FANANI MTENZI
Senior Member
- Jul 4, 2017
- 106
- 95
KOMBORA KIOTANI-33
BONIFACE BIRAGE
Balozi alikwisha kaata roho!Hangaiko la kutetea uhai wake lilikwisha nguvu na sasa aliona na kuhisi wepesi ulioambatana na usingizi mzito sana vikimjia kwa pupa na hatimae uhai wake ulififia na roho iliponyoka kifua chake pamoja na nafsi vikaenda katika ulimwengu wa roho.Balozi hakuwa hai tena alikuwa amefariki dunia!
***
Kilua alimsogelea mumewe aliyekuwa akimngoja katika moja ya vyumba binafsi mule ikulu.Alimuacha Serambovu upande mwingine huku akiwa ametoa amri afunguliwe pingu.
Kilua alikuwa na shauku kubwa kuonana nae baada ya muda mrefu sana kuwa nae mbali na sasa alikuwa amerudi hakujielewa kama alimpenda au ni ule ukaribu kwa sababu ni mume hayo yalikuwa mawazo gongana na majibu kinaya.Pengine hakujua lolote.Kwa dakika kama tano alijikuta akimtizama mumewe bila kusema kitu huku biwi la machozi llikicheza ngoma kwenye mafiga ya machozi.Machozi yalimtoka akajikuta akimkimbilia mumewe nakumrukia akamkumbatia kwa nguvu mwilini mwake.Dedani aliipata tena harufu ya manukato ya mkewe.
Alinukia kama malaika kwa utuli wa kupendeza pua.Utuli wa mwanamke wake!Mke aliyemkumbatia sasa alikuwa mbele yake.Ohh ni jinsi gani Dedani alimpenda Kilua kuliko vile alivyodhani.Alimpenda sana!Anamkubali moyoni mwake.Mama wa watoto wake.Mke wa ujana wake na nguvu zake.
Kwa dakika kama tano alikuwa amemkumbatia mkewe asimuachie na alitaka hivyo.
“Dedani wangu nifuate.”alisema Kilua akimshika mkono mumewe.Wakaenda pamoja hadi chumbani mwake walinzi waliombwa faragha na rais Kilua aliyekuwa na mumewe.
“Dedani unaendeleaje?”aliuliza Kilua akimshika mumewe usoni akimkagua aliona makovu kadhaa aliyopigwa alijua babie wana alikuwa katika maumivu makali sana kiasi hakuwa kawaida.Kilua alirudia tena kumkumbatia mumewe kama mkewe.Hungedhani alikuwa akichepuka na Serambovu bila breki.
“Binti yetu.Shani wetu anateseka Yule mwendawazimu anamharibu mtoto.’’alitoa habari bwana Dedani japo hakutaka lakini Kilua ni mamake Shani anapaswa kujua madhila ya mwana wake.Kitendo cha mwana wao kubakwa kilimuumiza sana Dedani nikumbukumbu mba6a sana kuwahi kutokea.Ni kweli binti yao katumbukizwa kwenye giza nene la unajisi.
Kilua alijikuta machozi yakimtoka sasa alijua fika ajali ya kifo iliyoondoa serikali ya Kisusi ilikuwa ni mpango na walijua yeye ndo raisi ajae hivyo mwanae kutekwa ulikuwa ni mpango wwa kuja kumtumia kama chambo.
“Tell me what happened?”aliuliza Kilua akiwa na shauku kuu.
“Nilipokufumania na Serambovu,ilikuwa siku mbaaya sana maishani mwangu na wala sikutegemekama ingekuwa vile kwa kweli.Nilikuwa na msongo wa mawazo na akili kufa kabisa.Ajabu nikaenda bustani ya mjini hapo ndo nilitekwa hawa watu wanajua mengi kukuhusu na hata mimi.Walianza kwa kunitumia meseji za ajabuajabu hapo walikuwa wananivutia niingie kwenye gari lao.”alieleza tukio zima llilivojiri hadi walipompeleka na sasa walikuwa wawili yeye na mkewe wawili tu kama ilivyo paswa kuwa tangu enzi ya ndoa yao.
Kilua kila akisikia usaliti wake na Dedani alihisi kama upanga unapita kwenye nafsi yake ukimsuta.Ni saw mume kuwa na hasira nae kwa jinsi alivyomtenda hata aliona hadhi ya kiti chake imeshuka mbele ya mumewe.
Dedani alitamani sana kumvutia mkewe dhidi ya shutuma za fumanizi lakini alijua huuyu ni mama kumletea shutuma zile na hivi ni rais ni kuzidi kumsumbua kichwa lakini vipi kuhusu yeye.Rais lazima ajue mipaka yake na sikuonea watu kijinga.Kabla yakuwa rais Kilua alikuwa mwanamke wake na hakupaswa kabisa kuingiza cheo kwenye mambo yao binafsi.
Lakini kifua kikawa kizito kwa dedani kubeba mambo hayo.
“Pole sana mume wangu.”alisema Kilua akijihisi hatia kwamba kazi yake imeleta kombora katika ndoa yao na sasa imesambaratisha kiota cha mapenzi yao.Ni kama hakumjua mumewe tena na penzi lao lilififia shauku penzi ni kama haikuwepo kuja kwake Dedani kahisi kitu kipya.Pengine hatia ndo inamla.Kilua alihitaji mtuu wa kuzungumza nae na kumueleza anachojiskia.
Lakini alihisi mtu huyo si Dedani.Aliona haya kumueleza au kuzungumzia hatma ya ndoa yao.
“Namuwaza Shani wetu najihisi vibaya sana kuwa mbali nae sijui zee Kavu atamenda nini?”alisema Dedani akiwa na wasiwasi mwingi sana.Wote wawili walikuwa na dukuduku moyoni kila mmoja alitaka kumwambia mwenzake anachojiskia lakini walikuwa na kigugumizi
“Kama mama kuna wakati naumia sana sijui kama amekula sijui wamemtenda nini ulichoniambia kwangu ni mateso makubwa nahisi utendaji kazi wangu utaathirika kwa namna moja au ninyingine.Lakini najitahidi kuna vita kubwa napigwa na hawa wanaharamu.Wanataka kuniangamiza na kuiangamiza nchi.Tayari nina mgogoro na rais wa Savanna Lands.Ohh!mme wangu nipo katika wakati mgumu sana hadi nahisi kuchanganyikiwa.”alisema Kilua akimsogelea Dedani ambae alijilaza kifuani mwake.Alijua kwa Dedani kuna upendo hasa wa faraja.Siku zote mwanaume huyyu alikuwa mkarimu kwake.Haijalishi ni mara ngapi mwanaume huyu kamsaliti lakini bado Dedani alimpenda mkewe.Alikuwa miongoni mwa watu waliojua kutia moyo.Tumezoea kumuona Kilua kama mwanamke msaliti wa ndoa yake lakini hatujamuona na mumewe wapoje upande wa pili.Walikuwa ndege njiwa wawili sare kama tu mwanamke huyu angeibeba kauli ya kuwa muaminifu kwa mumewe ila mambo aliyabananga muda mrefu.
“Shani anapitia mambo magumu natumai Mungu atamlinda kwa hili.Our daughter may never be the same again.:”sauti Ililowa kukata tamaa nakuhisi mambo magumu.Kupitia kipindi kile kilikuwa kigumu sana kwenye ndoa yao kiasi walihisi ugumu huo ni kama pigo fulani.Sahani ya urais ilikuja ni mtihani mgumu sana walikosa amani kwa namna fulani kuhusu mwana wa uzao wao.Kuna wakati ajihisi uanaume wake unapitia mgogoro kama kweli yeye ni mwanaume aliye mfaa Kilua au alikuwa hamtoshelezi vilivyo.Lakini bado Dedani alkuwa kichwa cha familia.Alikumbuka jinsi alivyoelezwa kwamba hata baada ya kutekwa bado mkewe alikutwa na mahusiano na hasimu wake namba moja yote ilionesha kidudu mtu katika ndoa yao alikuwa ni Serambovu mwenyewe.Nii kweli Kilua alikuwa na heshma kwake au ni maigizo tu.Kikawaida kama alimfumania basi alitegemea Kilua angeachana na Serambovu lakini tofauti ni kuwa sasa Serambovu yupo karibu sana na Kilua na tena ni chifu wa stafu nzima wa ikulu.Ni mtu muhimu sana kiserikali ni nafasi iliyomoja kwa moja na ushauri mkuu wa rais.Kumuondoa halikuwa jambo la mzaha!
“Dedani wangu promise me one thing?”alisema Kilua akihema alimuhitaji mume wake kwa sana .Alihitaji familia yake kuliko kitu chochote kile.
“Unahitaji nini?”
“Ukweli wako.”alisema Kiluwa kwa sauti yenye hamasa na ushawishi wa kike kabisa.Dedani kwa wakati ule alitamani mzibue makofi lakini alimeza ghadhabu moyoni mwake.Hivi huyu anataka ukweli gani kutoka kwake.
“Ukweli upi?”aliuliza Dedani kama vile hajui.Lakini alijua bila shaka mwanamke huyu anamgeuzia gia angani.Anabadili lengo na halisi ya taizo katika ndoa yao.Tatizo la ndoa yao ni usaliti ambao Kilua mwenyewe aliubariki.
“Unanipenda?”
Lilikuwa swali jepesi ila mazingira na hali halisi likawa gumu kama mwamba kulipatia jibu muaafaka.
DEdani alikuwa mzito huku kichwa kikiwa na maumivu makali sana ni vile aliheshimu madaraka ya mkewe pamoja na kiti chake.Anajua fika Serambovu amekuwa akila hii kitu na sasa amepoteza sifa za kumthamini mwanamke huyu tena.
“Nimekuuuliza swali nahitaji majibu.”
“Wewe mwenyewe unajua majibu ambayo ningekupa.Sioni umuhimu wa kukupa jibu unalolijua.”
“Then make love to me right now?”alijiamini kwa kauli ile.Kukiwa na msongo na mkazo wa mawazo Dedani angetamani kuwa kifuani kwa mmkewe wakijiliwaza pengine mkazo ungepungua na vile salama ya binti yao ipo sehemu mbaya.Dedani alihisi mwili wote kumsisimka ni muda tangu mkewe aoneshe kuwa na hamu nay eye kiasi cha kujielezea hisia zake mbele.Ilikuwa Dedani ndo mbembelezaji wa penzi la Kilua.Alihis anafakamia makombo yalioachwa na Serambovu.
“Mbona hunijibu.Make love to me now make me your woman just for this moment.Pengine itapunguza msongo wa mawazo hasa kwa sasa mwanetu katekwa.”ilikuwa sauti mkewe ambayo hakuitegemea kabisa kama ipo siku angetoa kauli kama ile kwa nyakati na hali kama zile.DEdani aliona mkewe amechanganyikiwa alijiuliza kama kweli Kilua anakumbuka mara ya mwisho alimkuta mazingira gani.
Bado hawakutatua mzozo wao halafu leo huyu mwanamke anategemea amwingilie kirahisirahisi.Dedani allipinga jambo ilo.
“Am sorry but najihisi mchovu sana sidhani kama nitaweza kushiriki.i have been through a lot.”alisema Dedani.Kauli yake ilimuumiza sana rais |Kilua japo ni mumewe na haki nae lakini hakutegemea kama angetamka vile.
“Kuna jambo baba naomba unieleze lakini usininyime haki yangu.”alisema Kilua kwa kudeka huku akijaribu kuiranda roho ya mumewe kwa mabusu ya shingo akilisaka penzi lake.
Dedani alimuwaza Shunie aliyemjia kichwani kwa ghafla palepale hakuhisi kufanya chochote na mkewe.aliona kufanya vile ni kuisaliti nafsi yake iliyoanza kupotea.Alikumbuka walivyofanya mapenzi mazito hisia zilikuwa kasi sana alipomfikiria hamu ilimshuka mauongoni na akatamani kumuona kwa wakati ule.Akili ya mtu ikifunuliwa unawezaa ona mambo ya ajabu ni vile zimehifadhiwa kwenye taswira ya ndani.
Dedani alijikuta akimgeukia mkeewe na kwa kasi ya ajabu alimwinua nakuanza kumbusu kwa nguvu kitu ambacho Kilua aliunga mkono huku machozi yakimtoka asijue ni ya furha au huzuni au alijutia nafsi yake kwa lengo lake la kumshikisha DEdani mimba ya mtu mwingine.KWa mara ya kwanza mtu na mkewe walikuwa katika fujo ya kukutana kimwili baada ya muda mrefu wa usaliti na upweke wa kukosaana kwa kutekwa.Dedani alifanya vile kuondoa mawazo ya kiumbe aitwae Shunie huku Kilua akiona ni nafasi nzuri kumshikisha mtu mimba.Ghafla mlango ukafunguliwa akaingia SErambovu bila hodi!
HERI YA MWAKA MPYA 2018 ASANTENI KWA KUFUATILIA MAPUNGUFU YA UCHELEWESHAJI TUSAMEHEANE.KOMBORA KIOTANI SAFARI BADO NI NDEFU NAWASIHI WAPENZI WA RIWAYA HII TUWE PAMOJA