KOMBORA KIOTANI-35

KOMBORA KIOTANI-35

FANANI MTENZI

Senior Member
Joined
Jul 4, 2017
Posts
106
Reaction score
95
KOMBORA KIOTANI-35

BONIFACE BIRAGE.

“Unasemaje?”aliuliza Kilua akiiwa anamshangaa Serambovu kwa kauli zake za matisho.Ilikuwa fedheha sana kwa upande wake na hakutegemea kama watu hawa watafikia hatua ya kumtishia kwa namna moja au nyingine.Serambovu alikuwa amevuka mipaka sasa.Ilionekana kwamba ana sauti kuliko vile Kilua alifiikiria na ilikuwa ni lazima Kilua ameze kiburi hiki lasivyo operesheni muhimu za kubaini watekaji wa mwanae zingefika tamati bila yeye muhusika kumaizi hasa ni nani muhusika mkuu kwenye mtandao huo.Kilua alikereka lakini akajikuta akiigiza kwenye maigizo hayo.

“Nimesema simtaki Dedani hapa ikulu!”aliurudia tena bwana Serambovu na sasa ilikuwa ni amri nasio ombi kama vile ilivyoonekana.

“Siwezi kufanya hivyo.Huyu ni mume wangu ningehitaji utulivu wenu.Nipo katika wakati mgumu sana kwa sasa iweje na wewe uwe problem?”Kilua alijaribu kumdhibiti bwana Serambovu kistaarabu pengine angemtuliza bila kuwa na hisia zozote.

“Hapana mimi simtaki.Kumbuka tuna mtoto!Dedani hapaswi kuwa na hiyo familia ni yangu mimi!Mimi ndo mtu wako tena damu kabisa tunashea kwa kuzaa!”

“Tumedumu sasa kwa kipindi kirefu na tume-survive bila kuachana.Sitegemei kwa sasa ukate tamaa kiasi cha kunidhalilisha na kuniweka katika wakati mgumu kiasi hiki?”alisema Kilua kwa upole.

“ Siyo kukuweka katika wakati mgumu bali napigania penzi langu kwako na hilo ndo la muhimu.Mimi ni mwanaume anayeithamini damu yake kuachwa bila kupigania ni kitu cha kizembe nahisi kuwa mbogo!”alijitetea Serambovu akiwa amedhamiria kuonesha nia yake.Angejidhibiti lakini hasira zilimzidi kiasi akajisahau kabisa kwamba kulikuwa na nini mbele yake.Hilo lilikuwa pigo kubwa sana kwake na kwa upande wake na kwa upande wa Kilua.Huku kujiachia kizembe anakokuachia kuna jenga picha ya jinsi gani alivyo na uhitaji wa kummiliki Kilua ambaye kwa sasa amempata mume wake.Uhitaji huu una hatarisha usalama wa Kilua.Pia nafasi ya Dedani anaitia mashakani.Kwa sasa Kilua alimuhitaji baba wa watoto.Pia angekuwa mbioni kuonekana katika hafla mbalimbali za kitaifa pamoja na familia yake.Kumtenga na mumewe ni kitu ambacho hakikuleta maana.Kulinda heshma na penzi lake kulimgharimu sana bwana Serambovu na kumdhooisha kifikra.Ilionekana ni ngumu.Pamoja nakuwa alipachikwa ikulu kama shushushu wa wanyonyaji lakini alitakiwa acheze karata zake kiakili au angezidi kupoteza.Hisia zake zilimzidi akasahau kwa kuteleza katika mipango yake.Na kama wakubwa wake wangelijiua hivyo bila shaka angekuwa katika wakati mgumu sana.

“Serambovu please behave well don’t be one of my problems.”alisisitiza Kilua akiwa na umakini huku akizidi kumpatiliza.

“Nakupenda Kilua?”alimjibu kwa kujiamini.Lakini haukuwa wakati wake kwa rais kumtilia maanani na sasa Serambovu kaonekana king’ang’anizi na kama mdudu aliyeingia sikioni huku akikera sana kwa hatua zake.Alishaharibu na sasa umimi unazidi kumpotezea imani kama mtu aliyeaminika sana na Kilua.

Kulikuwa na mengi ya taabu.Bila kuchelewa Serambovu alimvutia Kilua kwake kwa nguvu nakulazimisha busu la nguvu lakini aliona kwa mara ya kwanza Kilua akimkwepa kutoka moyoni hiyo ilikuwa ishara mbaya kwake!Alijichukia sana na kuhisi kasalitika kwa ujio wa Dedani hata zile busu za kuiba tangu enzi zao ni kama leo zimefika tamati!Hakuweza kusadiki jambo hilo hata kidogo na kutoka moyoni alichukizwa sana na kitu hicho.Serambovu alijikuta akilazimishwa kumuachia Kilua.

“Busu na pambaja zangu zimekuwa kama miiba?”alihoji pointi huku akimkazia Kilua macho kwa umakini wenye wingi wa huzuni.Kwa mara ya kwanza alihisi moyo wake kusagikasagika kama unga!Dedani heri usingetoka huko ulipokuwa.Alilaani sana kwa hatua hizo.

“Zimekosa mpapaso na ulaini wa Hariri.”alisema Kilua akijikaza.

“Mapenzi yana wenyewe.”alijibu Serambovu kwa kusikitika sana.

Ukimya ulipapasa na kuzuia ndimi zao kusema na kutenda kwa muda huku sakafu za mioyo zikipashwa na joto.Hapa Serambovu alihisi mengi sana huku akisaka maneno yenye rutuba kupunguza sintofahamu zilizoikumba dunia yao.Kiota alichohisi kukimiliki kilikuwa kimetwaliwa himayani mwake na sio riziki dhiki iliyomkumba alisawijika nafsini.

Kilua alipiga hatua kuondoka huku akijisemea,”Penzi langu kwa hawa wawili ni kama chungu na sufuria.Moja penzi lake linapata moto polepole kama chungu.Mwingine ni sufuria kutia kwenye moto linawaka kwa haraka.”alijiwazia akizungumza mwenyewe.Fumbo hilo likabaki mtimani.

Alielekea moja kwa moja hadi kwa mumewe.Alimtizama akijua fika bado ana hasira sana nay eye.Alimsogelea nakuketi karibu naye.Ukimya ukatawala ila palepale mlango ulifunguliwa wakaingia kina Masha pamoja na Toti wakiongozana na Shunie.

Wote walimpa salamu rais kwa mpigo kisha wakaomba faragha ya mazungumzo naye lakini Kilua aliomba waseme naye palepale.

“Mheshemiwa hili ni jambo la usalama wa taifa tunaweza zungumza faragha na simbele ya mtu mwingine.”alipendekeza bwana Toti.

“Hapana mnaweza zungumza mbele ya mume wangu.Ninavyojua anahusika sana katika zangu hadi sasa alikoswakoswa kupoteza maisha dhidi yangu.Anapaswa kushiriki katika hili.”

Toti walitizamana pamoja na Masha wakaona ni vyema kumshirikisha bwana Dedani.Pia rais Kilua alihitaji ushirikiano na mumewe hasa kwa jinsi alivyokuwa anapitia vipindi vigumu sana kiutawala.

“Mheshimiwa tuna ripoti kuhusiana na kuuawa kwa balozi wa Savanna Lands katika ardhi yetu.Ripoti za uchunguzi wa kina zinaonesha ni kifo cha kuuawa.Na muuaji alijua anachofanya na alikuwa mfanyakazi wa palepale hivi tunavyozungumza kikosi chetu kiliweza kumtia nguvuni.Kutokana na ulinzi uliokuwemo ilikuwa ni rahisi kujua mtekelezaji wa jambo.Pamoja na kumhoji sana mhusika hajaonesha nia ya kusema ukweli.Tumemweka kizuizini kwanza.”

“Hii italeta mzozo na Savanna Lands tena mkubwa sana.”alisema Kilua akiwatizama wasaidizi wake.

“Tunalitegemea hilo na hata majeshi yetu yapo makini sana kwa sasa pamoja na vyombo vya usalama.Kwa hatua tuliyofikia tangu wakati ule tunangoja timu ya wanadiplomasia wasimamie mazungumzo haya japo sidhani kama mauaji haya yatapita bila kuwa na maswali.Wanaweza sema sis indo tumemmaliza na hatujamlinda hata kumfikisha mahakamani.”alishauri Masha kwa msisitizo.

“Tunatakiwa kuwa na kauli ya kuridhisha jambo hili lisije kutumika kama fimbo kwa rais wa Savanna Lands atalitumia kuniandama kimataifa.”

“Mheshimiwa nadhani tunajuafika huu sio mkono wa serikali wala vyombo vyetu.Hii ni mipango ya huu mtandao naweza uita wa kigaidi kwa namna nyingine.”alisema Shunie.Macho ya Dedani yalikuwa yakimwangalia kwa namna Fulani huku yeye mwenyewe akikabiliana na mtizamo huo.

“Huu mtandao ndio ulioteka familia yako kwa sasa tunahitaji maelezo kwa Pangabutu.”

“Pangabutu anaendeleaje?”aliuliza rais Kilua.

“Kidogo anahafadhali.”alijibu bwana Toti.

Kilua alifikiri kidogo kisha akasema,”Nataka kwenda kumuona sasa hivi.”alisema Kilua huku akichukua simu nakuongea na mkuu wake wa usalama kumueleza kwamba anahitajika kwenda hospitali kumuona mtu.Ndani ya muda mfupi ikulu ilishughulika kwa ziara ya Kilua kwenda hospitali kumjulia hali bwana Pangabutu.

“Toti nataka tuwe pamoja tunakwenda hospitali kuna kitu ataniambia akiniona mwenyewe.”alisema Kilua.Wote walitikisa kichwa kwa hatua hiyo kuonesha inakubalika sana.Kilua pia alimgeukia mumewe,”Please my love be with me today.First public appearance.”alisema Kilua akimshika mumewe mikono huku akimtizama machoni.Dedani hakutaka kuwaonesha watu kama kuna mgomo baridi kati yake na mumewe.Alichofanya alijibu kwa kuitikia kama kumpa ushirikiano mkewe.

Baada ya muda msafara wa gari ulianza kuelekea hospitali alimolazwa kapten Pangabutu na vile alikuwa mtu muhimu kwa taifa ilimlazimu mkuu wa majeshi kuungana nao katika hafla hiyo.Pikipiki zilitangulia mbele kusafisha barabara isiwepo gari lolote lile wakati rais KIlua akipita eneo hilo.Ukaja msafara wa gari za polisi ambazo zilikuwa tayari kwa gari lolote kama lingetokea kuleta fujo basi lingeshughulikiwa vilivyo.Magari ya usalama yalisheheni kwa wingi huku kikosi maalum cha udunguaji kikiwepo katika msafara huo.Kikosi maalum kilitangulia kwanza hospitali na kuchukua wadhfa wa usalama ikiwemo kuwaweka tayari wadunguaji sehemu fiche za siri wakikagua usalama kwa rais Kilua kuzuru hospitali hiyo.

Wanausalama waliovalia kijeshi pia walikuwepo wakiwa na silaha zilizotayari kama tu ingetokea hatari yoyote kwa Kilua.Dedani sasa alionja joto ya nguvu iliyopo kwa mkewe.Kilua alikuwa rais wan chi anayelindwa kama mboni ya jicho.Usalama wake ulikuwa muhimu sana wa kutilia maanani.Mtu hutafuta pesa,penzi na nguvu.Kilua alipata pesa na penzi kwa Dedani na Serambovu sasa alipata nguvu!Nguvu ya kutawala na kutumikiwa na kusikilizwa.Dedani alihisi hata kumuogopa mkewe kwa ulinzi aliokuwa nao sio wa kawaida.Hii ilikuwa nguvu kuu!Muda huo wote Kilua alimshika mumewe mkono huku akifanya kama kuiminyaminya kwa upendo.Alijua moyoni alimuhitaji mumewe lakini hakujielewa alihisi kwa upande Fulani Serambovu aliutawala moyo wake.Ila alijua moyo wake kwa mara ya kwanza tangu aingie kuwa rais umekuwa na mabadiliko makubwa sana hasa akiwa ameonja joto ya jiwe kwenye kidonda.Sasa aliona mambo kwa mtizamo tofauti.Alikuwa na nguvu.

“Power is everything in life once you have it you control things.”alijiwazia na kwa kiburi hicho cha nguvu angefanikiwa kumdhibiti Dedani pamoja na Serambovu!Baada ya muda mfupi walifika hospitalini hapo.Msafara uligesha magari yao kisha wakashuka wanausalama na kutengeneza mzingo maalum kwaajili ya rais.

“Secure the perimeter CIC CLEOPATRA is on the move.”alisema mkuu wa usalama bwana Ditto kupitia kifaa cha masikioni na kila mwanauslama alipata taarifa hiyo.CIC CLEOPATRA ndo jina la siri la utambuzi wa Kilua kwa siku ile.

“CIC CLEOPATRA cleared ALFHA TEAM SNIPER SHOOT ON TARGET!VULTURE TEAM SECURE THE ENTRENCE ZONE.MOTHER TEAM EYES ON AIR BIRDS 1 2 3 CLEAR THE SKY.THE AREA IS SAFE!”Ditto alizidi kupasha taarifa kwa lugha ambayo wanausalama pekee waliieelewa.

Kilua alishuka wakishikana mikono na mumewe wakaelekea hospitali ndanI.Ilikuwa mara ya kwanza kwa Kilua kuonekana na Dedani katika sehemu ya umma.Hata waasaidizi wa Kilua walifurahi sana kwa jambo hilo wapo waliojua Serambovu alikuwa na mchezo Fulani lakini kwa ujio wa Dedani wakawa na imani kwa tabia ya Kilua kubadilika.

“Asante mme wangu kwa kuja na mimi hapa.”alisema Kilua akiubinya mkono wa Dedani kwa hamu.Dedani alionesha tabasamu kwa mkewe jambo ambalo lilizidi kumtatiza Kilua.Alijua hasira ya Dedani ilikuwa inamtafuna kimyakimya lile tabasamu halikuwa halisi bali maumivu makuu.

“Tuko pamoja.”alisema Dedani kuhakikisha.Walienda hadi alipo Pangabutu.Walimkuta akiwa chini ya uangalizi mkali sana.Kilua alimpa salamu pamoja na mkuu wa majeshi.Walimpa pole akiwemo katibu mkuu bi Saada.Pangabutu alifarijika sana kwa ujio wa rais Kilua.Huu ulikuwa ushindi kwake ingawa alijuafika kuna hatari itazidi kummendea.

“Tunakupa pole pia tunakuombea kwa Mungu upone haraka.”alisema Kilua akijaribu kumpa tabasamu.Tabasamu lilikuwa la moto hata wanaume waliokuwa pale walikubali kwamba KIlua ni chuma.

“Nashkuru mheshimiwa aasante sana.Mungu akubariki…Nimefarijika sana kwa ujio wako hapa.”alisema Pangabutu hadi akahisi kububujikwa na machozi.Kilua alimfariji kwa kumshika bega.

“Naomba uwe na amani taifa lipo kwaajili yako.Mimi nipo kwaajili yako.Nakuhakikishia usalama!”

“Ila mheshimiwa naomba faragha na wewe wabaki Masha na Toti.”aliomba Pangabutu.Alijiandaa kumwaga mpunga!Kilua aliwapa ishara watu wengine hadi mkuu wa majeshi hakupaswa kuwepo pale jambo ambalo lilimuogopesha sana jenerali Lupogo akijua bado yupo kwenye karata za Kilua.

Chumba kikawa salama kwa Kilua kuzungumza.Dedani alitoka akawa anaenda huku akizunguka alijiskia kwenda msalani alienda huko moja kwa moja.Kweli kichwa chake kilikuwa kizito sana kiasi hakuangalia alikuwa anaingia maliwato gani alijikuta akiingia maliwato moja nakugongana na mwanamke kifuani!Kuja kutahamaki alikuwa ni Shunie.Walijikuta wakitizama kwa hisia kali sana.Huku midomo ikichezacheza na kama kaupepo Fulani kakipuliza na nywele za Shunie kumchezacheza huku macho yake ya kike yenye ulegevu Fulani yakimtizama Dedani.Shunie aliijua saikolojia ya Dedani nay eye mwenyewe alijijua tayari moyo wake umeshakuwa mtama na sasa nafsi inasukumwa kama chapatti kwa uwepo wake na Dedani.Lilikuwa kosa kubwa sana kwa wawili hao kukutana katika mazingira yale.

Leo walikutana sehemu hii iliyo na ulinzi mkali sana hasa kwa uwepo rais.

Shunie ulimi ukawa mzito!Akimuona Dedani tangu tukio lile amekuwa hajielewi kabisa kuna lugha ambayo ilizungumza kihisia kati yao nahakuna aliyetayari kukiri jambo hilo.

“Mhh samahani sikujua kama…”mlimi wa Dedani ukawa mzito sana.Alitaka kupiga hatua na alijikaza kweli akapiga hatua kutoka nje ile anafika mlango alijikuta dhamira ikibadilia nia.Akamfuata Shunie kwa kasi nakumsogelea.Pengine yangesikika mashairi ya THE SONG OF LAWINO.Au tungesikia maneno matakatifu kutoka kitabu cha Suleimani WIMBO ULIO BORA.Au taratibu ala za kilatino,kifilipino na hao kina India.Msukumo mzito wa kisaikolojia ulimkumba Shunie!Alijikuta mikononi mwa Dedani bila kutarajia!Yakapita maneno kichwani mwa Shunie na Dedani.

HATA JUA LIPUNGE,NA VIVULI VIKIMBIE

NITAKWENDA KWENYE MLIMA WA MANEMANE,

NA KWENYE KILIMA CHA UBANI,

BIBI ARUSI,MIDOMO YAKO YADONDOZA ASALI,ASALI NA MAZIWA VI CHINI YA ULIMI WAKO:

Dedani alijikuta akifuata papi za midomo ya Kilua kwa msukumo wa hisia zilizobubujika kama kijito.Lilikuwa busu la hiyari…
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 65
Back
Top Bottom