Konda na Makonda

Red Scorpion

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,736
4,252
konda : cheke cheke! abilia nauli

abiria: mi mwalimi

konda: onyesha kitambulisho

mwalimu: (anashika mfukoni) hiki hapa

konda (anakichukua kile kitambulisho na kukikodolea macho pande zote mbili)....

konda: (anarudisha kitambulisho) sasa mbona umekalia siti

mwalimu : kwan kuna tatizo?

konda: hebu wapishe waliolipa nauli wakae

mwalimu: (kwa hasira) hebu acha kunizaliliasha kijana

konda: (akimuangalia mwalimu usoni) hivi we unaona ni haki kukaa wakati alielipa nauli amesimama?

mwalimu (kimya)

konda: kwanza nyie walimu nina hasira na nyie sana

mwalimu (kwa ghadhabu) hasira?

konda: eeh kwanza mlinichapa sana bado nifeli.... na leo unapanda gari yangu huna nauli..

abiria wengine: hahahahahaha

konda: dah yani sipendi kupakia hizi chenga kubwa

mwalimu: nani chenga?

konda : yan wewe ni chenga kuliko huyo mwanafunzi unaemfundisha

mwalimu: (kwa tabasamu la aibu) kivipi?

konda : we umekalia siti hujalipa hata mia lakin dogo kasimama na amelipa 200..

konda (kwa kejeli) sasa sema wewe na dogo nan chenga?

mwalimu (kwa hasira anafungua pochi na kutoa sh 5000 ) kata mia nne yako mbwa wewe.


MAKONDA WAZO LAKO NI GUMU KUTEKELEZEKA LABDA MWALIMU AWE NA ROHO YA JIWE
 
Mengi yamesemwa tangu makonda atangaze ujinga. Kwanza walimu wanadai mengi, nyumba nk Hakuna Mwl hata mmoja atatekeleza, atakaekubali kukwaruzana na konda
 
Hivi mwalimu anatumia shs ngapi kwa siku?halafu eti alipiwe nauli,waalimu wanazo changamoto nyingi zinazowakabili wala sio naili
 
Back
Top Bottom