Koo zenye wanaume wengi hazina Ushirikiano!!

Koo zenye wanaume wengi hazina Ushirikiano!!

Kigarama

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2007
Posts
2,492
Reaction score
1,242
Kwa utafiti wangu mdogo nilioufanya nimegundua kwamba zile Koo ambazo wamezaliwa wanaume wengi au wanaume watupu zina ushirikiano kidogo sana miongoni mwao kulinganisha na zile Koo zenye wanawake wengi au wanawake watupu. Hata mapacha wa kiume hawana ushirikiano sana ukilinganisha ushirikiano unaoonyeshwa na mapacha wa kike. Sielewi hili linasababishwa na maumbile au tamaduni za jinsia hizi mbili.

Labda wewe unajua!!
 
Koo za wapi hizo?
Mi najua za ninapotokea, ziwe na wanawake wengi au wanaume wengi bado zinakua na muungano/ushirikiano wa hali ya kuridhisha kama sio wajuu.

Hata hivyo mwanamke ni kiungo kizuri cha ushawishi hivyo hilo linaweza likachangia kwa wale watu wasio na ushirikiano wa asili.
 
kwanza definition ya koo ni nini?
Naona kama zinaongelewa familia hapa.
 
yan ukoo so wing wake ni koo, bt cna dfntion halc ya koo!upo hapo mkuu?
Koo kama vile za kina Nyerere, Sykes, Mwakingwe, Masanja,Sheuya,Mwenegoha, na Wasira. Kiafrika tunajitambulisha kwa koo kuliko familia zetu.
 
Back
Top Bottom