FANANI MTENZI
Senior Member
- Jul 4, 2017
- 106
- 95
KOMBORA KIOTANI-40
BONIFACE BIRAGE
Hawezi kwenda ndani polisi wa mkamate hata iweje.Huku nikuleta skendo nyingine ambayo ingemtafuna maana hadi sasa ana operesheni ngumu sana na kkitendo cha kumzimisha bwana Twalipo ni hatua kuchafuka.Jambo hili halikutakiwa lijulikane.
“Tulikuona kupitia kamera zilizofungwa.Tupo makini sana katika usalama wa hoteli yetu.Tunaoushahidi kwamba umemuua mtu hapa hotelini.”
Dedani alitaka kumpigia mkewe kusuluhisha jambo hilo lakini hakuona umuhimu.Kichwa kilichemka huku akijiuliza a,liyemuua mlinzi wake ni nani?Wakati anawaza hayo huku akisitasita alishtukia gari ikija kwa kasi nakureeshwa mbele yao.Walishuka vijana wenye silaha kwa haraka sana nakumvamia Dedani huku wakiwadhibti wale walinzi wawili wa hoteli.Walinzi walitaka kujibu mashambulizi lakini wakazidiwa kete na vijana hao.Dedani akadakwa nakuingizwa kwenye gari.Kikaletwa kitambaa cheusi.Tukio lilikuwa la haraka sana ni kama watu hawa walijipanga wakijua hatua zote zitakavyotumika hadi kufikia kumkamata bwana Dedani.Tayari alikuwa chini yao.Kitambaa cheusi kikafungwa usoni mwake.Kisha gari ikatiwa gia nakuanza kuondoka kwa kasi ya ajabu.
Dedani alifuurukuta alihisi fika hawa waliomfuata hapa wamejipanga na itakuwa walijua uwepo wake eneo hilo.Hawahawa ndo wamemdunga kisu mlinzi wake na bila shaka hawa ni timu ya Twalipo nambari moja na bila shaka kwa kuwa wamemkamata na kama wamejua Twalipo kazimishwa naye basi hawana budi kummaliza na Dedani.Gari ilikamata barabara nakuanza kuondoka eneo lile.
Wakati gari lile linatoka kwenye geti ndipo gari la polisi nalo linaingia kwa kasi ya ajabu.Wakawa wamepishana.Dedani akawa hatarini zaidi ni bora hata polisi wangemtia nguvuni kuliko watu hawa.Sasa alikuwa kwenye mikono mibaya sana.
Gari lilikata barabara za mji huo.Dereva wa gari alijitahidi kuondoka katika eneo la mjini kuepuka shari na wanausalama.Lakini wakati akitoka mjini alishtuka kuona kupitia kioo ccha pembeni gari likimfuata kwa nyuma kwa mwendo Fulani ambao ulitilia shaka.Dereva alijihadhari nakujaribu kucheza karata zake amzubaishe huyo anayemfuatilia.Ishara ya mtu kumfuatilia ilikuwa mbaya sana kwa dereva huyu kiasi alihisi kama mipango yao sasa haitakuwa vyema na inahitajika nguvu ya ziada kudhibiti ufuatiliaji wowote unaojitokeza.Dereva aliwapa ishara vijana wake.
“Hiyo gari nyeusi naona inatufuatilia.”alisema kwa hofu.Vijana wenzake wazee wakazi walitizama kisha wote kwa pamoja walianza kuchukua silaha zao nakuzikoki!Tayari kwa lolote na kama vita na iwe vita!Vichwani mlikuwa na maswali lukuki kwamba endapo watashindwa itakuaje?Wanakumbuka walipewa onyo kutoshiriki kutumia nguvu endapo watakuwa katikati ya jiji.Hapo ingewalazimu wanausalama kuingilia kati!Na kama ingetokea hivyo bila shaka operesheni ile ingechukua nafasi nyingine kabisa.Tayari walikwisha muweka Kilua kwenye kikaango cha kumfanya atekeleze wanavyotaka ikiwemo kuweka wepesi wa mumewe kutekwa tena.Hiyo pekee kama ingesikika kwa vyombo vya usalama ingekuwa hatari zaidi na pengine wangetumia mbinu zote kulidhibiti kundi hili.Haikuwa hali nzuri kujulikana kwamba rais kawekwa mtu kati na tayari wanampa vitisho vya hapa na pale.
Walikatiza barabara kadhaa nakufanikiwa kutoka nje ya mji bila kusababisha vurugu yoyote.Walipoanza kukamata barabara iliyotoka nje ya mji walishika kasi nakuzidisha mwendo wao wakijitahidi kupotelea mbali.Lakini sasa waligundua fika wanafuatiliwa na gari iliyokuja kwa kasi.
Kitendo hicho kikawa kengele ya hatari masikioni na bila shaka walitakiwa kushughulika vilivyo la sivyo yangetokea wasiyotegemea.Mwendo wa dakika kama tano gari lililokuwa nyumba lilikuja kwa kasi nakupita mbele yao nakuzidisha mwendo zaidi.Mita chache mbeleni walishtukia lile gari likigeuka kwa haraka nakuanza kuwafuata!Lengo likiwa kugongana au ishara ya kwamba mmoja wao anapaswa kusimama.Nao pia hakuwakutaka kuonekana mabwege walikaza mwendo bila kuonesha dalili ya kusimama!Kiburi kwa kiburi.Lakini dereva watekaji aligundua jambo endapo angegongesha gari kungetokea madhara na kama angeshinda wasingekuwa na mwanya wakuondoka bila shaka gari litakuwa na uharibifu mkubwa sana.Ilibidi afikiri mara mbili kati ya kugonga na kukwepa au hata asimame aone shari ya adui ni nini?
Lakini tofauti na mategemeo gari ile ilikuja nakuwagonga huku ikiwasukuma!Mtikisiko mkubwa ulisikika!Mkwaruzano ukatokea baina ya gari mbili hadi cheche zikaonekana.Dereva aliyumba kiasi akajikuta akiachia usukani!Dedani ajigandisha kwenye kiti kukwepa mtikisiko wa gari.
Ndani ya muda mfupi gari la watekaji lilikuwa limepoteza mwelekeo nakuingizwa kando ya barabara likajipigiza kwenye mti mkubwa!Kitendo cha ghafla sana!
Gari lililowagonga lilishika breki kali.Kisha mlango ukafunguliwa ndani akatoka Shunie akiwa bastola.Kwa kasi ya ajabu aliwafuata nakuwafikia.Alifika kwenye kioo nakumuona dereva akijitahidi kutoka akamuwekea bastola kichwani!Shunie akamuamuru atoke nje kimya kimya na wenzake kisha wamtoe Dedani.Zile purukushani zilifanya waangushe silaha zao.Wakatoka huku wakiwa wameumia kiasi kufuatia kugongwa kwa gari lao.Walisimama nje ya gari.
“Hamuwezi shindana na serikali hata siku moja!Huo upuuzi wenu unaishia hapa mbwa nyie!”alisema Shunie akiwa amevaa sura ya kazi.Aliwafyetulia risasi za paji la uso wote!Kisha alimfuata Dedani akamchukua akiwa bado amefungwa.Alimuelekeza kwenye gari lake wakapanda nakuondoka kwa kasi ya ajabu.
***
Mvua ilikuwa inanyesha kubwa sana.Ilikuwa nzito iliyoshuka kuinywesha ardhi kame.Pengine ilikuja kwa furaha!Shunie alikwisha mfikisha Dedani kwenye eneo ficho ambalo hakuna kidudu mtu angewafikia.Huko aliweza kumtoa kitambaa cha usoni pamoja na kamba alizokuwa kafungwa nazo.Dedani alihisi kichwa kizito sana.Aliishtuka kuona ni Shunie ndo kamuokoa.Dedani alihisi fedheha kwa jinsi msichana huyu alivyomtolea maneno machafu.Alihisi hastahili kabisa kusaidiwa naye.Lakini sasa Shunie kawa mkombozi wake.Katokea wapi?Alijuaje Dedani yupo matatani?Ilikuwa siri kuu.
“Shunie how?...”
Shunie aliweka kidole kwenye mdomo wa Dedani akimuashiria anyamaze.Pengine hakuna haja ya kuongea sana.
“Shsss!Cha muhimu you are safe with me.”alisema Shunie.Alienda akachukua mvinyo mkali nakumimina kwenye glasi mbili kisha alikuja nakumkabidhi Dedani glasi moja.Ulikuwa ni muda wakusheherekea operesheni maalum.
“Sipendi kutumia pombe mara kwa mara.”alisema Dedani.
Shunie alitabasamu kisha akasema,”Nimeanza tangu uliponifokea.”
Dedani alitizama chini kwa aibu.Hakuona neno lakutumia kulikuwa na msongo na hali ilikuwa imechemka.Walikuwa peke yao.
“Kwani hapa tupo wapi?”
“Hapa tupo balcksite.Siwezi kukwambia ni wapi?Hakuna anayejua ulipo isipokuwa mimi.”
“Ilikuwaje ukajua nimevamiwa?”
Shunie alifikiri kidogo kisha akatabasamu,”Hiyo ni top secret samahani mkuu siwezi kukwambia.Just know you are safe with me.”
Dedani aliheshimu jambo hilo.Akakumbuka waziwazi kwamba alimshambulia bwana Twalipo na tayari ushahidi upo.Mwili wake ulihofu kama mkewe akijua na kama mahasidi wa mkewe watatumia jambo hilo kumuadhibu.
“Shunie.”
“Bee?”
“Nimemshambulia Twalipo.”
“Ndo nani?”
Ilibidi Dedani amweleze ukweli tangu apate vitisho vya bwana huyo hadi sasa.Hilo lilikuwa tishio kubwa sana na tayari limemtia doa kubwa sana.
“Ungeniambia tangu mwanzo wala usingechafua mikono yako kwa hao masaliti wa taifa.”
“Kwa aajili ya rais ilibidi nifanye hivyo.Nachukia sana wanavyomhangaisha mke wangu.Mambo yalianza kuwa mazuri lakini sasa naona kama doa linguine linajitokeza.”Dedani alikamata ile glasi nakunywa.
“Una uhakika ulimuua?”
“Ndiyo.Na ndo maana wale walinzi walisema wameona nikimshambulia kupitia kamera zao za cctv.Ushahidi wanao.”
Shunie alifikiri kidogo.
‘Kama ushaidi huo haujafika polisi au kama wanao kuna namna yakuufutilia mbali.Lakini ikiwa habari itavuja kwa umma tujiandae maana adui wa familia yako watatumia kama fimbo ya adhabu.”
Dedani alionekana kuwa na mawazo mazito sana kiasi aliogopa.Lakini uoga usingekuwa suluhu ya kutatua jambo hilo.
“Shunie nipo tayari kukupa chochote kile ila naomba unisaidie kuondoa ushahidi huo?”alisema Dedani akiwa amedhamiria.Shunie alikumbuka maneno makali aliyotolewa na bwana huyu.Hasira ilimpanda sana kiasi alitamani kumfanya Dedani amlipe kwa gharama kubwa sana.
Shunie alifikiri kisha akadhibiti hasira zake,”Dedani huhitaji kuomba.Just ask for it I will be there for you.”ilikuwa kauli iliyotoka moyoni mwa Shunie.Kitu kikachipuka moyoni mwa Dedani akajikuta akimsogeelea Shunie akamkamata nakumvuta kwa pupa.Shunie alilegea sana na pumzi kutoka kwa pupa alikuwa amesalimu amri.Kile alichoona ni muhali kutokea kilikuwa kinaenda kutokea.
Ilikuwa muda wa mahaba.Shunie akili ilihama akajikuta machozi yakimtoka sana.
“Tatizo nini?”
“Naogopa sana Dedani!”alisema akiuficha uso wake kwa mikono.
“Usiogope huenda unachohisi kikawa upande wa pili pia.”ilikuwa kauli iliyomuamsha Shunie kutoka kwenye giza.Alitafsiri fika kuwa labda Dedani anamaanisha na yeye anampenda pia ila mazingira hayakuruhusu.Dedani ni mume wa rais Kilua.Ni kioo cha jamii kuna mambo anapaswa kuyakwepa.
Shunie alimkumbatia kwa nguvu zote huku akilia mfululizo bila kujielewa kama ni furaha au huzuni.
Kilichofuata hapo kilikuwa siri yao.
Alihisi ngozi yake mkabala naya kwake.Alihisi pumzi zake na harufu ya mwili wake ilimjia vizuri kwenye pua zake kiasi ikaamsha hisia fiche za mwiii.Dedani alimsahau mkewe kwa muda.
***
Serambovu alikuwa amejiwa na mkuu wa polisi katika ofisi yake pale ikulu.Serambovu akiwa amepokea flash disk alikwisha ipachika kwenye tarakilishi yake na sasa alikuwa akitizama video iliyokuwa ikicheza.Serambovu alitabasamu kumuona adui yake akifanya shambulizi kali sana lililopelekea mtu kufariki dunia.
Serambovu akatabasamu.
“Unakopi ngapi?”alimuuliza mkuu Yule wa polisi jimbo la Capital.
“Ninazo mbili hiyo niliyokupa na moja imebaki kwaajili ya usalama wa polisi.”
“Ulitaka kufanyaje na ushahidi huu?”Serambovu alimuuliza.
“Hii ni familia ya rais.”
“Rais Kilua anafuata sheria sana sidhani kama atalegeza jambo hilo.Jiandae na upelelezi na popote Dedani atakapoonekana akamatwe haya ni maagizo kutoka ikulu.Sheria ni sheria tu.”alitoa kauli hiyo bwana Serambovu akijiandaa kwa bomu.
“Lakini huoni kwamba tutamuathiri rais Kilua?”
“Mimi ndo chifu wa ikulu kauli ya rais inapitia kinywani mwangu nakuagiza popote atakapoonekana Dedani kamateni yeye.”alisisitiza Serambovu.Ilibidi mkuu wa polisi aondoke huku akiacha maswali lukuki itakuwaje?Serambovu alifungua microsoftword tayari kuandika makala ndefu inayo husu kuhusika kwa mume wa rais Kilua kwenye mauaji Hotel ya Chemchem!IUlikuwa mtihani mwingine mzito sana!