1. Naam... Sababu kubwa ni Siasa kwa maana ya siasa kuelekea uchaguzi, huku ikikolezwa na mafahari wawili wakimataifa wasioweza kukaa katika zizi moja.
Hao mafahari wananguvu na wanaingilia hadi mambo nyeti ni wakongwe katika gemu ya siasa mithili ya kungwi/somo ambaye ana mingle katika ndoa ya watu na kutoa manual script/ratiba ya nini, nani, wapi sangapi, na kivipi faragha yenu kifanyike.
Sasa tuachane na hao mafahali tujadili sisi mifigo wafuasi.
2.Sababu ndogo ndogo
Kimsingi hali hii tunayopitia kipindi hiki kuelekea uchaguzi chanzo kikuu/mzizi wa tatizo ni serikali yenyewe inazalisha tatizo badala ya kutatua tatizo yenyewe inalikuza tatizo.
Kwanini nasema inalikuza tatizo ni kwasababu baadhi ya raia wenye kujali wanapoona shida mahali wanasubiri mrejesho/ufumbuzi wa tatizo wanapoona hakuna kinachofanyika, kisaikolokjia hilo gape likisipo zibwa kwa hatua stahiki automatically binadamu ataliziba yeye kwa mawazo/idea au matendo anayoyajua yeye.
Pindi ananyanyuka na hoja mawazo au vitendo vyake binafsi moja kwa moja serikali inamjia juu na kumuona mkosoaji anayeikashifu serikali(viongozi) anaonekana amevunja sheria na anachukuliwa hatua kama kukamatwa na polisi kufikishwa mahakamani... Ilhali chanzo cha tatizo na mwenye makosa ni uongozi kuto kuwajibika kukosa weledi katika majukumu yao matokeo yake wanaacha mambo mengi wazi wananchi wakiyaona na kupigia kelele inakuwa nongwa.
Hii sio sawa nashauri serikali tekelezeni wajibu wenu ipasavyo.
Kwa mwenendo huu na ulimwengu ulivyofunguka hivi sitarajii hali iendelee kuwa hivi hivi kwa kwa afya ya nchi, hivyo basi mabadiliko na maboresho ni muhimu sana... Na kama hakuna nia yoyote ya mabadiliko ya kanuni sheria basi watawala wahakikishe nchi inajifungia piga propaganda raia wenu kama wanavyofanya North Korea bila hivyo "patachimbika, dawa inachemka, tutakua kujenga ukuta tusipo ziba ufa"
Hitimisho
Tunatarajia nini kama viongozi tutakua hututimizi majukumu yetu ipasavyo na kwa weledi tunataka tugundue nini? Hali hii inayoendelea sio nzuri na ni uthibitisho kwamba kunamahali tunafeli.
Asante.