KOMBORA KIOTANI-42

KOMBORA KIOTANI-42

FANANI MTENZI

Senior Member
Joined
Jul 4, 2017
Posts
106
Reaction score
95
KOMBORA KIOTANI-42

BONIFACE BIRAGE

Ilikuwa hatari kwake.Hatari iliyomtisha na kumdhoofisha na akashindwa kujua anajisaidiaje.Walinzi wa rais walimweka chini ya ulinzi mkali sana na tayari walikuwa mbioni kumuadabisha nap engine wangemuua palepale.

Dedani akajua amewekwa sehemu mbaya na wanausalama hawa.Alikuwa amemjeruhi vibaya sana mke wake.Napengine angepoteza maisha au hata angempoteza mtoto.Kwa sasa Dedani alikuwa adui wa taifa kwa kuhatarisha maisha ya rais Kilua.Lilikuwa pigo kubwa sana lililohitaji kukemewa na kudhibitiwa.Alijua amejitakia kifo.

“Nahitaji kumuona mke wangu?”Dedani aling’ang’ania.

“Hatuna imani na wewe.”alisema moja ya walinzi.

“Ni mke wangu!”alijitetea bwana Dedani akijaribu kuweka mambo sawa pengine wangemuelewa.

“Tunajua ni mkeo.Lakini kwetu sisi Kilua ni rais wa Kiota.Ni amiri jeshi mkuu ndo mwenye dhamana pamoja ya taifa.Hatua yako ya kumpiga ni tishio na wewe ni hatari kwa usalama wa rais.Hatuhitaji uwepo wako karibu naye.Tafadhali tunaomba utulie.”

Dedani alijua amelikoroga pengine haukuwa mpango lakini imetokea tu kwamba amempiga mkewe tumboni na sasa kamsababishia maumivu makali sana hali inayoleta sintofahamu kwa upande wake na usalama wake.Itakuwaje kwa mwanamke huyu kuwa kaibu naye.Hata aseme ilikuwa bahati mbaya bado wasingemwelewa.Ukelele ulisikika wa rais Kilua akilia kwamba mume wake atamuaa.Ukelele ulioashiria kwamba kulikuwa na ugomvi na bila shaka walinzi walikuwa nje ya ofisi hivyo walimsikia vilivyo.Wameingia wamemkuta rais akiugulia mauvimu isitoshe anavuja damu kuashiria kwamba amepigwa.

Rais Kilua alikuwa ameweka hali yake ya ujauzito siri na walinzi hawakujua zaidi yake na daktari wake tu.Siri hii ilikuwa mahsusi kuficha jambo hilo ili lisitumike kama njia ya kumwadabisha rais KIlua kuhusiana na tandabelua inayomuandama.Hakupanga kuvujisha siri hii lakini imebidi siri ivuje.

CHUMBA CHA MATIBABU

Madaktari wakiwa chini ya usimamizi wa ulinzi wa rais walifanikiwa kumshughulikia rais Kilua.Mitambo ya upumuaji alikuwa imepachikwa kwenye pua.Alifungwa mitambo mingine mahsusi kwa aajili ya matibabu.Daktari aligundua jambo moja kuwa mimba ya rais Kilua ilikuwa imeharibika baada ya kupokea pigo zito sana kutoka kwa mumewe.

“We have to save her first!”alisema daktari akifanya upasuaji wa kuondoa kijusi.Timu ya madaktari wengine walikuwa kwenye chumba kile wakimshughulikia bimkubwa hali ilikuwa tete na sasa mambo yamebadilika sana.Kilua alikuwa chini ya mikono salama.Tayari walikwisha pasua tumbo na sasa walikuwa wakifanya kazi ya kuondoa kijusi kile.Ni fedheha kwa mwanamke kupoteza mtoto!

“The baby is gone!”

Mashine za chumba cha upasuaji zilisikika zikitoa milio kuonesha shughuli ilikuwa pevu.Hali ilikuwa kwenye hatari ya ponya niponye.Wapo waliotoka jasho palepale maana rais wan chi alikuwa matatani.Upepo ulikuwa unabadilika sasa.

***

Taarifa za rais Kilua kuingizwa chumba cha upasuaji zilipenya hadi kwa Serambovu.Alipata kupitia pandikizi wake katika ulinzi wa rais alimtumia ujumbe.Kwa Serambovu huo ulikuwa ushindi mkubwa sana na aliamua kuutumia kwa nafasi iliyo bora ili mambo asije kuyabananga!Alichokifanya aliwasiliana na timu yake ya THE BIG BOYS kuwapa taarifa.

“Wakuu kama nilivyosema mheshimiwa yupo hoi.”

“Ni vizuri tunaweza kutumia nafasi hii kuchukua nchi.”

“Hayo ni mapinduzi siwezi kujihusisha na uhaini.Nimeshatengeneza jina siwezi kuwa rais aliyempindua mwenzake.No kwa hilo naomba mniwie radhi wakuu.”alijitetea bwana Serambovu akijitahidi kujitetea.

“Hii ni nafasi yako itumie vizuri.”

“Kumbukeni rais Kilua hana baraza la mawaziri kwa nafasi kama hii hatuwezi kumuondoa madarakani.”
“Akiwaa na baraza bila shaka wewe hautakuwa na nafasi ya kushika wadhfa wake.Tumia mwanya akiwa hapohapo hospitali wa wewe kutwaa madaraka.Kill her then we take power.”

Serambovu alijikuta akiwaza sana japo alikuwa tayari kufanya makubaliano lakini isingekuwa kwa namna ile.Bado Kilua alikuwa mzazi mwenza na asingekuwa tayari kumuondoa madarakani kwa mtindo ule.Tayari alikuwa ameandika makala iliyomhusu Dedani na tayari amekwisha isambaza kwenye mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari.Ilikuwa nafasi ngumu sana kwa yeye kumzimisha Kilua.Upepo ulikuwa umebadilika baadaa ya Dedani kumjeruhi mkewe hadi akapoteza ujauzito na sasa Serambovu alikuwa anashauriwa kuchukua madaraka.Ilikuwa hatua ngumu sana kwake.

“Kwanini mmeamua hivi?”
“Tumegundua Kilua ni imara kila siku anakuwa imara zaidi na tusipo muondoa maapema tutaambulia hasara.Anatakiwa aondolewe kwa gharama yoyote.Unatakiwa kuchukua madaraka kwa nguvu.Tuna watu wetu kwenye jeshi watakutetea.They will appoint you as president.”

“Kwanini tusingoje apone?”
“Kama akipona jiandae kubeba msalaba wa wewe kuitwa msaliti.Tutathibitisha ulisuka mipango ya kumteka mumewe na mwanae.Automatically hautapona!”sauti ya upande wa pili ilijibu.

“Lakini sioni umuhimu wa kutwaa madaraka kimapinduzi taifa litayumba.”
“Serambovu sisi tumewekeza pakubwa kupata mafuta ya taifa lenu.Hatupo tayari kukubali hasara hiyo itokee.Uongozi wa rais Kilua ni mwiba na mpaka sasa ameonesha nia kwamba anatujua na yupo tayari kukamata wote waliohusika na mauaji ya rais Kisusi.Upembuzi wetu umethibitisha kwamba kuna uwezekano rais Kilua alipata file nambari 13:14 nakujua vyote vilivyomo.Hadi sasa kuna mpango wa mashushushu kuja kukagua eneo lile.Hakuishia hapo ameshajua nyendo zetu na kibaya zaidi anaanza kupachika mizizi yake .Ameshasambaza upupu watu wenye uaminifu kwake wanaanza kuingizwa na mumewe.We must eliminate her haraka.”ilisema sauti kavu upande wa pili.Habari ya kwamba Kilua yumo kwenye chumba cha upasuaji ilikuwa heri kwake na sasa wangesogea kwenye hatua ya pili kutikisa taifa.

Mtiririko ulikuwa umebadilika sasa na rais Kilua alionekana kama kizuizi.Wameteka familia yake lakini wapi?Sasa ni bora kumfutilia mbali.

“Jamani tuwe makini katika hatua hii?”

“Uzembe hauwezi kutokea.Tutafanya usumbufu kidogo wakati nchi ikiwa kwenye ghasia tutaweza kuondoa lile kontena letu la vifaa pale bandarini nakulipeleka kwenye visima vyetu vya mafuta.”

“Nani atakuwa rais?”

“Wewe!”ilijibu sauti ile ikimaanisha hali ikamfanya Serambovu kujiandaa kisaikolojia kwa mabadiliko mapya yanayokuja.Lakini kichwani mwake aliona ni vyema amfanye Kilua aondoke nchini.Punde akipewa akipokonya madaraka bila shaka atamfukuza badala ya kumfutilia mbali hapo ataanzisha uhasama kati yake na Kilua kwa kumpokonya madaraka kisha atamfukuza kwa lengo lakuyasalimisha maisha yake.Vilevile kama akifanikiwa kumfukuza nchini atakuwa ameingia mgogoro na mabwana wa THE BIGI BOYS kwani atakuwa amekaidi agizo la kumfutilia mbali Kilua.Serambovu alikuwa kwenye wakati mgumu sana.

Serambovu alihisi kichwa kuwa kizito kiasi akaona upepo ulivyobadilika ni hatari kwake na hatari sana kwa taifa lake.Hatimaye mkataba wa 13:14 ulikuwa umefikia wakati mwingine.Ni kama upepo ulikuwa ukibadilika na wahusika walikuwa katika kasi ya haraka kuhakikisha upepo unabadilika.Kila anayehusika alihitajika kulishwa sumu.Serambovu alikuwa amewekwa mtu kati kalishwa na sasa aliona pia umuhimu wa kumuua Kilua.Hilo lilikuwa wazo pia.

Upepo hupima nguvu mti.Kiota ilikuwa majaribuni tena.Rais wao mpendwa yumo chumba cha upasuaji akishughulikiwa kuondoa mimba iliyoharibika baada ya kupigwa na mumewe huku nako Serambovu amelishwa sumu mahsusi yakumuondoa Kilua madarakani haraka iwezekanavyo!Dedani kitanzini kwa kumjeruhi mkewe!Shunie tayari amekwisha angukia katika penzi zito lisilo na maelezo kwa kumpenda mume wa rais Kilua.Yalikuwa ni maswali lukuki yasiyo na majibu maswali yasiyo na hitimisho kwamba nafsi hizi zitafanikiwaje?

Serambovu alikata simu kisha akaenda hadi ofisini mwa rais Kilua.Alifungua mlango bila kugonga hasa akijua yeye ndo chifu wa ikulu.Akakutana na jenerali Lupogo akiwa amesimama.Jenerali Lupogo akamuangalia Serambovu kwa umakini.

“Jenerali?”aliita Serambovu akiogopa maana alitakiwa kumuamrisha jenerali Lupogo aingize vikosi vya usalama barabarani.Wazo hilo likawa linaonekana kama mvuke.Ujasiri wake ni kama mshumaa uwakao kwenye upepo mkali kiasi akahisi yeye mwenyewe hajiamini.

“Ndiyo mkuu.Tupo tayari kuchukua oda kutoka kwako.”alitamka maneno hayo jenerali Lupogo.
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 54
Back
Top Bottom