Korea Kaskazini yasema inajiandaa kushambulia Japan

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Korea Kaskazini imesema kuwa ulipuaji wa makombora manne hiyo jana ulikuwa mafunzo ya kujiandaa kushambulia vituo vya kijeshi vilivyoko nchini Japan na kwamba shughuli hiyo ilisimamiwa na kiongozi wa Taifa hilo katili Kim Jong-un.

Rais Trump alifanya mashauriano kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, na Rais wa muda wa Korea Kusini kujadili jinsi ya kujibu kitendo hicho.

''Korea kaskazini imefyatua makombora yake manne leo na kuangukia karibu na eneo letu la maji lenye manufaa kwetu kiuchumi.
 
Dogo anajua mchina yupo nyuma. MCHINA ANAMTUMIA TU DOGO KUTIKISA HAWA ALLIES WA USA JAPAN N SKOREA kama ambavyo USA amewaweka wale imposters pale Israel ili wawazingue waarabu kila siku ndio mchina na North Korea. So hata USA n JAPAN hawawezi kumgusa maana ni kama umemgusa mchina
 
Japan haina weapons kali inategemea ilindwe na USA kama korea kusini
Japan kijeshi wako vzuri sana ila hawana nuclear weapons tu. Na km North Korea akamuua kushambulia Japan bhas haitopita hata dakika na yy ataanza kupokea makombora ya US toka nyambizi(submarine) za US zilizo kwenye rasi ya Korea.Mwaka Jana ilikuwepo Los Angeles class submarine sijui mwaka huu itakaa ipi hpo.
 
Dogo anapiga mkwala tu hana huo mpango wa kushambulia! Marekani wamefurahia maana huo mfumo wa kujilinda watakaoufunga Korea kusini hawautoi bure! Pesa ya kufa mtu imeingia! Na ni hasara kubwa kwa Korea kusini!
 
Marekan mjanja sana hapo anaua ndege wawili kwa jiwe moja. Kwanza uwepo wa THAAD utazuia makombora ya North Korea pia radar za THAAD kama wataalam wanavyosema pia itacover part kubwa tu ndani ya China hivyo kuchunguza nyendo za China kijeshi hasa mahali yalipo maeneo ya kurushia makombora (silos).Wewe hujiuliz kwann China anambana South korea kila pembe aghaili mpango wa kuleta THAAD lkn wapi tena US ndo kaamua kuiharakisha maana ilitakiwa iletwe kat kat ya mwaka na ianze kufanya kaz mwishon mwa mwaka huu lkn kwa sasa itaanza kaz mapema kabla ya hapo.
 
Sijui nini kinataka kutokea ila kwa uelewa wangu North Korea akianzisha vita hata Kama atapigwa na kushindwa madhara na uharibifu na idadi ya vifo kwa askari na raia wa Japan na South Korea hayatasahaulika katika historia Ya hii dunia, lakini kitendo cha USA kushusha THAAD jana usiku South Korea labda kinaweza kubadilisha hali ya mambo japo China imekasishwa Sana na jambo hilo
 
Huyu dogo kwa mikwara balaa, anachezea sharubu za wakubwa kilasiku
 
Sijui nini kinataka kutokea ila kwa uelewa wangu North Korea akianzisha vita hata Kama atapigwa na kushindwa madhara na uharibifu na idadi ya vifo kwa askari na raia wa Japan na South Korea hayatasahaulika katika historia Ya hii dunia, lakini kitendo cha USA kushusha THAAD jana usiku South Korea labda kinaweza kubadilisha hali ya mambo japo China imekasishwa Sana na jambo hilo
Mkuu huenda n/Korea Ana back up ya urusi
 
Back
Top Bottom