KOMBORA KIOTANI-31

KOMBORA KIOTANI-31

FANANI MTENZI

Senior Member
Joined
Jul 4, 2017
Posts
106
Reaction score
95
KOMBORA KIOTANI-31

BONIFACE BIRAGE

Wengi walikuwa na shauku ya jinsi kipindi kingeenda kwa siku ile na jinsi kingepokewa na umma.Kulikuwa na stori kubwa iliyongoja kuruka hewani.Kilikuwa kipindi maalum kwa siku ile yenye mengi ya kushangaza na kushtusha.Pigo kwa rais Kilua kama mambo yangeenda kama kipindi kinnavyotakiwa kuruka hewani siku zote.Dedani alibeba uhusika wa aina yake kwa siku ile na jinsi tukio litakavyokuwa.Hakuwa tu analipa kisasi bali pia likuwa anaweka familia yake kwenye sura mpya yenye wingi wa sintofahamu.



Kamera zilikuwa tayari kuruka hewani.Na kama ilivyoada kwenye utawaala wowote ule lazima rais awe na mashushushu wake waliotapaakaa kila pembe ya ardhi ya Kiota.Ujio wa ghafla wa mume wa rais Kilua katika studio za televisheni ya pamekucha.Ndani ya muda mchache aliokuwepo bwana Dedani tayari habari zilianza kusambazwa kama moto wa nyika katika viungaa vya upashaji habari nyeti wa rais kuwa mumewe kaonekana.Wapambe wa Masha walikuwa kazini kuhakikisha sura ya Dedani popote itakapoonekana ilindwe.

Kipindi kilikuwa tayari kuruka .Mtangazaji maarufu wa kipindi kile alikuwa shauku ya kuhakikisha kwamba habari ile inapata kipaumbele.Kwa mara ya kwanza tanguu rais Kilua kuingia madarakani familia yake inapata ipaumbeele kuonekana mbele ya umma.illikuwa nafasi nzuri kwa mtangazaji Lora kutoa kipindi kile adimu mahojiano rasmi na mume wa rais Kilua ambayo yangekuwa tunu kkubwa kwake kuwahi kufanya.

Shunie akiwa kwenye gari alichapuka kwa harakaa nakumrushia teke mlinzi aliyepembeni yake.Alimpiga kwa kishindo nakufanikiwa kumkwida nakuifyetua shingo hali iliyopelekea mlinzi huyo kupoteza fahamu na asijue kinachoendelea.Shunie kwa haraka ya ajabu alifanikiwa kudhibiti vibaraka wengine waliokuwa kwenye gari.Hatua ya kuwashambulia ilikuwa hatari sana kwani ilionesha ukaidi wa hali ya juu.Ni kwamba alikuwa anaruka viunzi vya zee Kavuu na kuwa huru.Hatua hiyo bila shaka ingeleta hatari kwa usalama wwa Shani ambaye alitegemea nidhamu yao la sivyo mambo yangekuwa ndivyo sivyo.Kama Shunie kafikia hatua hiyo basi hatari ipo waziwazi kuwa msalia mtume haupo tena na maisha ya mtoto Shani hayatakuwa na salama tena kwani tayari makubaliano yameingia kombo na kuhatarisha kabisa usalama wake.

Shunie alitoka nje moja kwa moja nakuelekea kwenye ofisi za kituo kile cha habari kwa lengo la kuzuia isije ikatokea mahojiano yale kupanda hewani.Ghafla ile ya kuingia kwake ilikuwa kwenye hatari sana.Alipita kama mtu wa kawaida anayeingia kwenye jengo hilo ila akiwa na ajenda zake za isiri tayri kwa lolote ambalo lingejitokeza.Alienda hadi zilipo ofisi husika huku akitafuta chumba cha kurushia matangazo maalum kwa aajili ya kutekeleza Shambulio lile.Akiwa anakatiza kwenye korido alimuona mlinzi akiwa katika sare zake nadhifu pamoja na mtutu wa bunduki akiwa ameubeba.Pale akili ya Shunie ilifanya kazi kwa haraka kwamba amnyang’anye mlinzi bunduki ile kisha yeye aitumie kufyatua risasi kuleta taharuki na watu wote kwenye jengo lile wakimbie lakini pia njia hiyo bado ingeonesha juhudi zake za kutuma ujumbe kwa zee Kavu kuwa ni mkono wa Shunie wenye jeuri hiyo.Pia kungeweza kuleta vyombo vya ulinzi na usalama jambo ambalo lingerahisisha kwa Dedani pamoja na yeye kupatikana kwa urahisi.Lakini pia aliwaza njia nyingine ikiwa ni kufinya kengele ya moto kuashiria kuna hatari ya moto ili watu wawe na taharuki na yeye kufanikiwa kusitisha mahojiano kati ya Dedani na watangazaji wa kipindi kile.Lengo kuzuia kuchafuliwa kwa rais Kilua kwa wakati ule.Njia zote zilikuwa kinzani kwa namna moja au nyingine na zote zilikuwa na tija hasi na chanya kwamba Dedani angefanikiwa kutoka mikononi mwa watu hao.Lakin hakusahau kwamba atakuwa amemuweka mashakani mto to Shani.Ilitakiwa awe na uamuzi wa haraka la sivyo mambo wangezidi kuyabananga.

Ktika purukushani alijikuta akimuwahi bwana mlinzi kiisha kumkwida kwa haraka akamnyang’anya silaha yake.Matukio yote yalikuwa kama bahati nasibu ya tatu mzuka au biko tangu afanikiwe kutoka garini hadi kuingia humu ndani.Alifyetua risasi juu kwa kishindo.Timbwili la mlio lilirindima kwa fujo nakuzizima zima.Akarudia tena kufyetua risasi kama nje.Tayari uhatari uliozua taharuki ulisikika pembe zote za jingo lile.Watu walibaini ulikuwa mlio wa risasi hata waliokuwa studio ambapo tayari walianza mazungumzo kwa njia ya kumkaribisha bwana Dedani huku akielewa yupo mubashara na umma mkubwa ulikuwa unamuangalia.

“Karibu sana bwana Dedani.’’alianza mtangazaji.

‘’Nashukuru kwa ukaribisho.’’alijitahidi bwana Dedani kuonesha tabsamu lake hafifu akijua sasa mambo yameiva kwa kiasi kikubwa.

“Wewe ndo mume halisi wa…”kabla hajahitimisha sentensi yake muhimu ulisikika mlio wa risasi Paa!Paa!Paa!Mliio huo ulimuogopesha hadi Dedani mwenyewe akajikuta akitetemeka.Waliokuwa wameshika kamera ilibidi waziachie chini nakipindi kuondolewa hewani kwa haraka sana.Palepale mlango wa chumba kile ulifunguliwaa kwa ghafla na Shunie kuvamia.Akiwa kashika mtutu wa bunduki.Wote waliomuona walijikuta wakitaharuki na nywele kuwasisimka kwa fujo ya asubuhi ile.Katokea binti nadhifu mrembo kama yai mwenye mtutu wa bunduki kaingia kwenye chumba cha kurushia matangazo!

Shunie alimfuata Dedani nakumnyooshea bastola kasha akamuamuru ainuke.

‘’Inuka mikono juu.’’alitamka akijiamini huku usso wake ukibeba umakini wa hali ya juuu.Dedani alitii nakuinuka wote wakatoka kwa pamoja katika chumba kile huku Shunie akiwa anaonekana amemweka Dedani chini ya ulinzi waandishi kadhaa wa vyombo vya habari walikuwa wakichukua picha ya tukio lile kwa simu zao wengine wakipiga picha na wengine wakirekodi video kabisa maalum kwa kusambaza habari ile.Shunie akaonekana akimshikia bastola mume wa rais Kilua katika jingo la kituo cha habari cha pambazuko tv.Taswira ya Shunie ikaingia kwenye mtirirko mwingine wa sintofahamu iweje iwe vile?Hata dakika hazikupita kabla hajafika nje ya jengo lile tayari wengine walianza kusambaza rekodi ndogo za video kwenye mitandao ya kijamii.Taarifa ikisema mume wa rais Kilua ashikiwa bastola akiwa katika chumba cha mahojiano.

Mashushushu wa Kiota waliona taarifa ile nakuanza kuwasiliana na wenzao waliokaribu na jingo lile na kweli kwa waliopata taarifa ile hawakuchelewa ndani ya dakika zilezile walianza mara moja kukagua jengo lile.Wamo mashushushu waliokuwa kama wafanyakazi nao pia walianza kufuatilia kutaka kumjua aliyemshikia Dedani bastola.Shunie alionekana kama adui ndani ya mfupi na kwamba hatua zozote zitakazopelekea yeye kukamatwa asingeonekana kama vile shujaa bali adui wa taifa.

Hatari ilikuwa imepelea hali kuwa tete na ndani ya muda usio na kipimo vyombo vya usalama vikaanza kazi.Shunie alitoka hadi nje na Dedani nakuelekea yalipo maegesho ya magari pamoja nakuwa katika taharuki ile lakini bado aliweza kujidhibiti yeye kama yeye asiweke mashaka yoyote yale kwa Dedani.Zile purukushani zilifanya baadhi ya watu kuwa bize kukimbilia ponya yao.Shunie alishusha bastola chini ikawa haina ulazimu tena wa yeye kumtishia bwana Dedani.Hakumtishia kwamba anamuweka chini ya ulinzi bali alifanya vile kumuondoa pale kwenye chumba cha mahojiano.

Nje hakujua aende wapi.Gari waliloletwa nalo aliona likiwa palepale alipoliacha.Aliona wale vijana aliowadhibiti kabla haajavamiwa wakiwa wameerejewa na fahamu huku wakishangazwa jinsi mambo yalivyokuwa Shunie alitambua fika sasa upepo nao unabidili mwelekeo na siajabu zee Kavu akichukua hatua kali kwa tukio la yeye kumkwapua Dedani.Aliona mwanya ule autumie vyema ilikumtorosha Dedani.

“Shunie tunaenda wapi?’’aliuliza Dedani akitweta.

“Nakutorosha hatuwezi kurudi kwa yule afriti!’’

“Hatma ya mwanangu itakuwaje ikiiwa Kavu hataniona?Huoni kuwa umeniletea matatizo makubwa sana dhidi ya jambo hili?Kurudi kwangu kwake ndo pona ya Shani wangu.’’

‘’Turudi iliazidi kushinda?Niliapa kuirejesha familia ya rais Kilua na sasa nimefanikiwa kumpata mmoja ya mateka wawili na wewe ndo mmoja wao.”alitamka Shunie akizidi kujikaza.Dedani alimuwaza mwanaye kwa sana alimfikiria sana lakini pia alimpenda mkewe hakupaswa kutoa shutuma zile mbele ya umma kulinda heshma ya kiti cha urais alichopewa na mkewe.

“Sikiliza DEDANI nimeshughulika na waovu kama hawa najua hawana mipaka hata ukirudi bado tu mwanao ataendelea kuteswa.Huwezi msaidia mwanao ukiwa mateka.Hicho ni kitu ambacho hakiwezekani.Najua bwana Kavu atataka akupate tena lakini wewe usimpe nafasi yeyote yakuweza kukudhibiti.Akikutaka na atataka urejee kwake bila shaka hapo tutaweza kukufanya chambo cha kumtia mbaroni.Lakini inabidi tucheze karata zake kwa minajili yakujiokoa kwa jambo hili la sivyo atatumaliza.Naomba niamini sifanyi haya kwa kuhatarisha maisha ya Shani bali nafasi kwa sisi kuweza kupata nguvu tukiwa kwenye ngome zetu.Yeye ni mbabe akiwa ametuweka kwenye himaya yake na sisi lazima tuwe wababe tukiwa kwenye ngome zetu anachotaka kutumia ni udhaifu wa kumteka mwanao na sisi tutumie udhaifu kama ubabe kwetu.’’

Dedani alibaki kumshangaa huyu binti.

Shunie alienda hadi kwenye lile gari nakumuweka moja ya vijana wale chini ya ulinzi kisha alimnyang’anya simu nakumpigia mkuu wa idara ya usalama wa taifa bwana Toti.Namba maalum kwa wafanyakazi wa idara hiyo alizitumia kumpigia bwana Toti nakumueleza alipo.Ndani ya dakika kumi wakiwa wamejificha lilikuja gari la idara hiyo huku llikifuatiwa na mengine kama manne yakiwa na wanausalama wao walijikoki kisilaha wakafanikiwa kumchukua Shunie na Dedani pamoja nakuwaweka vijana wa mzee Kavu chini ya ulinzi.

Gari nyeusi zilitifua vumbi zikiingia eneo lile kwa kasi.Walishuka wanausalama na mara moja wakaweka mzingo wa usalama kwa Dedani.Toti mwenyewe alikuwepo kwenye operesheni ile akimkumbatia Shunie kwa ujasiri aliouonesha kumuokoa mume wa rais Kilua.Watu wawili muhimu walikuwa matekani lakini sasa mmoja kafanikiwa kupatikana.Lilikuwa jambo lenye kutia moyo na hata kuonesha imani kwamba mtoto Shani angepatikana tena.

“Shunie nakupa pole kwa uliyopitia.”alitamka bwana Toti akifarjika kwa kazi aliyoitekeleza Shunie.

“Nahitaji kumuona rais kwanzaa.” alisema Shunie akimtizama kwa makini bosi wake huyo.

“Hata yeye anahitaji kukuona mara moja.”alisema bwana Toti wakiingia kwenye gari huku Dedani akisisitiza hataki kuwa mbali na Shunie.Toti alipanda nao gari kuelekea ikulu.Kwa haraka ya ajabu magari yalikuwa yakisugua lami.Safari ya ikulu.Taarifa ya kumshutumu rais Kilua ilikuwa imefeli na sasa taarifa ni kwa mume wa rais KiLUA Kuonekana kwenye ofisi za pambazuko tv kisha kutekwa na mwanamke na baada ya hapo anaonekana akienda ikulu.Kila alitoa tafsiri yake!
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 53
Back
Top Bottom