Kondom zageuzwa bangili Rukwa

Kondom zageuzwa bangili Rukwa

Obugwa Izoba

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2013
Posts
10,480
Reaction score
11,688
BAADHI ya wanawake mkoani Rukwa wamebadili matumizi ya kondomu za kike kwa kuzivaa kama urembo wa bangili. Mkurugenzi wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Rodi inayohusika na kutoa elimu kwa jamii ya njia sahihi ya kutumia kondomu ili kujikinga na maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU), Gideon Mpina aliyasema hayo jana, alipokuwa anazungumza na gazeti hili mjini hapa.

Alikiri kuwa matumizi sahihi ya kondomu za kike ni changamoto kubwa mkoani humo, kwa kuwa kondomu hizo zina umbo la bangili na baadhi ya wanawake wanazitumia kuvaa mikononi kama urembo.

"Bangili za kondomu hizo zimekuwa kivutio kikubwa kwa wanawake. Wanazivaa mikononi kama urembo kwani zinapendeza machoni sababu zikipigwa na mionzi ya jua zinabadili rangi mbalimbali na kuwa kivutio cha aina yake," alisema Mpina.


Source: HabariLeo
 
Back
Top Bottom