Deinstein 01
JF-Expert Member
- May 12, 2024
- 2,087
- 3,916
Habari Wakuu!
Kama kichwa cha habari kinavyosema, kosa lenyewe ni kuishi bila mpango naam kuishi bila plans.
Leo hii ukiona kijana kamaliza chuo halafu mwaka unaisha yupo nyumbani bila mishe yeyote ujue halikuwa hana mpango wa maisha yake baada ya kuhitimu. Na vijana wengi wa sasa wana hili tatizo.
Ndugu zanguni kama tunavyojua ya kuwa maisha ni safari na hauwezi ukasafiri kama hauna final destination yaani malengo na kama haujui njia utakayoitumia kwenye safari yako yaani mpango.
Moja ya sababu zinazowafanya watu waishi bila mpango ni kutojua malengo yao yaani watu wengi hawajui kusudi lao la kuwepo duniani ndo maana hata mpango wa kufikia hilo kusudi hawana. Na pia sababu nyingine ni kutokuwa na muda wa kufikiri kuhusu maisha yao inawezekana kuwa ni ubusy au uvivu tu wakufikiri.
Ukitaka kufanikisha lengo lako lolote lile liwe la kiuchumi, kisiasa na kijamii mfano kuoa. Wakuu ukiona ndoa imevunjika kuna possibility kubwa ya kuwa hao wanandoa hawakukaa pamoja na kuandaa mpango wa jinsi watakavyoishi kwenye ndoa yao. Of course mipango inaweza kuvunjika ila haimaanishi ndo ukate tamaa plan A ikienda wrong nenda kwenye plan B, kukata tamaa ni sawa na kwenda nje ya plan.
Yangu ni hayo tu wakuu. Siku nikibarikiwa nitaandika nyuzi kuhusiana na jinsi ya kujua kusudi lako la kuwepo duniani.