KOMBORA KIOTANI-36

KOMBORA KIOTANI-36

FANANI MTENZI

Senior Member
Joined
Jul 4, 2017
Posts
106
Reaction score
95
KOMBORA KIOTANI-36

BONIFACE BIRAGE

Katika kumbatio hilo na busu la ghafla Shunie alikuwa amefumbwa mbali sana kiasi cha kushindwa kukabiliana na hisia zake ambazo sasa zilimezwa na mwanaume huyu!Mume wa rais Kilua na kumfunika katika mahaba mazito sana.Msukumo uliomjia ghafla kwa kweli haukuwa na maelezo au ufafanuzi.Kwa wanasaikolojia huwezi kuitafsiri hali hii kama msongo wa hisia kali sana dhidi ya mtu wa jinsia tofauti.Mtu anashindwa kujizuia awapo naye na hukuta hata maelewano hakuna lakini wengi huishia katika anguko la penzi zito ambalo kila waonanapo ni wao pekee ndo wenye falsafa yao.

Kaupepo kadogo kalipuliza na kumpepea Shunie ambaye sasa alikuwa ameupokea ulimi wa Dedani huku manukato yake yakimfikia Dedani ambaye aliyapokea nakumsababishia pumzi zake kumpandisha kwa fujo kwa hawaa.Shunie aliivuta vizuri harufu manukato ya Dedani japo kulikuwa na mchanganyo wa manukato ambayo aliyasikia kutoka kwa KIlua lakini haya aliweza kuyapata kwa Dedani na mchanganyo wa manukato binafsi.Shunie asingeweza kujizuia.Alimuhitaji mtu huyu kwa hisia kali sana napengine kiherehere cha roho kingetulia punde kama bwana Dedani angefikia hatua ya kuishia ubavuni mwake.Lakini hakujielewa alikuta akisahau mengi ikiwemo mtu wake aliyemposa bwana Pablo na sasa hatma ya moyo wake ilikuwa kwa Dedani mume wa rais Kilua.Hupendi mtu kwa kumchagua mazingira na nyakati na hali ndizo huipeleka moyo kwenye kiota chake.

Kwa dakika kama mbili hawakuutambua uwepo wa eneo lile.Walikuwa watu wawili tu katika kumbatio zito la mahaba lilikuwa busu la kuvutana na kila mmoja akitaka kuwa zaidi ya mwingine na bila shaka waling’ang’aniana.Shunie alihisi anamuhitaji Dedani nay eye Dedani alihisi anamuhitaji Shunie pengine ule mshawasha wa kumuwaza nakumfikiria hata wakati akiwa na mkewe alihisi anakuuiona na kuhisi manukato ya mwanamke huyu kiasi akajishuku kwamba bibi huyu anasambaa kwenye fikra zake.

Vivyo kwa Shunie alijua bwana huyu katawala fikra zake na kujitandaza kiasi cha kuziba kama

Utando wa buibui kwenye ubongo wake.

Chozi likamponyoka Shunie,”Mheshimiwa tafadhali.”alisema Shunie akijiondoa kwenye himaya yenye joto.

“Sorry Shunie please forgive me.”alisema Dedani kwa pupa huku akizidiwa kwa kuhema kwa fujo.Wote walihema roho zikiwaenda mbio.Kila mmoja aliutamani uwepo wa mwenzake lakini uhalisia haukuwa ruhusu.Pengine hakuna aliyejua kwamba kwenye mioyo wamekwisha salitika.Walikuwa wameivana.Lilikuwa penzi la ghafla ambalo halikuwa na ufafanuzi nap engine wao wenyewe hawakujua kama kweli walikuwa wanapendana au ni tama tu ya ngono ilikuwa imewapa mshawasha usio na kipimo.Kila mmoja alijaribu kudhibiti lile wazo aliloliogopa la kwamba alikuwa anamuingilia mwenzake mwenye familia yake.Alikuwa anaingilia penzi la mtu.

Wakati Dedani anataka kuondoka Shunie alimshika mkono,”Ngoja.”

Dedani alisita nakusimama.Huku moyo ukimwenda mbio bado alizihisi sakafu za midomo ya Shunie ikiwaa kwenye midomo yake ikimsugua.

“Kuna nyakati nawaza sana.”alisema Shunie huku aibu za kike pamoja na huzuni kwamba kinachotokea hakielewi kabisa.

“Unawaza nini?”
“Kwamba nakuhitaji.OOhh!Dedani nni jambo gani linanitokea?Sijawahi muwaza mume wa mtu tangu nizaliwe lakini wewe umekuwa udhaifu wangu Dedani?”Shunie alisema akilia machozi.Alikuwa anaugua moyoni.

“Unahisi kitu gani?”Dedani alimuuliza Shunie huku akimkazia macho.

“Mimi ni mtu mzima.Najua ninapoona akili yangu inabadilika inakuwa inakuwa kama ya motto mdogo.Dedani I think am deeply inlove with you!”aalisema Shunie kitu ambacho kilikuwa mwik😵le wake Kilua amsikie.

Dedani hakumjibu kitu alijikuta akizibua kofi paa!Lilikuwa kofi la mpenzi halikuuma.Kilichomuuma ni kule kuhisi anakataliwa!Labda hakutegemea kukubaliwa lakini hakuhitaji pia kukataliwa.Kilikuwa ni kitu ambacho hakiwezekani.

“Unadhani nitembee na mwanamke kama wewe unayejirahisisha kwangu?Wewe kahaba?Hivi unadhani kukushikashika ndo kwamba nakuhitaji?”Dedani akawa mkali tofauti na sifa alizopata alijikuta amebadilika sana kiasi hata yeye hakujielewa kilichombadilisha.

“Dedani usiseme hivyo?...Mheshimiwa wewe ndo uliyenibusu…siyo…”

“Na ukakubali?Ulijuaje kama nakupima?Mimi mke wangu ni rais wan chi usifikiri kuniokoa na kujirahisisha kwangu ndo kutanifanya ni kuhonge hela?”

“Mheshimiwa?Usiseme hivyo mimi siko hivyo…”Shunie alihuzunika sana.Hakutegemea kabisa alijuta kumpa mwanya bwana huyu lilikuwa kosa kubwa sana ambalo alijutia mwenyewe.Kilichotokea walikijua wao wenyewe.

“Unataka ni mwambie mke wangu?”alisema Dedani alitishia.Alifanya vile kuondoa jambo ambalo lingewaweka kwenye wakati mgumu.

“Nakubali adhabu yoyote utakayonipa.Mimi ni mtu mzima nitavumilia lakini sio kuniweka katika vita na mkuu anaweza kunifutilia mbali lakini kama hiyo ndo njia pekee basi sina budi kuibeba adhabu hii!”

Dedani alishtuka sana na hata hakujua alikuwa anasema na hakujua madhara ya maneno yake!Alichokifanya aliondoka katika uwepo wa mwanausalama Yule aakimwacha akiwa hampatilizi bali akihofia kauli zake.

***

Utulivu wa hospitali ulizinduliwa na uwepo wa mkuu na msafra wake kiasi chakufanya kila mmoja awe katika harakati.Leo Kilua alikuwa katika mazungumzo mazito kati yake na kaptein Pangabutu.

“Mheshimiwa nadhani ni wakati wa kujua kinachoendelea.”alisema bwana Kaptein kwa sauti iliyoamua kumwaga mboga zote.Sasa makadabrasha ya 13:14 yanaenda kujulikana waziwazi.

“Nakusikiliza.”

“Siruhusiwi kusema jambo hili lakini inabidi niliseme.Nilikuwa mpambe wa rais awamu Fulani.Kuna mkataba wa siri uliingiwa miaka Fulani.Taifa la Kiota liligundulika kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta.Matajri wakubwa waliona fursa hivyo ikawapasa kuchangamkia tenda hii.Lakini ilibidi wawe na mnyororo utakaowazubaisha waafrika kwa minajili ya wao kutimiza adhma yao.Mnyororo huu ulikuwa na vitengo ambavyo vinashikilia mkataba.Hawakutaka taifa linufaike kwa jambo hili.Walitaka wakamate uchumi wa mafuta na njia pekee nikuingilia muundo wa serikali yetu.Walishawishi rais wa kipindi nilipokuwa mpambe wake.Alitaka kuingia lakini masharti hakupaswa kuwa na hisa kwenye mradi yeye alitakiwa tu awe mwezeshaji wa mpango huo.Alilipwa fedha nyingi sana.Shughuli za uchimbaji zilitakiwa zipelekwe bungeni iundwe sharia lakini kwa mujibu wa wakubwa wa mpango huo hawakutaka sheria yoyote iwekwe maana Kiota ilikwisha kumbwa na demokrasia yenye nguvu na watu walikuwa werevu kiasi ingeleta ugumu.”alisema maneno hayo huku Kilua akirekodi kupitia simu yake.

“Kwanini waogope sheria kutungwa?”

“Ingewadhibiti kupata asilimia 100% za rasilimali zetu.SO ilitakiwa wasuke mnyororo na huo ni special kwa kutumia njia za panya.Faili nambari 13:14 ndo mnyororo wenyewe uliosuka ni dhana inayofukuta kuwahujumu wanaoingia.Baada ya kuusuka wakawekwa watu wakuutekeleza.Aliyeingia alikula kiapo cha siri no turning back.Mnyororo huu umekuwa na masharti magumu na kila aliyediriki kwenda kinyume alifutiliwa mbali na wengine kuingizwa.Simple mistake they finish you!Viongozi waliokuwa tawala zilizopita wale waliouawa kwenye ajali pamoja na serikali ya Kisusi wapo waliofanya uzembe kwenye mnyororo na The Big boys wakatoa amri wafutiliwe mbali.Rais Kisusi alitishiwa kuondolewa madarakani ndani ya muda mfupi.Alikuwa na wasiwasi sana hata alipokuwa ikulu kila hatua ilikuwa inaonekana na alihisiwa hatarini maana na yeye alianza kusuka mpango wa kudhibiti mnyororo huo lakini ulikwisha anza kuzama.”alisema bwana Pangabutu nakumfanya Kilua kuhisi kijasho chembamba kikimtoka alijaribu kuunganisha matukio akajuafika kila kitu kilikuwa ni mpango maalum.

“Kisusi alijuafika siku zake zinahesabika japo mkuu wake wa majeshi alimuhakikishia usalama but The big boys walikuwa hatua nyingi mbele.Wakaaamua kumzima kabisa.Rais awamu iliyoanzisha mnyororo alijuafika kalisaliti taifa na alijua Kisusi angeemuumbua hivyo alipanga kuonana nae siku ile ya sherehe za uhuru na baada ya pale angemwaga mchele wote.Aliwaambia baadhi ya waliokuwa kwenye mnyororo ambao yeye aliingia nao akijua ni watiifu.Lakini siri ilivuja kabla.”alisema hivyo akaomba maji anywe.Ilikuwa kama picha simulizi ya kutisha alikuwa anahadithiwa.

“Ikawaje?”

“Ndo ukapangwa mnyororo kuvunjwa lakini kabla ya sherehe za uhuru miezi sita nyuma waliamua kubadili mzunguko.Ikiwemo namna taifa litakavyokuwa huko mbeleni baada ya Kisusi kuondolewa madarakani.Kuna mabadiliko ya kikatiba yalifanyika katika uongozi kuhusiana na mtiririko wa kurithi madaraka ulivyo.Mtiririko huu kwa mara ya kwanza ulimpa mtu mwenye cheo cha ugavana wa jimbo kushika nafasi ya urais endapo waliopo kwenye mtiririko hawapo.Walimtaka gavana dhaifu asiye na makucha.Jimbo la Kibatari lilikuwa sehemu nzuri kwani gavana wake hana nguvu ya Umma maana huteuliwa na rais na sio uchaguzi wa wananchi.Huyu waliona ingekuwa rais kumpelekesha.Wewe ulikuwa shabaha.Kwa muda Kibatari huonekana kama ugenini hasa tukijua eneo hili lilichukuliwa kutoka taifa la Savanna landa miaka mingi iliyopita wakati wa vita.Inasemekana wakazi wengi wa Kibatari ni asili ya Savanna Lands na tayari rais wa Savanna Lands alikuwa kwenye mnyororo.Yeye angetumika kama chambo kukushawishi lakini uliwashtua nakuwa na nguvu sana kiasi ikabidi waweke uadui mkubwa kati yenu.”

Kilua aliduwaa mambo yalikuwa mazi.

“Kwanini watuchonganishe?”

“Alitaka ubwana wakati alikuwa kitwana.”

“Duh?”

“Sasa wewe mbona hawakukufuata siku zote.”

“Niliwekwa mahususi kuja kuvumbua haya namuamini sana Mungu na hakika kanilinda kuja kusema ukweli ni jinsi gani mambo yantendeka katika bara jeusi!Ukitaka kuwamaliza watu watengenezee theory Fulani wahangaike kupambana nayo huku wao wakiwa tayari wamepigaa hatua ndefu.”

“Agent Shunie alikuwa amepiga picha meli Fulani na kwa mujibu wa upelelezi wake vilikuwa vifaa vya kuchumbia mafuta.”alisema rais Kilua.

“Sishangai na sasa wamefikia hatua yakuleta vifaa huo ni ubabe mkubwa sana.”

“Vifaa hivi bado vipo bandarini na hadi sasa meli yao haijafanyiwa clearance japo kwa mujibu wa taarifa hazioneshi ni nani kaziagiza na mara kadhaa wametaka kutumia muhuri wa ikulu.”

“Ndo hatua zenyewe.”alisema kisha akanywa maji.

“Unashauri nini kifanyike.”
“Kuna watu wengi wakuwekwa kizuizini kitendo tu cha kusababisha ajali ile ni sawa nakuondoa serikali madarakani ni kosa na wanahitaji kusakwa kuleta maafa kwa taifa.Unatakiwa uanze mabadiliko ya hali ya juu najua bado hujaunda baraza la mawaziri hivyo ni bora kulitengeneza kwanza.Ila uwalinde siajabu wakauawa hata kabla hawajaapishwa.”

***

Shunie akiwa hajielewi kitendo cha kutishiwa kusemwa tu alihisi dunia inambadilikia bila kufikiri alienda hadi kwenye roshani tayari kujitupa aangukie kichwa apasuke afutike duniani hapo moyo hautaumwa.Kulikoni kuwekwa nguvuni na rais Kilua bora ajiondoe kabisa uhai!Shunie alianza kujihesabia hatua namna atakavyoruka!Alijisogeza hadi ukingoni mwa roshani akapanda zile chuma tayari kujirusha!Mapenzi yalimharibu Shunie.
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 57
Back
Top Bottom