Kombe La Dunia Ndani Ya Ardhi Ya Zanzibar. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kombe La Dunia Ndani Ya Ardhi Ya Zanzibar.

Discussion in 'Sports' started by Junius, Oct 23, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wameomba kupatiwa fursa ya kulikamata kwa mikono na kulibusu kombe la dunia linalotarajiwa kuingia nchini mwezi wa Novemba mwaka huu.
  Ombi hilo limetolewa muda mfupi na wajumbe hao baada ya Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Zanzibar, Ali Juma Shamhuna kumaliza kuwasilisha ripoti ya serikali juu ya ujio wa kombo hilo nchini katika kikao cha baraza la wawakilishi kinachoendelea Maisra Mjini Unguja.
  Wajumbe hao wakiwemo mawaziri wa serikali waliomba wapatiwe nafasi japo kidogo kwa ajili ya kulishika kwa mikono yao na kulibusu kombo la dunia wakati litakapowasilia visiwani hapa katika uwanja wa ndege wa Zanzibar.
  Hata hivyo Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema mtu pekee atakayeruhusika kulishika kombo la dunia linalotarajiwa kuletwa nchini Novemba 22 mwaka huu ni Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.
  Akijibu ombi hilo Waziri Shamhuna alisema ingawa wajumbe hao wana hamu kubwa ya kulishika kombo hilo na kutaka angalau wapewe nafasi ndogo ya kulikamata na lakini kutokana na hali ya kiprotokoli anayepaswa kulishika ni rais wan chi pekee na sio mtu mwengine yoyote.
  “Ni kweli najua kuwa mna hamu sana na kutaka kulishika na kulibusu hilo kombo litakapokuja hapa kwetu lakini mheshimiwa rais peke yake ndiye atakayepata nafasi ya kuligusa na limekuja nchini kwa sababu ya kuwa hapa kwetu kuna rais” waliambiwa wajumbe hao ambao walikuwa na hamu yakupata majibu kutoka kwa waziri huyo.
  Shamhuna alisema mbali ya kuwa Rais atapata fursa ya kulishika watu wnegine watakaopewa nafasi ya kulipna kombe hilo ni vijana walioshiriki mchezo wa copa coca cola na wapenzi wengine wa michezo amabo wao kwa pamoja wakiwepo wajumbe wa baraza la wawakilishi na viongozi wa serikali wakiwemo mawaziri watapata fursa ya kuliona kwa macho tu na sio kuligusa.
  Akiwasilisha maoni ya kambi ya upinzani kuhusiana na ujio wa kombo hilo Waziri Kivuli wa Habari, Utamaduni na Michezo, Najma Khalfan Juma alisema “Nakubaliana na Mheshimiwa Waziri kuwa tukio hili ni muhimu na heshima kwa Zanzibar na kila mmoja wetu ni vyema akalifurahia na kuliuunga mkono hasa kwa vile Fainali za Kombe hilo 2010 zitafanyika ndani ya ardhi yetu ya Afrika, huko Afrika Kusini” alisema Najma huku akishangiriwa.
  Alisema ujio wa kombo hilo visiwani hapa ni ishara ya kuwa Zanzibar kwa kiasi inakubalika katika taasisi za kimataifa za michezo, kwa kuwa ujio wa Kombe hili haukufanikiwa tu kwa sababu ya hisani bali kwa kuona kuwa Zanzibar ina nafasi muhimu katika Tanzania, nchi ambayo pia ni ya pekee Afrika nzima ambapo Kombe hili litakaa kwa muda mrefu.
  “Hapo kabla Zanzibar ilisononeka pale Mwenge wa Olimpiki ambao ulifika Dar es salaam ikiwa ni mji pekee Afrika nzima kufika na kutembezwa, haukuweza kuvuka bahari na kuja Zanzibar na moja ya hoja iliyotolewa wakati huo ni ufupi wa muda lakini wako pia waliosema kuwa kuipa Zanzibar nafasi ni kudhulumu mikoa mengine ya Tanzania” alisema Waziri Kivuli huyo.
  Aliwaambia wajumbe wa baraza hilo kwamba “Itakumbukwa pia huko nyuma heshima inayofanana na ujio wa Kombe la Dunia ilikuwa ni ile ya Mwenge wa Michezo ya Jumuia ya Madola na furaha ya kupokea na kuutembeza mwenge huo sote tunaikumbuka. Mheshimiwa Spika, niruhusu niseme kuwa kuja kwa Kombe la Dunia ni taswira ambayo lazima itiwe katika mtizamo maalum ili kulipa jambo hilo stahiki yake, na sisi tunaotembelewa na kombe hilo tupate nafasi ya kujiuliza masuala mengi, na sio kutizama tukio hili kwa macho ya kisiasa” alisema Najma.
  alisema mpira wa miguu ndio mchezo maarufu na mkubwa kabisa duniani na hata hapa ndio mchezo unapata umuhimu lakini mchezo huo una ushawishi mkubwa miongoni mwa vijana na kama unatumiwa vyema unaweza kujenga mapenzi ya wananchi kwa nchi yao.
  “Sote tunajivuna kuwa Fainali za Kombe la Dunia zinafanyikia Afrika kwa sababu tunataka kujikurubisha na mafanikio ya kutambuliwa Afrika kupewa heshima hio kwa mara ya kwanza ingawa tungependa nchi yetu ingekuwa dimbani lakini hatukuweza kupata bahati hiyo na kwa hivyo tutakuwa watazamaji tu” alieleza Najma ambae ni Mwakilishi wa nafasi za wanawake (CUF).
  Alisema kwamba kuhusiana na ujio wa Kombe hilo hapa nchini utakuwa na maana sana iwapo Wazanzibari watapata fursa mbili ikiwemo kwenda kuona michuano hiyo huko Bondeni kwa mwenye uwezo au kuweza kuona mechi hizo kupitia kwenye televisheni.
  “Mheshimiwa Spika nimeona niliseme hili na mapema kwa sababu ya khofu kuwa inaweza ikatokea kukakosekana mipango ya uhakika ya michuano hiyo kuonekana na wananchi kama ambavyo tumeshawahi kukosa kuona michuano mengine mikubwa. Najua kuwa kuna suala la kununua haki za kutangaza, lakini hili litafutiwe ufumbuzi mapema na sio kuongojea zima moto” Alisema Mwakilishi huyo.
  Alisema iwapo michuano hiyo itaonyeshwa basi wengi wanaamini itasaidia kuraghibisha mchezo wa soka hapa Zanzibar ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa kiwango chake kimeshuka na hilo limekuwa likisemwa na Kocha Marcio Maximo na kushikilia kuwa hiyo ndio sababu ya kutochagua wachezaji wa Zanzibar kujiunga na timu ya Tanzania, Taifa Stars.
  “Hivi sasa soka ya Zanzibar imepata mwamko mpya kwa matukio yaliojiri hivi karibuni ikiwa ni pamoja na ujio wa kocha mpya wa Kimasri, kupata nafasi mchezaji wa Kizanzibari kwenda chuo cha soka huko Ureno na tukio la karibuni la zoezi la kuchagua vipaji lilofanywa na Oranje Academy la kuchagua vipaji ambavyo vitaendelezwa ili kulenga kupata wachezaji wa kulipwa. Pia, tukio la Zanzibar kujiunga na shirikisho la nchi ziso wanachama wa FIFA, yaani International Footbal Union, ni hatua yenye muelekeo mzuri” alisema Waziri Kivuli huyo.
  Kombe la Dunia litakuwa na maana iwapo kutakuwa na dhamiri ya kutaka kubadilisha na kuchukulia kuja kwake kombe hilo kuwa ni changamoto ya mabadiliko ambapo mchezo wa soka una nguvu ya kuunganisha watu, tungependa ujio wa Kombe la Dunia iwe ni chachu ya kutuunganisha maana kama litakuja na kuondoka na watu wakawa hawajiga hatua katika eneo hilo basi itakuwa na maana ndogo sana ya kuja kwake.
  “Tunapenda kupongeza wazo la Kombe hilo kupokelewa au kufikishwa katika Bustani ya Forodhani. Pale ndio uso wa Zanzibar mbali ya kuwa ni ndani ya mji wenye hadhi ya Urithi wa Dunia. Sisi tunawaomba wananchi wote walipokee Kombe hilo kwa moyo mkunjufu maana ugeni huo ni wetu sote” alisisitiza Mwakilishi huyo.

  SOURCE: ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Haijambo wametukumbuka...hatua ya kwanza hiyo.
   
 3. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #3
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Wanaendekeza childish infantuation badala ya kufanya kazi za maana.

  Hamna kuwapa kombe walibusu mpaka wananchi wapate maji kwanza.
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  He he he he!
  Mkuu hii ni michezo tu watu wakati mwengine wafurahi bwana...weshazuga watu vya kutosha iliyobaki saivi kuchekacheka tu.
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo wewe una support wazuge watu halafu wachekecheke tu?
   
 6. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #6
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Absolutely NO.
  Let them register their shame before the bored-tired wananchi.
  they are filius nullius in charaters.
   
 7. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #7
  Oct 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sasa kwa nini na wewe unachekelea kuchekacheka kwao?

  Are you one of them or one of the bored-tired wananchi?
   
 8. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  The letter...
   
Loading...