Kosa kubwa sana CHADEMA wamefanya kusema Serikali ndiyo iliyomshambulia Tundu Lissu bila ushahidi wowote!

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,317
Kama Kuna kosa kubwa Chama cha Chadema wamefanya mwaka huu ni ile hali ya kuiaminisha jamii ya kitanzania na kimataifa kuwa shambulio la Tundu Lissu limefanywa na vikosi vya ulinzi na usalama vya Serikali.

Huo mtazamo wa Viongozi wa Chadema na wafuasi wao kuhusu Serikali kuhusu na shambulio kwa Tundu Lissu utawasumbua sana ktk mahusiano kisiasa.

Na jinsi wanapanga kupeleka malalamiko yao UN na Jumuia ya kimataifa ni kudhihirisha kuwa kweli Serikali imehusika na hawana Imani nayo.

Nadhani huu mtazamo wa Viongozi wa aina hii kuwa kila Kitu unasingizia Serikali si Mzuri sana.

Sidhani kama Chadema wanaweza kuweka ushahidi wowote mezani usio na shaka kuwa ni kweli Serikali imehusika.

Kwasababu RPC Muroto wa Dodoma alitoa wito mwenye ushahidi wowote apelekwe Polisi labda Viongozi hao watakuwa wamepeleka.

Tumuombee Tundu Lissu apone haraka na uchunguzi utoe taarifa mapema kuhusu shambulio hilo.
 
Serikali umesikia ikikanusha kwamba haihusiki?
Chunga mdomo wako
 
Huo mtazamo wa Viongozi wa Chadema na wafuasi wao kuhusu Serikali kuhusu na shambulio kwa Tundu Lissu utawasumbua sana ktk mahusiano kisiasa.
Lini CDM imekuwa Na mahusiano mema Na serikali kuanzia mabomu ya Soweto hadi vifo vya kushambuliwa

Na jinsi wanapanga kupeleka malalamiko yao UN na Jumuia ya kimataifa ni kudhihirisha kuwa kweli Serikali imehusika na hawana Imani nayo.
Waruhusu wachunguzi Wa kimataifa waje kufanya uchunguzi Wa vifo vyote ili kuondoa mashaka,kukataa maana yake ni KUJILINDA dhidi ya aibu.

Nadhani huu mtazamo wa Viongozi wa aina hii kuwa kila Kitu unasingizia Serikali si Mzuri sana.
Hivi ni Nani wamiliki Wa SMG? Na kwanini tukio litokee eneo LA viongozi Na sio eneo LA wazi Kama ni uhalifu Wa kijambazi? Na kwanini walifanikiwa kutoka?Nani anayeweza kupita eneo LA viongozi bila sababu ya msingi?WASIWASI NDO AKILI.

Sidhani kama Chadema wanaweza kuweka ushahidi wowote mezani usio na shaka kuwa ni kweli Serikali imehusika.
Trends Na matukio ya nyuma,kauli Na chuki za wazi ndio yanafanya suspect number moja awe huyo unayedhani.

Kwasababu RPC Muroto wa Dodoma alitoa wito mwenye ushahidi wowote apelekwe Polisi labda Viongozi hao watakuwa wamepeleka.
Kuvamiwa Na kuuwawa kwa polisi Na mbwa wao miaka kadhaa nyuma tena tukio LA usiku hakuna MTU aliyeona,wahusika wote waliuliwa tena wakiwa Dodoma,Morogoro,Pwani Na Dar es Salaam.Je polisi walipata wapi taarifa za wahusika.Mbona hili kigugumizi? FBI wanaweza kutusaidia iwapo Muroto Hana taarifa.

Tumuombee Tundu Lissu apone haraka na uchunguzi utoe taarifa mapema kuhusu shambulio hilo.
Hapo umenena hata Kama ulikuwa unaombea iwe vinginevyo
 
Kwasababu RPC Muroto wa Dodoma alitoa wito mwenye ushahidi wowote apelekwe Polisi labda Viongozi hao watakuwa wamepeleka.
Kama hakuna aliyepeleka ushahidi wowote kuhusu tukio hili,basi na wewe
huna haki ya kuandika ulichokiandika mpaka polisi watakapotoa majibu
ya uchunguzi wao wa ni nani aliyehusika na hilo tukio.

Hatuwezi kila kitu kusubiri raia walete taarifa wakati polisi
ina uwezo wa kufanya uchunguzi na ni taaluma yao,
wameisomea humu nchini na nje ya nchi.

Ni vyema tukae Kimya badala ya kukurupuka
na maelezo yasiyo na ushahidi.Kama vipi
polisi iwaite waliotoa hizo shutuma wawahoji labda watapata pa kuanzia.
 
Kama Kuna kosa kubwa Chama cha Chadema wamefanya mwaka huu ni ile hali ya kuiaminisha jamii ya kitanzania na kimataifa kuwa shambulio la Tundu Lissu limefanywa na vikosi vya ulinzi na usalama vya Serikali.

Huo mtazamo wa Viongozi wa Chadema na wafuasi wao kuhusu Serikali kuhusu na shambulio kwa Tundu Lissu utawasumbua sana ktk mahusiano kisiasa.

Na jinsi wanapanga kupeleka malalamiko yao UN na Jumuia ya kimataifa ni kudhihirisha kuwa kweli Serikali imehusika na hawana Imani nayo.

Nadhani huu mtazamo wa Viongozi wa aina hii kuwa kila Kitu unasingizia Serikali si Mzuri sana.

Sidhani kama Chadema wanaweza kuweka ushahidi wowote mezani usio na shaka kuwa ni kweli Serikali imehusika.

Kwasababu RPC Muroto wa Dodoma alitoa wito mwenye ushahidi wowote apelekwe Polisi labda Viongozi hao watakuwa wamepeleka.

Tumuombee Tundu Lissu apone haraka na uchunguzi utoe taarifa mapema kuhusu shambulio hilo.
Hivi wale waliorusha mabomu kule kanisani Olasiti na Soweto serikali ilishawapata ??
 
Umesema chadema wamefanya kosa kubwa kuituhumu serikali, Mimi binafsi sipingani na wewe.Sasa wewe tueleze ni nani ametenda haya,maana hawa jamaa wameshafanya kosa kutaja serikali wakati haihusiki.Ninaimani haya umeyasema kwakufanya uchunguzi yakinifu hivyo basi ni vema ukapeleka taarifa polisi juu ya hao unaowajuwa kutenda jambo hilo,kuliko kulaumu chadema ambao wametaja mshukiwa ambaye wewe hukubaliani nao.

Sasa napenda kukupa shule jinsi ya kuchunguza jambo lolote lile: Kwanza kabisa unaangalia matukuo ya nyuma kabla ya tukio kuu,then unaangalia nyendo za maadui wa mlengwa kabla ya tukio,tatu unaangalia taarifa za matukio ya nyuma kama zilifika sehemu sahihi inayohusika na uchunguzi,na kama taarifa ilifika unapaswa kuangalia jinsi ilivyo shugulikiwa,na kama haikufika unapaswa kujiuliza kwa nini taarifa haikufika.

Jambo jingine unaangalia matendo yaliyotokea wakati wa tukio,lakini ukiwa unaangalia wale uliokuwa unawahisi kama kuna uhusiano wowote.Mwisho unaangalia matendo yanayoendelea baada ya tukio kwakuangali wale unaowahisi.

Kwahiyo haya mambo yanautaratibu wake,siyo unajiandikia tu bila kutumia critical thinking.Kwa nyongeza,MTU anayeweza kuchunguza mambo haya kiyakinifu ni yule mwenye sifa ya introvert na si extrovert maana huyu sifa yake kuu ni kuharibu uchunguzi kwaajili ya misifa na mbwembwe mbele ya mkusanyiko wa watu.
 
Kama Kuna kosa kubwa Chama cha Chadema wamefanya mwaka huu ni ile hali ya kuiaminisha jamii ya kitanzania na kimataifa kuwa shambulio la Tundu Lissu limefanywa na vikosi vya ulinzi na usalama vya Serikali.

Huo mtazamo wa Viongozi wa Chadema na wafuasi wao kuhusu Serikali kuhusu na shambulio kwa Tundu Lissu utawasumbua sana ktk mahusiano kisiasa.

Na jinsi wanapanga kupeleka malalamiko yao UN na Jumuia ya kimataifa ni kudhihirisha kuwa kweli Serikali imehusika na hawana Imani nayo.

Nadhani huu mtazamo wa Viongozi wa aina hii kuwa kila Kitu unasingizia Serikali si Mzuri sana.

Sidhani kama Chadema wanaweza kuweka ushahidi wowote mezani usio na shaka kuwa ni kweli Serikali imehusika.

Kwasababu RPC Muroto wa Dodoma alitoa wito mwenye ushahidi wowote apelekwe Polisi labda Viongozi hao watakuwa wamepeleka.

Tumuombee Tundu Lissu apone haraka na uchunguzi utoe taarifa mapema kuhusu shambulio hilo.

Mambo kama haya siyo kwamba Tanzania ndiyo nchi ya kwanza watu kupigwa Risasi au kuuwawa kwa njia nyingine .Zipo nchi nyingine yalifanyika haya na wahusika walijulikana ni nani alifanya kwa ajili ya nini kwa faida gani na tukumbuke Upelelezi wao huenda ndani mpaka kujua sababu.

Na hapa Chadema wanachokifanya sio kibaya kwani kuna baadhi watu wanasema kupigwa Risasi kwa Lissu wao ndio wahusika mfano ni Jumapili iliyopita asubuhi kuna kipindi kilirushwa na Star Tv na Mtangazaji anaitwa Mapuri kukawa na kiongizi wa Chadema wa hiyo kanda .

Yaani tangu kipindi kinaanza mpaka mwisho kinaishi maswali yote ni ya kichama lakini huyu jamaa alikuwa yuko vizuri kwa kila aliloulizwa.

Ebu niambie Chadema kwa haya kwa nini wasiende ktk usalama wa kimataifa wao wana listi ndefu ya watu wao waliouwawa kwa vipindi tofauti kwa hiyo hii hatua walioichukua sio mbaya kwani mfanya tukio akijulikana ni vizuri kuliko kuto kujulikana.

Haya mambo sio mazuri kwa jamii ya kitanzania yaani hatujawahi kuyasikia haya.
 
Kama hakuna aliyepeleka ushahidi wowote kuhusu tukio hili,basi na wewe
huna haki ya kuandika ulichokiandika mpaka polisi watakapotoa majibu
ya uchunguzi wao wa ni nani aliyehusika na hilo tukio.

Hatuwezi kila kitu kusubiri raia walete taarifa wakati polisi
ina uwezo wa kufanya uchunguzi na ni taaluma yao,
wameisomea humu nchini na nje ya nchi.

Ni vyema tukae Kimya badala ya kukurupuka
na maelezo yasiyo na ushahidi.Kama vipi
polisi iwaite waliotoa hizo shutuma wawahoji labda watapata pa kuanzia.
Ni kweli si vizuri kuandika kitu usichokijuwa,maana majitu mengine hata hiyo saikolojia ya kawaida hawajaisoma.
 
Uongo hupanda lift lakini ukweli hukwea ngazi... Ni swala la muda tu

Mtani kwa sababu ni ukweli uliopanda ngazi na sasa umeanikwa tu juani ukauke ili usioze.
1.Polisi hawa ni pamoja na Mkuu wa Polisi wa Dodoma aka RPC walifika kwenye tumia zaidi ya masaa mawili baada ya tukio.

2.Kumkatalia Lissu pesa za kutibiwa Kwenye proper hospital walijua fika Muhimbili Haina vifaa vya kufanya operation alizohitaji hili ni pamoja na dawa.

3.Kutokufanya mahojiano na walinzi wa getini ambao ni Polisi pia hadi Leo.

4.Kutokumhoji Dereva siku ya tukio waluposhtuka ni baada ya kuambiwa na walifanya tukio dereva aliwaona hivyo watagite mbinu ya kumnyamazisha

5.Hadi Leo hakuna Uchanguzi wala upuuzi wowote unaofanyika zaidi ya kukimbizana na vijana wa Chadema waliovaa T-shirt za Pray4Lissu au wanataka kufanya Maombi whether Albadir au Maombi ya kawaida.

Utaniambia hapo hakuna Mkono wa Serikali??

Cha msingi Serikali inatakiwa kutambua kwamba kuna Technology ambazo ukicheza kidogo unaumia mwenyewe.

IPO siku wanasema siri ni ya MTU mmoja tu.
 
Kama Kuna kosa kubwa Chama cha Chadema wamefanya mwaka huu ni ile hali ya kuiaminisha jamii ya kitanzania na kimataifa kuwa shambulio la Tundu Lissu limefanywa na vikosi vya ulinzi na usalama vya Serikali.

Huo mtazamo wa Viongozi wa Chadema na wafuasi wao kuhusu Serikali kuhusu na shambulio kwa Tundu Lissu utawasumbua sana ktk mahusiano kisiasa.

Na jinsi wanapanga kupeleka malalamiko yao UN na Jumuia ya kimataifa ni kudhihirisha kuwa kweli Serikali imehusika na hawana Imani nayo.

Nadhani huu mtazamo wa Viongozi wa aina hii kuwa kila Kitu unasingizia Serikali si Mzuri sana.

Sidhani kama Chadema wanaweza kuweka ushahidi wowote mezani usio na shaka kuwa ni kweli Serikali imehusika.

Kwasababu RPC Muroto wa Dodoma alitoa wito mwenye ushahidi wowote apelekwe Polisi labda Viongozi hao watakuwa wamepeleka.

Tumuombee Tundu Lissu apone haraka na uchunguzi utoe taarifa mapema kuhusu shambulio hilo.
Wewe umeyatoa wapi?Wewe ndio serikali?he hao chadema wametoa taarifa hiyo lini? Nyie vijana wa Lumumba mbona mnaweweseka? Siku ya 14 Leo Moyo wa Tundu Anti_virus Lissu bado unagunda, Aibu yenu.
 
Back
Top Bottom