Kosa la uzururaji bado lina mantiki kwa hali ya sasa?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
666
Wakati wa mkoloni watu wengi waliokosa kazi rasmi ‘formal employement’ walikuwa wakikamatwa kwa makosa ya uzurulaji. Swala hili lilifanyika kwa malengo ya kuwanufaisha wakoloni kwa muda mrefu sana.

Pamoja na sababu nyingine zilizowekwa kuwa ni makosa ya Uzurulaji ilikuwa pia kwa sababu ya kuwazuia walioko kijijini kutotamani kuja mjini kwa kuwa wangekamatwa. Ilibidi wabaki mashambani ili kuendelea kuzalisha.

Ukiangalia kwa ukaribu utagundua kuwa kipindi cha ukoloni kazi za pesa walikuwa nazo wakoloni na walihitaji kodi kwa nguvu sana, na kodi iliyotegemewa ilikuwa direct one, ili kuepusha watu kushindwa kulipa kodi ilibidi wakafanye kazi mashambani huko ili kama sio kupata hela kwenye manamba basi auze vitu alivyolima ili kulipa kodi kwa mkoloni.

Nadhani mtakumbuka kipindi mtu kutembea ni lazima uwe na vibali tofauti tofauti kibali cha mwisho kufutwa ilikuwa ni kwenye kodi za baiskeli.

Nchi ilipokuwa huru watu wakalazimika kuja kwenye maeneo ya miji ili kupata huduma za kijamii kwa urahisi watu hao wakaona uzuri wa maisha ya mjini na wakaacha kujituma sana, mwisho wakaanza kulima kwa nguvu kwa kupewa the same case ya uzurulaji.

Hivi sasa tafiti za kiuchumi zinaonyesha watu wengi kijijini huja mjini kutafuta kazi ili kujikidhi. Pia nchi zinazoendelea kama Tanzania zinaonyesha kuwa sekta isiyo rasmi ndio huajiri watu wengi kuliko sekta rasmi.

Kutokana na sababu hizo, wengine hujiajiri kwa kazi mbalimbali zikiwemo za kufanya kazi hadi mida ya usiku, lakini kwa kuwa wako katika sekta isiyo rasmi watu hao hawana utambulisho wa kuonyesha kazi wanayofanya.

Hali hii imepelekea watu kukamatwa na kupewa makosa ya uzurulaji mjini. Lakini swali linakuja kama kweli kosa hili liko sahihi kwa wakati huu wa sasa. Hivi karibuni kuna wabunge waliambiwa wangekamatwa kwa kosa hilo.

Je swala la uzurulaji libaki kuwa kosa la kumuweka mtu ruande kwa wakti wetu wa sasa?

Signed

Oedipus
 
Sioni mantiki yoyote kumuita mtu mzururaji na wakati huohuo katiba inaruhusu free movement of people within tanzania as long as huvunji sheria zilizopo.
 
Hizi ni sheria za kijinga sana kuwaita watu wazurulaji tena wakati mwingine wakiwa wanatoka kwenye starehe kutumia their hard earned cash
 
Hili wazo zuri kabisa
Haiwezekani vijana wamevaa magwanda wanadhurura tu hawafanyi kazi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom