SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 5,136
- 7,904
Ujio wa Kocha Benchikha pale Simba ulitakiwa uambatane na kufungua ukurasa mpya wa mashirikiano kwa kila mmoja pale Simba hasa kati ya wachezaji na viongozi achilia mbali mahusiano kati ya viongozi kwa viongozi.
Baadhi ambao tunajua jinsi migogoro ndani ya taasisi hizi za waswahili zinavyokuwa tulikuwa tunategemea kuwa Benchikha mwanzoni kabisa atalishwa sumu za visasi na migogoro ya nyuma iliyomvuruga Robertinho aliyeamua kula na vipofu.
Katika safari ya kwanza tu ya Simba nje ya Tanzania chini ya Benchikha walipokuwa wanakwenda Botswana kuna tukio nililiona likaniambia Benchikha anaenda kurithishwa migogoro. Lilikuwa ni suala la muda tu kabla ya haya yanayoendelea sasa kuibuka na nadhani tutaenda kuona mengi zaidi.
Tatizo la Simba ni ombwe kubwa la kiuongozi. Huu ni mzizi wa matatizo yake yote. Management ipo kama kiini macho tu ila hawana kazi na hawajapewa nguvu za kutekeleza majukumu ya kila siku ya timu.
Unaambiwa kuna Kamati ya Nidhamu ambayo si sehemu ya Management ya timu. Unaambiwa kuna Baraza la Ushauri ambalo si sehemu ya management wala sehemu ya Bodi ya Wakurugenzi. Migogoro ambayo ingetakiwa kuishia katika mikono na maamuzi ya Kocha au Manager inapelekwa kwa Kamati ya Nidhamu ambayo tunaambiwa inajitegemea na haiingiliwi na mtu yoyote. Hii ni klabu ya mpira au imekuwa Chama cha Siasa?
Kibaya zaidi, viongozi binafsi wameajiri baadhi ya wanachama ambao wanalishwa maneno ili kuwachafua wachezaji na kuwalinda viongozi. Hawa virusi wanaoitwa "wenye mvuto" wengine wana access ya moja kwa moja na Benchi la Ufundi na taarifa za siri za Klabu na wanazitoa bila woga. Wanaweza kutoa taarifa za kumchafua mchezaji au kocha ambazo zinaweza kuwa siyo kweli wakijua wazi mchezaji au kocha hawezi kutoka kujibizana nao hadharani ila uongozi hauwachukulii hatua yoyote hao wanachama.
Nimekuwa nasema Simba kuja kusimama na kutulia itachukua muda mrefu sana kwa sababu hakuna viashiria kuonyesha watu wana nia ya kweli kutatua migogoro yao. Watu wanavumiliana tu halafu baada ya muda wanaanza kuvurugana tena. Hii mitikisiko tuizoee.
Kwa kumalizia Simba bado haijapata mbadala sahihi wa Clatous Chama. Ni kweli Chama ana tabia ya kupoza mashambulizi ya timu ila kama mnategemea Saido Ntibazonkiza, anayepoteza 90% ya mipira inayokuja kwake kwa sababu ya kuanguka anguka, kwa kutoa pasi za hovyo au kwa kutokuwa na first touch nzuri, ambaye kuja kwake Simba ndiyo kwa kiasi kikubwa kuliharibu muunganiko mzima wa uchezaji wa Simba ndiye awe tegemeo pale Simba, futeni matumaini yote hata yale mapya yaliyoanza kujitokeza baada ya kumfunga Wydad.
Benchikha alipokuja tu nilisema akiona mambo yasiyoeleweka hatutakuwa naye ifikapo January. Embu ngoja tusubiri.