Kongole Spika Dkt. Tulia kwenye Sheria umeiva

Mkuu sijawahi kutazama hilo bunge kibogoyo la majizi ya kura hata kwa bahati mbaya. Nimelipuuza kwa kiwango Cha juu, hivyo siwezi kupoteza muda wangu kuangalia huo uchafu.
Mkuu Tindo,

Ni kweli kabisa usemayo. Lakini mimi huwa ninaamini hizi muvi na tamthilia tunazoziona kwamba kiongozi mkubwa anatoa maelekezo fanya hivi na usifanye hivi ni vitu halisi kabisa katika maisha yetu ya kila siku.

Uenda ufanisi wa watu umefichwa kwasababu ya mabavu ya serikali kwa viongozi wa juu, Hakuna mtu atakuwa yupo tayari kupoteza familia yake na kuiingiza kwenye matatizo.

Mimi naamini wapo baadhi ya wabunge ni watu makini sana ila wanashindwa kufanya kazi zao kwa ufanisi sababu wapo kati kati ya simba.
 
Ni kweli kabisa..
JUst imagine kichwa kama Mwakyembe kingekuwa Upinzani ,Pamoja na Paramagamba..?
Tulia kwa sasa anarelax sana...
Juzi nimesikitika kuona mwanasheria mkuu naye pia kuna baadhi ya vitu haelewi sasa kuna haja gani ya yeye kuwa bungeni?
Hii ni hatari sana!

Unajua kuna muda mpaka unabaki unashangaa. Mfano makonda alipokuwa kigoma jana, kuna Diwani alisimamishwa tangu mwaka 2021 kisa amekutwa si raia wa Tanzania. Mwaka wa 3 raia hawana diwani, mkurugenzi anaulizwa hakuna analojibu.

Nikasema laiti kama angekuwa mzee baba hayati magufuli watu wengi wangeondoka sema kakosa full power.
 
Hahahaha hana tofauti na anaesikiliza BBC🤣🤣🤣
BBC ni world class news outlet! Ukiongea hivyo unanipa mashaka na weledi wako! Kesho utasema Aljazeera, na CNN and the like utasema ni chini ya TBC
Wewe unaiamini Xinhua :D :D :D :D
 
BBC ni world class news outlet! Ukiongea hivyo unanipa mashaka na weledi wako! Kesho utasema Aljazeera, na CNN and the like utasema ni chini ya TBC
Wewe unaiamini Xinhua :D :D :D :D
Hiyo world class dish lake liliyumba kuelekea sehemu moja,si huru. Ndo maana nikasema hivo. Maana taarifa zake za mchongo.
 
Hii ni hatari sana!

Unajua kuna muda mpaka unabaki unashangaa. Mfano makonda alipokuwa kigoma jana, kuna Diwani alisimamishwa tangu mwaka 2021 kisa amekutwa si raia wa Tanzania. Mwaka wa 3 raia hawana diwani, mkurugenzi anaulizwa hakuna analojibu.

Nikasema laiti kama angekuwa mzee baba hayati magufuli watu wengi wangeondoka sema kakosa full power.
Serkali ya sasa hivi inajiendea tu kama kuku aliyekatwa kichwa ukitaka kujua Angalia Hizo ziara za makonda utagundua luna maovu mengi sana
 
Spika Tulia kaiva sana kwenye suala kutafiri Sheria, naangalia hapa Bunge live wanapitisha muswada wa tume ya uchaguzi naona anamtoa knout mpaka AG huyu dada ni balaa wabunge wote wanampigia makofi.

Mbeya tunasema Tulia mitano tena.
Acheni kusifia watu wasio waadilifu. Uadilifu ndo usomi in action mengine ni mbwembwe tu.

Mbona msomi kashindwa kutafsiri amri ya mahakama which is so simple, kuwatoa COVID 19, bungeni?

Hatutaki usomi wa ki interest , tunataka uadilifu wa kisomi.
 
Point.

Ni taa iliyozimwa na kufichwa gizani. Haina msaada wowote.

Maana ni kheri mbwa aliye hai, kuliko Simba mfu!!
 
Pengine hujaelewa kitu, hapigiwi makofi Tulia kama Tulia kinachopigiwa makofi ni kiti Cha Spika ambacho ni mamlaka ,Hata ungekuwa wewe ndio umekaa juu ya hicho kitu ungepigiwa makofi hata kama hujui sheria
Watu wanapiga makofi posho zimeongeza badala wakae bungeni siku 14 sasa ni 21 x 470,000 = 9,870,000 + 16,000,000 Grand total 25,870,000 hiyo ni February pekee nje na rushwa na takataka zingine
 
Spika Tulia kaiva sana kwenye suala kutafiri Sheria, naangalia hapa Bunge live wanapitisha muswada wa tume ya uchaguzi naona anamtoa knout mpaka AG huyu dada ni balaa wabunge wote wanampigia makofi.

Mbeya tunasema Tulia mitano tena.
Hata kwenye darasa la wajinga, kunakuwepo wa afadhali.

Spika Anna Makinda aliwahi kutamka kuwa mtu pekee aliyekuwa msaada mkubwa kwa Bunge, serikali inapopeleka miswada Bungeni, alikuwa Tundu Lisu. Kwa maneno yake Makinda, ni kwamba Lisu ndiye aliyekuea anawafumbua macho wabunge katika kuelewa kilichokusudiwa na Serikali, na ubaya wa sheria inayopendekezwa.

Pengo la Tundu Lisu Bungeni halijapata wa kuliziba.

Mtu mwingine iliyekuwa makini sana kwenye kuchambua miswada alikuwa John Mnyika. Mnyika siyo mwanasheria lakini uwezo wake mkubwa wa akili ulimwezesha acheze kila eneo kwa kiwango cha kufikiriwa kuwa ni fani yake.

Waliopo sahizi bungeni, licha ya kwamba hawakuchaguliwa na umma, lakini wengi wao hata uwezo wa akili ya kawaida hawana.
 
Kuijua sheria ni raha sana.

Binafsi hakuna mtu anayenitisha kwenye maisha kwa sababu ninaijua sheria.

Dr. Tulia akikuwa moja ya walimu wangu.

Wengine ni Prof. Kabudi, P.J.A.M, Prof. Luoga F, etal
Ata Mimi mkuu Jana Tulia akataja mischief nikakumbuka mbali Sana legal method
 
Mkuu Dr,

Hakika usemayo ni ukweli mtupu.
Kama jana angekuwepo mheshimiwa Tundu lissu bungeni, ndani kule watu wangekuwa wananyukana kwa hoja tu.

Nimetazama bunge lakini Tulia ni mtu makini sana ukweli pale bungeni hana challenge haswa kwa wabunge wakike wengi bado hawawezi kujenga hoja.
Kuna kadada fulani ni kembamba huwa mara nyingi anaongelea haswa kuhusu vijana yule dada ni mtu smart sana ila jina limentoka.

uchaguzi ujao tunategemea upinzani watapata viti vingi ili tupate hoja ambazo zimekosekana kwa muda.
Mkuu jana bunge lilikuwa la watu wachache Tulia ndo alikua amelitawala
 
Back
Top Bottom