Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Nakubaliana nawe Mkuu, nauli bado ni 'za moto sana'. Lakini, mambo yatarekebishwa tu MkuuKweli tatizo nauli zoa si rafiki wajaribu ku adjust kidogo mbona wenzao fast jet walimudu kwa nauli rafiki ambapo wengi tulifaidika? Sasa ATCL mpaka mtu wa kawaida mnyonge na masikini wa Magufuli ukune kichwa sana kumudu nauli zao
Hovyoooo! kwa lipi toka awe Rais sijanufaika kwa lolote nilokuwa nayapata enzi za JK ni yaleyale, yani jamii yangu yoteee hatuoni lolote we're still the same.Asante Petro kwa mrejesho.Twende na JPM 2020.Jamaa atatutoa
Maneno haya huwa yananichekesha sana,ndoto ya Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli
Kwani Chadema sio watanzania au sijakuelewa...?Chadema njooni haraka tupingeeeeee
"" huduma zimeimarika sana. Kuanzia Cabin Crew, Marubani ""
Hapa kwenye marubani ufafanuzi mkuu'
Leo hujaweka namba zako kulikoni huwa hupigiwi?Waungwana wa JF nawasalimu,
Nipo safarini kuelekea Kigoma kikazi. Hivi sasa tunatua Uwanja wa Ndege wa Tabora kwakuwa tunapitia hapa kwenda Kigoma. Tupo na Ndege TC 128 aina ya bombardier. Nalazimika kulipongeza Shirika letu la Ndege kwa kuimarisha huduma.
Nimekuwa nikisafiri na Ndege za AirTanzania kwa muda mrefu hapa nchini na hata nje ya nchi. Nikiri kuwa kwa safari za ndani ya nchi,huduma zimeimarika sana. Kuanzia Cabin Crew, Marubani na Watumishi wengine wa AirTanzania, ukarimu na umakini unatamalaki.
Kwa safari zangu za Kigoma kwa Ndege za kuelekea Burundi na kupitia Tabora, leo nimeshuhudia Ndege yetu ikibakiwa na siti tupu tatu tu. Ni jambo la kutia faraja na kuonyesha wananchi kuridhishwa na huduma za AirTanzania. Kongole sana kwenu AirTanzania!
Kuimarika kwa huduma za AirTanzania ni kuisimamia kwa vitendo ndoto ya Rais wetu Dr. John Pombe Magufuli aliyejitoa kwa uwezo na maarifa yake yote kuhakikisha AirTanzania inaimarika na kuwa nembo yetu kitaifa.
Najivunia AirTanzania, najivunia kuwa mtanzania!
Ni lini tz tutakuwa na ndege za mizigo?Waungwana wa JF nawasalimu,

Tatizo ni kuua washindani wake, katika Biashara huwezi kujipima kama huduma ni zuri au la bila kua na mpizani wa dhati katika hiyo biashara, hiyo nikama propaganda tu. Mkubalie fast jet umpe na hizo route zote ndani ya mwezi moja utaona Atcl niwababaishaji I swear...