Mwanaukweli
JF-Expert Member
- May 18, 2007
- 4,789
- 1,732
Mkuu, si kweli kuwa tulikuwa tunaenda vizuri. Wakati huo hata viatu tulikuwa hatuna, tulikuwa tunavaa matairi ya mpira. Nguo, tulikuwa tunabadili vitambaa vya sanda kuwa batiki tukiita kamanyola.Tatizo lipo hapo, mpaka Miaka ya '90 tulikuwa tunaenda vizuri sana tu, yaani tulikuwa tunamalizia kuweka Misingi ya kama ni Ndege basi ianze kuruka, kwa bahati mbaya sana kuna watu ambao hawapendi maendeleo yetu waliliona hilo (nahisi) hivyo wakatuingilia na kutushinikiza tuingie kwenye Mfumo wa Uhuru wa kupitiliza, na sasa Matokeao yake ndio hayo!
Unaweza ukawa hauoni hatua tuliyopiga, lkn mpaka Miaka ya 1985 watu waliokuwa wanajua kusoma na Kuandika Nchini kwetu walikuwa ni 88%, shauri ya Elime ya Watu wazima tulikuwa na tunawapita hata Nchi kama Uturuki, na mambo mengine mengi tu mazuri!
Hivyo tulikuwa ndio wazungu wanasema ready for take off kwa maana Misingi yote ilikuwa sasa tayari, ila sasa tukaingiliwa na mambo ya Uhuru usio na Mipaka!
Kulikuwa na uhaba wa kila kilicho cha muhimu kwa uhai.
Nakuwekea hapa data za kukua kwa uchumi wakati huo unaoutukuza kuwa tulikuwa tunaenda vizuri.
Source: URT Ministry of Finance.
Tutaanzaje kupaa wakati growth ilikuwa negative?
