Konyagi bandia

Konyagi bandia

Tyupa

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2013
Posts
802
Reaction score
657
Asilimia 60 ya konyagi inayonywea kwenye bar zote Tanzania ni ya BANDIA.Hali hii inatokana na uzembe wa hali juu ya viongozi wa kampuni ya Tanzania Distillers inayotengeneza konyagi.Vingozi wa kampuni hii bado wapo kwenye giza totoro jinsi konyagi yao inavyohujumiwa.

Kwa sasa eti wamebandika mabango makubwa yanayolipiwa fedha nyingi ambazo kwao ingekuwa ni sehemu ya faida kubwa pia.Mabango hayo yanaonesha hatua kwa hatua jinsi mteja wa konyagi atakavyobaini konyagi halisi na ya bandia hasa ile ya pakiti au kiroba.Matangazo hayo kwenye mabango hayana maana yeyote kwa sababu watengenezaji wa konyagi bandia wanatumia pakiti zile zile za Tanzania Distillers zilizokamili na wao wanajaza pombe yao ya GONGO.

Ukiangalia kwa mwonekano ni konyagi halisi kama pakiti ya konyagi inavyooneshwa kwenye mabango, lakini ukionja unakuta ladha ya gongo au madudu mengine.Mkurugenzi wa kampuni inayotengeneza konyagi anatakiwa aamke kwenye usingizi achunguze pakiti zao za konyagi zinatoka vipi hadi zifike kwa watu wanaojaza gongo.Mabango ya konyagi yaliyopo mitaani na barabarani ni mapambo tu na wanapoteza pesa zao bure
 
Mimi siku hizi nimeacha kabisa viroba kwani mara mwisho kunywa ni mwaka jana.Nilikunywa kiasi kidogo lakini cha moto nilikiona nilianza kutapika huku nakunya kwenye suruali wima.
 
Haifai kabisa hii kitu,ukiamka asubuhi chumba chote ni harufu ya Gongo utafikiri umetoka kilabuni
 
Nilikua nataka nishangae!! Hivi tangu lini mtu akanywa konyagi halafu akatapika? Siku hizi raia wanarudisha chenji balaa.
 
THATHA KWANINI USIRIPOTI KIWANDANI HATUA ZIKACHUKULIWA? ACHA KUWAHARIBIA BIASHARA BANA! SIO FRESH!
-->>ONANA NA UONGOZI UJULISHE TU!
MODS
*******
ERASE THIS!
RUBBISH!
IMPACT AMBAYO INAWEZA TOKEA MTOA POST UTAWEZA FIDIA?
BETTER ERASE YOURSELF!
ii
qualif.buz.lawyer
****************
 
Viroba na konyagi ni gongo tu ile, watumiaji wote wanaunguza maini tu na kuwa marehemu wakujipendea.
 
tegeta nyuma ya kibo compex kwenye lile godown ndani wanatengeneza konyagi mwitu inamilikiwa na msaki, na kiwanda kingine kiko kipawa hata maofisa wa tanzania distilers na tra wote wanapajua.
viroba vya konyagi vyote vyenye label ya njano kwenye bei elekezi ni feki!
 
Mimi siku hizi nimeacha kabisa viroba kwani mara mwisho kunywa ni mwaka jana.Nilikunywa kiasi kidogo lakini cha moto nilikiona nilianza kutapika huku nakunya kwenye suruali wima.

Ulikunywa gongo !;;
 
juzi nilipata pakiti tatu tu lakini hadi Leo hali yangu ni mbaya mno,nilitapikaaa halafu nimeota vidonda kooni haviponi kwa dawa mpaka Leo,naanza kuelewa sasa
 
Back
Top Bottom