Kongamano la maonesho ya tatu ya mafuta na gesi asilia Tanzania

ROBERT MICHAEL

JF-Expert Member
Oct 23, 2012
5,056
2,850
Lengo: Maendeleo ya sekta ya mafuta na gesi asilia kwa manufaa ya watanzania.
Eneo: Mlimani city
Wadhamini: Wizara ya Nishati,TPDC,Ewura,UDSM
Wahudhuriaji: Watanzania pekee
Mgeni rasmi: Steven Masele
Lugha: Kiswahili
Muda wa kongamano:Siku 2
 
Steven Masele amekaribishwa kuja kutoa nasaha zake akiwa amemwakilisha Makamu wa rais wa JMT.
 
Masele amepewa kuleta ujumbe na waziri wa Nishati na madini kuwa wizara imejiandaa vizuri kushirikiana na wadau wote wa uchimbaji na uzalishaji wa gesi na mafuta wawe wa ndani na nje.
 
Masele amesema kongamano hili litawashirikisha Watanzania wengi maana lugha itumikayo ni Kiswahili .Anasema ugunduzi wa mwanzo ulitokea mwika 1970.Anasema mpaka sasa hakuna ugunduzi wa mafuta bali ugunduzi bado unaendelea.
Anasema kwa sasa zaidi ya 50% ya umeme umetokana na gesi asilia.
Anasema sekta ya gesi asilia na mafuta itachochea sana maendeleo ya viwanda.
1500 MW nyingine zitakuwa tayari mpaka 2015.Kwa hiyo mpaka 2015 kutakuwa na jumla ya 3000MW kutokana na vyanzo mbalimbali.
 
Serikali inafanya jitihada ya kuwatambua watanzania walio nje ambao ni wataalamu wa gesi na mafuta ili warudi nyumbani kusaidia hii sekta.
 
Ili tunufaike na hii sekta tunahitaji kuitunza amani yetu.Taifa lolote liingiiao kwenye migogoro linapoteza utulivu wa kufikiri na watu wasio kuwa na mema na nchi ndipo wanapochukua nafasi.
Serikali iliwatambua wote waliochochoea vurugu za Lindi na Mtwara.
Serikali haitamvumilia yeyote atakayechochea vurugu awe jirani au mataifa makubwa.
 
Serikali imeweka mifumo ambayo itakayowezesha kunufaika na hii sekta na Shirika lake TPDC ndio lenye jukumu hilo.
Kwa mawazo yake yeye Masele anasema Kilimo hakijaondoa umasikini wowote japo ni uti wa mgongo.
Kazi ya TPDC kusimamia na kuchochea uchimbaji wa mafuta,kuishauri serikali kwenye sekta ya mafuta,kufanya utafiti.....
TPDC kushirikiana na Algeria kuhamasisha matumizi ya gesi ya majumbani.
Ewura wamefanya kazi nzuri kwenye mafuta haswa kwenye bei.
Serikali ipo hatua ya mwisho ya kuandaa sera ya ushiriki wa wazawa kwenye sekta ya gesi asilia.
 
Anashukuru waandaaji wa kongamano maana itawapa fursa watanzania kujifunza na kujadili masuala ya maendeleo ya mafuta na gesi kwa manufaa ya watanzania.
 
Back
Top Bottom