiasi kwamba hawezi kumaliza siku mbili hajaja kufanya kazi zake. Hata kama hana kazi ya kufanya alipita kutusalimia. Yule baba alinipenda sana "Sio kimapenzi tafadhali" kwani nilikuwa namfanyia kazi zake vizuri.

Baada ya muda fulani alitaka kujua historia ya maisha yangu. Nilimueleza bila kuficha chochote, alisikitika akaniuliza kwanini nilikatisha masomo. Lakini baadaye alinisihi sana nirudi shule, ingawa sikuwa na uwezo kwa kurudi alinihaidi kunigharamia kila kitu. Nilirudi shule ila kabla sijamaliza kusoma hiyo elimu ya sekondari alipata uhamisho wa kikazi akahamia mkoani MOROGORO.

Hilo halikuwa mwisho wa ufadhili wake, tuliendelea kuwasiliana mpaka nikamaliza kidato cha nne. Baadae nilipata kazi nzuri nikawa na uwezo wa kuendelea na chuo kwa ngazi ya cheti. Lakini msaada wake haukuishia hapo. Aliendelea kunigharamia nusu ya ada na mimi nikawa namalizia nusu iliyobaki mpaka nikamaliza chuo ngazi ya cheti.

Aliniambia ana watoto kadhaa wakiume na wakike mmoja. Alinikaribisha kwake ambapo alikuwa akiishi na housegirl tu. Mkewe alikuwa akiishi DSM kikazi. Baada ya kuhamia mkoani Morogoro Kuna mwezi fulani nilipata likizo nikaenda kumsalimia, wanawe wawili pia walikuwa wanasoma mkoani hapo. Weekend moja alinikaribisha kwake kumbe siku hiyo pia alikuwa amewaita wanawe. Alinitambulisha kwao na kuwaeleza uhusiano baina yetu bila kuficha chochote.

Wanawe walinipokea kama mmoja wa familia, tulikaa nao pale kama watoto wa familia moja kwa muda kama wa wiki kwani nao walikuwa likizo, baada ya wiki mwanaye mkubwa aliondoka na kwenda kwa mama yake DSM, kwa vile nami nilikuwa na safari ya kwenda BAGAMOYO niliona sio vyema nipite DSM bila kwenda kumsalimia mama "mke wa yule baba" Nilianza safari mpaka DSM nilipofika sikumkuta yule mwanae kwani alikwenda MKURANGA.

Yule mama alikuwa na taarifa ya ujio wangu pale kwake. Nilifika mida ya jioni alinipokea na akafurahi kuniona kwani alikuwa akinisikia kupitia kwa mmewe na watoto. Nilillala pale kwa siku moja, kesho yake niliaga na kuondoka kwenda BAGAMOYO ili nimalizie likizo yangu na kurudi mapema kazini. Nilichelewa kutoka Bagamoyo make nilikaa kwa muda wa siku kadhaa. Nilipitiliza mpaka MORO nikaenda nikamuaga baba yangu mlezi na kurudi kazini DOM.

Maisha yaliendelea vizuri na undugu baina yangu na ile familia ulidumu, hata mwanawe yule baba aliwahi kuja kwangu yeye pamoja na mwanaye wakakaa kama wiki hivi. Baada ya mwaka hivi yule baba akafiwa na mama yake mzazi yaani bibi mlezi. Alinitaarifu kuwa "Bibi yako amefariki Mkoani Tabora hivyo mimi na mdogo wako tupo njiani kuelekea msibani. Mama yeye alitangulia.

Hapo nilijiongeza nami nikajiandaa kesho yake kuelekea msibani Tabora. Niliomba ruksa kazini nikaondoka kuelekea msibani. Tangu mwanzo wa safari nilikuwa nawasiliana na yule dada bintiye baba yangu mlezi. Mpaka nafika stendi ya TABORA nilikuwa nawasiliana na yule dada ili anipe maelekezo ya mahali msiba upo.

Nilipoteremka garini nilipigiwa simu na yule dada, nilipokea ili nipate maelekezo namna ya kufika msibani. Lahaula!!!! Nilisikia sauti tofauti na ya yule dada mara nikagundua ni sauti ya mama mkewe baba mlezi ikiniuliza kwa ukali "UNAKWENDA WAPI WEWE"?? Nikamjibu nakuja msibani mama. Akaniuliza "NANI KAKUPA TAARIFA YA MSIBA"?? Nikamjibu baba ndiye kanipa taaarifa.

Alisema maneno makali na machache "NISIKUONE KATIKA USO WANGU, NITAKUCHAFUA SURA YAKO" Nilihisi kuchanganyikiwa nisijue la kufanya ukizingatia nilikuwa mgeni Tabora. Nilitafuta mahali nikaenda kupumzika nikitafakari ni nini kosa langu. Baada ya muda nafikiri baba alitaka kujua nimefika wapi kwani ilikuwa jioni sana, sijui walizungumza nini baina yao ila yule dada alitaka kunifuata mahali nilipo ili niende msibani. nilijitetea kuwa nilikuwa mahali salama nimepumzika nitaungana nao kesho yake. Walikubali kwa shingo upande.

Nililala pale mpaka kesho yake, asubuhi niliondoka kurudi Dodoma bila kuwaaga wala kwenda msibani kwani niliogopa huenda yule mama alilazimika ku-calm down pasipo ridhaa yake na angeweza kunifanya chochote kile. Walipomaliza msiba walirudi Moro ya yule mama alirudi DSM. Baada ya kama siku tatu yule dada alinipigia simu kunilaumu kwamba mimi naharibu ndoa ya wazazi wake.

Kiukweli sikumuelewa alikuwa anamaanisha nini, nilipomuuliza alijibu kuwa najifanya sijui na maneno chungu mzima. Nilichomjibu ni kwamba "asilolijua ni kama usiku wa giza" Nilimpigia yule baba na kumueleza jinsi mwanaye anavyonishutumu akanijibu niachane naye kwani sisi na Mungu wetu ndio tunaoujua ukweli..

Ni karibu mwaka sasa sina mawasiliano na familia ile. Na ni kweli NAAPA MBELE YA MWENYEZI MUNGU yule baba hakuwahi kunitaka kimapenzi wala kuonesha dalili za kunitaka.

Poleni sana kwa kuwachosha. Sasa nauliza wapi nilipokosea waungwana mpaka yule mama kunihisi vibaya????????
 
Wivu wabongo low level of thinking.Achana na huyo baba Pia just move on mwambie thank you for everything .You need peace
 
Hujakosea kitu chochote dada, nakupengeza kwa kutofika msibani maana huenda hungeharibika kitu, wewe mshukuru mungu na huyo mzee kwa kukusaidia, na ujitahidi kusonga mbele kimaendeleo kwani naamini huyo mzee ndio kitu ambacho nayeye alipenda uwe nacho.
 
Hujakosea kitu chochote dada, nakupongeza kwa kutofika msibani maana huenda huyo mama angekuchenchia kweli, wewe mshukuru mungu na huyo mzee kwa kukusaidia, na ujitahidi kusonga mbele kimaendeleo kwani naamini huyo mzee ndio kitu ambacho nayeye alipenda uwe nacho.
 
Mbu waning'ata nashindwa kuandika.. Ngoja kidogo niingie kwenye net
 
Mbona hili liko wazi dadangu,binti alipokupigia simu na maneno chungu nzima content yake ilijaa masuala ya mapenzi..wakiimani kuwa wewe unatoka na baba yake. Sasa binafsi hujafanya kosa ila unajua fika sababu ya yote hayo ni nini..ni hisia kuwa una uhusiano wa KIMAPENZI na yule baba na ndiyo maana yule baba alikwambia "WEWE NA YEYE NDIYO MNAOUJUA UKWELI". Mshukuru Mungu kwa kila jambo na endelea na maisha yako,endelea kumuombea kheri baba yako mlezi.
 
Pole mwaya, mshukuru Mungu hapo ulipofikia, endelea na maisha yako.
 
.......huna kosa ila, jiweke kwenye nafasi ya huyo mama. Ingekuwa ni wewe, mumeo anamfadhili binti mdogo mzuri kama wewe ambaye "hana mahusiano yoyote" ungejiskiaje?

....unadhani huyo binti angelipa vipi "fadhila" za ufadhili huo?
 
,shukuru mungu mpaka ulipofikia sasa na endelea na maisha yako
 
Hili lisikuumize moyo wako. Yaliyotokea yako nje ya uwezo wako kuyarekebisha ili ukweli ujulikane ila Mwenye Mungu anaujua ukweli. Binadamu wengine hawaamini kama Mwanaume anaweza kutoa msaada wa aina yoyote ile hasa kwa mwanamke bila kuwepo ngono. Endelea na maisha yako ila kila siku iendayo kwa Mungu muombee yule Baba kila la heri katika maisha yake kwa msaada mkubwa aliokupatia hadi kufika hapo ulipofika, huna haja ya kusononeka kabisa.
 
Wivu wabongo low level of thinking.Achana na huyo baba Pia just move on mwambie thank you for everything .You need peace

Nashukuru Natalia, ni wivu ndio ulikuwa unamsumbua yule mama. Lakini ninarudi nyuma na kujiuliza alinionea wivu kwa kipi?
 
Last edited by a moderator:

Asante ndugu yangu.
 

Ndugu Rogie, Kabla ya msiba yule dada hakuwahi kusikia wala kuuliza kama kuna kitu chochote kinachoendelea nyuma ya pazia. Na wala sikuwahi kuonesha ukaribu zaidi ya heshima apewayo baba toka kwa mwanaye. Sikuwaki kuwaza kama itafika siku moja anihisi hivyo. Nilishangaa ni nini kilitokea kwa ghafla mpaka anihisi hivyo?
 
Last edited by a moderator:
.......huna kosa ila, jiweke kwenye nafasi ya huyo mama. Ingekuwa ni wewe, mumeo anamfadhili binti mdogo mzuri kama wewe ambaye "hana mahusiano yoyote" ungejiskiaje?

....unadhani huyo binti angelipa vipi "fadhila" za ufadhili huo?
.


@mleta mada.. Nadhani Mbu amemaliza kila kitu.Tena nampa huyo mama big up.. Alijitahidi kwa kiasi chake.

Huenda kuna mambo ambayo yalikuwa hayaendi sawa katika familia na wewe ukaonekana ndo sababu. Lakini kubwa zaidi ni wivu wa kimapenzi ambapo mama alishindwa kuvumilia.

Na mbaya zaidi u can't prove ya innocent.


Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
.......huna kosa ila, jiweke kwenye nafasi ya huyo mama. Ingekuwa ni wewe, mumeo anamfadhili binti mdogo mzuri kama wewe ambaye "hana mahusiano yoyote" ungejiskiaje?

....unadhani huyo binti angelipa vipi "fadhila" za ufadhili huo?

Ndugu yangu Mbu, Unataka kusema tunapotaka kuwasaidia watu tuangalie jinsia? Yule mama kama alikuwa ana doubt na mie angelifanya uchunguzi ili kupata ukweli na sio kukurupuka.

Kwanini unahisi kwamba malipo ya fadhila yangeishia kwenye mapenzi?
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK

Nashuku sana kwa ushauri ndugu BAK, Ningelikuwa na uwezo wa kumfanya yule mama aamini kuwa hakukuwa na kitu chochote nyuma ya pazia ningelifurahi sana. Lakini uwezo huo sina. Hii issue imekuwa ikinisumbua sana kichwani.
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK
Nitakuwa muwazi kabisa kwako. Ulijiingiza sana pua yako pasipohusika. Tungekuwa tunafahamiana ningekuonya hili toka mwanzo manake ningeliona ujio wake. Kulala kwa watu is deep!

Ni sawa kutambulishwa kwa familia nzima. Lakini habari ya wewe kuja kulala nyumbani kwangu wiki nzima. Na uje kulala kwangu tena! Ingekuwa sawa kwenda kusalimia na kula dinner ama lunch tu, lakini sio kulala. Na kilichomuumiza zaidi nadhani ni mwanae kuja na mjukuu kukaa kwako wiki.
Mbu, asante kwa kuwa honest. Viatu vya huyo mama vingem'bana mwanamke yeyote. Hata tuwaulize wanaume humu jf:

mkeo anamfadhili kijana muda wote, na hatimae unakutana nae na unaambiwa alilala kwako wiki wakati haupo. Japo na wanao walikuwepo. Ukimuangalia kijana ana six pack, na wewe kitambi kiko mahali pake!
 
Last edited by a moderator:

Dada yangu sijui wala siwezi kujua kama kulikuwa na tatizo katika familia yake. Lakini kumbuka kuwa mie nilikuwa naishi mbali sana (nimetumia miji isiyohalisi ili kuwaelewesha) kiasi kwamba baada ya yule baba kupata uhamisho ilinichukua takribani mwaka mzima ndipo nikafunga safari kwenda kumsalimia.

Unampa huyo mama big up kwa kukurupuka au? Je ningemwambia anipe ushahidi wa mahusiano yangu na mumewe je angeweza?
 
Last edited by a moderator:
Labda kitendo cha kufungia safari msiba ndo kilimstua kuwa sasa umemuwin mumewe, na wanae. Na unatafuta umaarufu kwa ndugu wa mumewe.

Kumbuka ameishi miaka mingi kwenye hiyo familia, na atakuwa ameshagongana na baadhi ya ndugu wa mumewe. Labda alihisi unajiuza ukubalike.

Honestly, kama ni mie nafadhiliwa hapo ningeweka kadistance flani kati yangu na baba mlezi
Nashukuru Natalia, ni wivu ndio ulikuwa unamsumbua yule mama. Lakini ninarudi nyuma na kujiuliza alinionea wivu kwa kipi?
 
Last edited by a moderator:
Reactions: Mbu
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…