Kongole nyingi sana Uhamiaji Tanzania. Mmetupa heshima Watanzania

Escrowseal1

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
4,423
4,197
Huduma za uhamiaji Tanzania zimenikosha nikawiwa kuwapongeza. Sina uhakika kama Watanzania wenzangu wanawaona kama nilivyowaona.

Nawapongeza kwa yafuatayo:
1. Mmejenga mifumo very smart hasa ya malipo ya pesa ya serikali. hai attempt watumishi na ni rahsi, online applications is just fantastic.

2..Operations hapo uhamiaji kuanzia getini ni first come first serve uwe mwekundu, mweusi, blue you have equal chance na mnasimamia utaratibu hadi nilisahau kama niko nchini kwangu.

3. Watumishi wa uhamiaji hapo makao makuu mna discipline ya hali ya juu all the time mnafanya kazi kama siyo Watanzania niliowazoea kuanzia hao vijana kwenye ukaguzi, customer service, mafisa wakaguzi hapo madirishani na finger prints just not immigration that I know. Mzigo mlokuwa nao ni mkubwa ila mnachapa kazi sana kama siyo Waafrika jamani.

4.Tofauti na tulivyojizoesha Watanzania kwa passport zinazohitaji fast track mnamaanisha kweli fast track never believed. Mifumo yenu ni veey smart nawatumishi smarter.

5.Mmedisplay namber kwa watukutu wa rushwa kurepotiwa na box la maoni. Muhimu sana.
Nawashauri kuboresha yafuatayo hapo headquarter .

1. Priority kwa wenye uhitaji maalum kama seat , lining up nk

2. Fungeni AC hasa eneo la wateja .wateja na watumishi wanapata shida.

3. Sometimes vyoo havina maji

4.Wekeni utaratibu wawatu wanaokuja na begi za mgongoni. Watu wanalazimika kulipia kwani hamruhusu kuingia nazo mngeweka hata tag mtu akaziacha kwa walinzi kama ni necessary.

5. Hakuna sign kabisa ya rushwa hapo ofisini ila kuna vishoka mtaani wanaosaidia hiyo huduma kwa kucharge pesa kubwa .sina uhakika kama ni Rushwa ila haileti picha nzuri kwa mapinduzi mliyofikia.

6. Fanyeni ubunifu sehemu ya kuchukulia passport kule polisi ni kero watu wanajaa mno na utaratibu uboreshwe.

7 Saidieni idara mnazofanya nazo kazi kama NIDA . Idara ya nida ni aibu kwa nchi bado inafanya kazi kama ujima imejaa rushwa kila kona nchi nzima .nahsi ni idara inayoongoza kwa rushwa ndogondogo Tanzania nzima. Hata mwendesha boda boda anakwambia we toa 20,000 upate kitambulisho faster .wasaidieni wanatuangusha.

Mwisho naomba mamlaka zione juhudi zenu mapato yenu yareflect uchapakazi wenu na uzalendo wenu. kweli wakinamama wanaweza.
 
I see. Kama ni hivyo hongera kwao. Ila naona kama unajipigia promo hivi. Hiyo namba 2 nina mashaka na jinsi ulivyoipamba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mdau tu nimepata huduma yao. Its not a joke solution ni kwenda ukapate huduma yao halafu urudi. NIDA mombasa gongo la mboto ndo aibu ya taifa.

watu wanapanga msitari juani utadhani kamba .,mlinzi alowekwa kuhudumia utadhani kalala kunywagongo lughambovu. Reception unakutana naving'ast wauza huduma wanauliza pesa hadharani mbele ya wateja.NIDA ni aibu ya taifa.

I tried to compare the two .mi sikai Tanzania to be honest uhamiaji wako very civilized na nimewapenda bure its simple kama upo Tanzania tembelea makao yao makuu. wanawakilisha where we supposed to be tunaofanya kazi nje mnajua comparison mnayoipata mkirudi nyumbani. Uhamiaji wamenikosha.

Watanzania tumezoea kuponda bila kusifia panapostahili.sina maslahi na uhamiaji . Is just the best from the worst
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Kweli uyasemayo. Mwenyewe niliomba passport wiki 2 zilizopita,jana nimetumiwa ujumbe nikachukue ( nipo kanda ya kati). Jumla ya pesa ya serikali 150,000tsh, sijatoa hata kumi pembeni.
 
Hawa matonya(ombaomba) wa barabarani wajirekebishe. Wanawake wanaweza, Mh Rais labda amteue IGP jinsi ya ke
 
Kweli uyasemayo. Mwenyewe niliomba passport wiki 2 zilizopita,jana nimetumiwa ujumbe nikachukue ( nipo kanda ya kati). Jumla ya pesa ya serikali 150,000tsh, sijatoa hata kumi pembeni.
Ukienda na mtazamo wa kutoa pesa wafanyakazi wenyewe wanakushangaa tangu ni me angage nao sijanusa dalili hata chembe ya rushwa its just unbelievable idara zikajifunze kwao.
 
Hawa matonya(ombaomba) wa barabarani wajirekebishe. Wanawake wanaweza, Mh Rais labda amteue IGP jinsi ya ke
Nilidhani niko ulaya wanchotaka ni evidence tu ya application tofauti na immigration ya ujima
 
Kweli uyasemayo. Mwenyewe niliomba passport wiki 2 zilizopita,jana nimetumiwa ujumbe nikachukue ( nipo kanda ya kati). Jumla ya pesa ya serikali 150,000tsh, sijatoa hata kumi pembeni.
Ni ishara njema hiyo mkuu kwamba kama mambo yataendelea kua hivi basi kama nchi tunaelekea pazuri
 
Hakuna taasisi naichukia kama hii, yaani natamani kuhamia nchi jirani jinsi nilivyosumbuliwa passport, hivi kwanini uhamiaji wasitoe tu passport baada ya kujiridhisha ni raia?

Yaani utadhani passport ni visa ya marekani kweli? Nahisi wafanyakazi wa hicho kitaasisi si watanzania, na nafikiri hawajui watanzania wzngi waliozamia nchi kama south hawana passport kutokana na usumbufu wao, wangewapa passport tu xatu wajitafutie maisha.

Siipendi hii taasisi hata kidogo , watu masikini uhamiaji si rafiki kwao na nchi itaendeleq kuwa masikini kwasababu uhamiaji unawablock watu kutoka nje ya Tanzania eti passport mpaka uwe na mwaliko, mtu ana nauli anataka kujilipua si mmpe passport akajaribu maish kama ni Mtanzania?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwisho naomba mamraka zione juhudi zenu mapato yenu yareflect uchapakazi wenu nauzarendo wenu.kweli wakinamamawanaweza.
"...mamlaka...;" "...uzalendo..." Sijui kwa nini umeamua kuandika vile!

Lakini mada yako ni ya kutia moyo sana.

Na hili uliloliweka katika mstari huo wa mwisho, ndio hasa 'carrot' yenyewe ambayo husemwa katika juhudi za upambanaji na rushwa.

Hapa ingestahili, Magufuli mwenyewe siku moja akiwa na furaha zake, atoke zake Idodomya, afunge safari na kuwatembelea kwa kustukiza, na kutoa bwabwaja zake za kawaida na kuwatupia 'carrot' hizo ulizopendekeza hapo.

Siku hiyo hiyo, kabla hajarudi nyumbani anatua hapo NIDA na kutumbua watu kadhaa papo kwa papo.

Kama ulivyoeleza katika mada yako, hii idara ya Uhamiaji huko nyuma ilikuwa majanga sana.

Pasi za Tanzania zlikuwa ni aibu tupu, unatamani hata usionyeshe pasipoti yako ni ya wapi kwa watu wengine.

Sisemi kwa kuambiwa, niliyashuhudia mwenyewe miaka kadhaa nyuma iliponibidi kwenda kupata pasipoti mpya hapo makao makuu.

Raia wa nje, hasa wahindi na wasomali ndio walikuwa kama wenye ofisi hiyo, sisi wengine tukiibaki kusubiri wenye nchi yao wahudumiwe kwanza.

Ilikuwa inaumiza sana, na hasa ukijua huna lolote unaloweza kufanya kuibadili hali hiyo.
 
Uhamiaji ndio aibu kwa nchi mkuu tuache utani, bila connection unacheleweshwa mno kupata passport yako. Siipendi hili litaasisi nililala siku 4 nje ya uhamiaji baada ya hela ya guest kuisha. Mwezi mzima nimesafiri hadi Dar kwajili ya passport.
 
Uhamiaji ndio aibu kwa nchi mkuu tuache utani, bila connection unacheleweshwa mno kupata passport yako. Siipendi hili litaasisi nililala siku 4 nje ya uhamiaji baada ya hela ya guest kuisha. Mwezi mzima nimesafiri hadi Dar kwajili ya passport.
Labda tu bahati yako mbaya mkuu sina connection yoyote nilipata huduma yenye heshima kubwa kuwahi kupata katika ofisi za umma .wana pressure kubwa ya watu ila sijasikia complaints za hovyo. Misingi yote inafuatwa kwa standards za kimataifa nilikuwa sina imani kama wewe.
 
Back
Top Bottom