Juliana Shonza
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 2,009
- 1,607
Wapendwa katika Bwana..!!
Nimepata taarifa ya mkutano na kongamano kubwa litakalohudhuriwa na takribani kila mwanakijiji wa Tamaa Mbaya, katika eneo la kaskazini mwa nchi yao wakienda kujadili juu ya kuondokewa na mwenzao, aliyekuwa jemedari na nahodha wa chombo chao.
Lakini kilichonifanya niandike sio kukutana kwao, bali hoja inayowakutanisha. Hoja ya kusaka mchawi aliyesababisha kuvurugikiwa kwao na chombo chao kwenda mrama..mmoja wao alijenga hoja vizuri kuwa si jambo jema kuiacha chunusi imee, lazima utafutwe ufumbuzi kabla chunusi hiyo haijageuka Tambazi.
Vichekesho ni kuwa yule waliyemfanya kinara wa kikosi kazi cha kusaka mchawi wao, ndio mchawi mwenyewe. Lakini mmoja wao aliwaambia maneno ya hekima katika kongamano hilo kuwa ''tatizo letu tunawazungumzia watu ambao hatuna madaraka nao badala ya kumjadili 'mwele' aliye mbele yetu. Sio hekima kumjadili Bwana Majipu katika kongamano la kumsaka mchawi wa wanaTamaa Mbaya"
NB
Mimi zamani nilikuwa mwanakijiji wa Tamaa mbaya lakini sikieni Ujumbe wangu kwenu;
"Wanatamaa mbaya, hasa ninyi VIJANA. Nyinyi ni majimbi tu, si majogoo. Nyinyi si watu, watu hudadisi nafsi zao, na nyinyi mtakapoanza kudadisi nafsi zenu , mtakapoanza kupekuwa mazingira yenu, mtakapoangalia mambo kwa jicho kali, mtakapoanza kutafuta asili ya mambo, LAZIMA muulize kwa nini, kwa vipi na kwa sababu gani..humo ndio mlimo na UTU, HESHIMA na UHAI, sio katika domo kaya.
Nimekufunzeni, nimekwambieni, nimekufunulieni siri za Tamaa Mbaya, mimi nimeona mengi lakini nimekuonyesheni nyinyi ikiwa mnajali ni juu yenu kutaka kuelewa ama kupuuzia.
Nawatakia Ijumaa Njema.