Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,133
- 39,079
Habari wakuu; mwezi mmoja uliopita ni watanzania wachache waliojua kwamba katika sehemu moja ya nchi hii, huko wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza kuna kijiji kiitwacho Koromije. Lakini wiki ya mwisho ya mwezi Februari imeshuhudia hata tusiojua tujue huko Mwanza kuna Koromije na kwa watanzania sitashangaa kuanza kuona magari, bajaji, au pikipiki zikiandikwa jina hili maarufu kwa sasa. Hii inanikumbusha Samunge, kijiji kilichopata umaarufu wa ghafla baada ya kuibuka kwa Babu Mwasapile na jinsi Serikali ilivyohangaika kupeleka miundombinu muhimu kwa kipindi kifupi na kuwafanya wananchi wa Samunge waanze kufurahia si matunda ya Uhuru bali matunda ya muujiza wa kikombe cha Babu. Ninachojiuliza kwa sasa, je, Koromije itapata matunda iliyopata Samunge? Na huu mtindo wa watanzania kupandisha hadhi ya eneo ghafla kutokana na tukio fulani una manufaa au unadidimiza maeneo yetu?