Wana jamvi,jana pale Kimara mwisho kwenye konakona ambapo sasa hivi watu wanapaita kitonga kulitokea ajali mbaya sana,dereva wa lori lililokuwa limebeba container alishindwa kumudu zile kona gari likaangukia pembeni miguu juu,huku sehemu ya dereve likiwa nyang'anyang'a.
Juzi yake lori mbili zilishindwa kupishana zikagonganakiubavu ubavu,tena yale malori ya fourty feet ndo hata kupishana na gari ndogo hayapishani kabisa.
Sasa pale nia yao sijui wamejenga ili lipite gari moja tu au?..wafanyabiashara walioko pale wanasema kila siku kuna ajali ya magari kugongana.
Sasa hapa la kujiuliza,je pale kimara mwisho kulikuwa kuna sababu ya kuweka konakona zile ambazo dalili zimeshajionyesha kuwa kuna uwezekano wa baadae kuja kujitokeza ajali mbaya zaidi.
Ushauri wangu litafutwe ufumbuzi haraka kabla hayajaja kutokea maafa makubwa zaidi.Pia waziri magufuli tembelea pale kimara mwisho uone kama kulikuwa kuna ulazima wa kuweka konakona nyingi kama zile.​