Mwisho naomba mamraka zione juhudi zenu mapato yenu yareflect uchapakazi wenu nauzarendo wenu.kweli wakinamamawanaweza.
"...mamlaka...;" "...uzalendo..." Sijui kwa nini umeamua kuandika vile!
Lakini mada yako ni ya kutia moyo sana.
Na hili uliloliweka katika mstari huo wa mwisho, ndio hasa 'carrot' yenyewe ambayo husemwa katika juhudi za upambanaji na rushwa.
Hapa ingestahili, Magufuli mwenyewe siku moja akiwa na furaha zake, atoke zake Idodomya, afunge safari na kuwatembelea kwa kustukiza, na kutoa bwabwaja zake za kawaida na kuwatupia 'carrot' hizo ulizopendekeza hapo.
Siku hiyo hiyo, kabla hajarudi nyumbani anatua hapo NIDA na kutumbua watu kadhaa papo kwa papo.
Kama ulivyoeleza katika mada yako, hii idara ya Uhamiaji huko nyuma ilikuwa majanga sana.
Pasi za Tanzania zlikuwa ni aibu tupu, unatamani hata usionyeshe pasipoti yako ni ya wapi kwa watu wengine.
Sisemi kwa kuambiwa, niliyashuhudia mwenyewe miaka kadhaa nyuma iliponibidi kwenda kupata pasipoti mpya hapo makao makuu.
Raia wa nje, hasa wahindi na wasomali ndio walikuwa kama wenye ofisi hiyo, sisi wengine tukiibaki kusubiri wenye nchi yao wahudumiwe kwanza.
Ilikuwa inaumiza sana, na hasa ukijua huna lolote unaloweza kufanya kuibadili hali hiyo.