Kosa kubwa sana CHADEMA wamefanya kusema Serikali ndiyo iliyomshambulia Tundu Lissu bila ushahidi wowote!

Unauliza swali la kitoto sana, nani kafanya , kwani mleta mada ni Polisi? Subiri ripoti ya Polisi.
 
kwenye sheria kuna kitu tunakiita circumstantial evidence na hiki ndicho CDM wanachokitumia kujenga hoja hazijengwi kwa tofali na cement kama unavyojua wewe.
Circumstantial evidence inatumika pale ambapo amabapo hakuna ushahidi thabiti wa kuhusiana na tukio.
Lissu hajahojiwa,dereva ambae amesema anawajua washambulizi,hajahojiwa unapata wapi nguvu ya kutoa circumstantial evidence?
 
Toa uthibitizo wa maneno uliyoandika.
Uthibitisho ndiyo huo wa hayo maneno unataka yapo mengine...Viongozi wa Chadema anasema Serikali ndiyo wahusika wa shambulio la Tundu Lissu unataka nini zaidi? Wekeni ushahidi wa Serikali kuhusika ndiyo tunataka.
 
Kauli za mkuu ushahidi wa kwanza na umetolewa, mkuu alisema TL msaliti na wasaliti wapigwe lisasi hii ni amri halali na askari watiifu lazima watekeleze.

Mpaka Leo hao watu wasiojulikana hawajulikani, ingekuwa raia lazima wangeacha alama.
Mkuu ndiyo nani?
 
Huyo RPC wako yeye sio amesomea uchunguzi? Atafute ushahidi mwenyewe. Ngoja FBI waje hawataopata ushahidi?
 
Mbona hyo iko wazi.. Hata mtoto mdogo anajua.... Ndo maana mlikuwa mnaogopa ha Harubadili isisomwe....
 
Uchunguzi pekee ni wa vyombo huru vya kimataifa, acha maneno weka muziki wewe
 
Unasema Chadema wamefanya kosa kubwa kulaumu serikali bila ushahidi wowote haya wewe una ushahidi gani kwamba wa kinyume Chake?
 
please mtoa hoja unaweza kutupatia hapa facts za tangazo hilo kutoka chadema wakisema serikali inahusika,keep in mind chadema wana SG na spokesperson wao,sio kila mtu ni msemaji wa chadema.
 
Wakiongozwa na Lazaro Nyarandu MZEE wa kusafirisha Twiga

Ni kweli serikali ilitaka kumuua Lissu na ushahidi upo 100% .
Ni Magufuli alitamka akiwa Ikulu akimwambia spika wa bunge, Job Ndugai, aliyeupata uspika kwa kumpiga mtu hadi akazirai,na hapa namnukuu Magufuli.
"Wakiwa ndani ya bunge wana kinga wanaweza kuropoka chochote, Wewe wafukuze wote wanaoropoka, wakitoka nje mimi nitawashughulikia "
Mwisho wa kunukuu.
Lissu hakuwa na ugomvi na mtu zaidi ya serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…