Komandoo Salmin: Nini kilichojiri akaanguka 2000? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Komandoo Salmin: Nini kilichojiri akaanguka 2000?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, May 27, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Naomba kuuliza, ni kipi kilimsibu Salmin na kampeni yake ya kuongezewa muda kugombea Urais?

  Maana naona yeye ni kiongozi wa pili kutoka Zanzibar ambaye aliishia "kudhibiiwa" na CCM!
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  May 27, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Inasemekena alikuwa anafuata nyayo za kina Seif Shari Hamadi, na mzee Alhaji Abdu Jumbe... Ni yale yale muendelezo wa Serikali tatu. Lakini kwa bahati mbaya alichelewa sana.
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,312
  Likes Received: 5,600
  Trophy Points: 280
  Sasa anataabika na ugonjwa wake wa macho...Jk amemuokoa sana....kumlipia kila kitu....kukaa china miezi 3 hivi
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Alicheza vibaya karata yake, na alichelewa mno kuwakilisha hoja yake na mbaya zaidi alikuwa tayali ameshajenga uadui na upande mwingine wa CCM ambao wana sauti sana katika hatima ya uongozi visiwani humo.
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  - Political miscalculations, yeye alikuwa ana bank on Mkapa, kwmaba kwa sababu alimsaidia Mwalimu, kumpa urais Mkapa over Kikwete basi Mkapa hana ubavu wa kumzuia kuwa rais tena wa term tatu,

  - Wafadhili wasingekubali huu ujuha, CCM siku zote wako careful kuwa on line na wafadhili, ndio maana siku ya kumfundisha adabu Salmin kule CC Dodoma, Salmin aliitwa mbele ya kikao na CC wakamuomba Mkapa atoke nje, ili wamshughulikie wenyewe, na kwa hasira ya wajumbe wengi dhidi ya Salmin, wakamwambia wazi kwamba hata mgombea wake Bilali wanamtwanga na kumpa Karume, aliyeshindwa naye!

  Respect.

  FMES!
   
 6. dmaujanja1

  dmaujanja1 JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2009
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu FMES hayo macho ndiyo wajumbe walimtenda huko Dodoma?
   
 7. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2009
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  kosa lake ni kutaka kuitoa zanzibar katika makucha ya mkoloni tanganyika
   
 8. M

  Masatu JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ubeba ulichopa mipaka, kauli yake zake kuwa "hakuna baba wa taifa wala babu wa taifa" ( Nyerere akiwa hai ) ziliwatia mashaka watu kuwa jamaa akibadili katiba na kuendelea huko mbele hata huo muungano utakuwa matatani.

  Mkong'oto aliwapa CUF ikiwa pamoja na kuwasweka ndani takriban miaka 3 viongozi waandamizi wa CUF akiwemo mpwae, mtoto wa dada yake Juma Duni kwa kile kilichoitwa 'uhaini". Ilifika wakati hata dada yake ( mama wa Duni ) alimuomba amwachie akasema muache akae ndani kwa "sio nyanya zile labda zitaoza!".

  Nguvu kubwa ya wana mtandao ( Bara ) JK, RA, EL, Membe et al ilisimamisha jaribio la NEC- ZNZ kubadili katiba. Ikumbukwe NEC - ZNZ ilisha ridhia mabadiliko ya katiba.

  Wana mtandao (ZnZ ) akiwemo Karume, Seif Khatib, et al kusimama kidete kupinga jaribio la kubadili katika.

  Ujinga wa Salmin kutojua SMZ inaongozwa na serikali ya Muungano.
   
 9. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mh!! Kweli hayo?
   
 10. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Nyie vijana wa Othman hamkuja JF kuihujumu serikali yetu. Fanya kazi iliyowaleta humu.
  Naapa nitawasema.
   
 11. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2009
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 340
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hawa viongozi wa zbar huwa wanajisahau mpaka maslahi yao yanapokwisha ndio huanza kukurupuka!
   
 12. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Komandoo alikuwa ni miongoni mwa ile "kama huru" akijifichaficha siku hizo, Marehem Mzee I.A.Wakil alishambonyeza "asifanye papara" akajamuudhi Nyerere, naye komandoo alifuata ushauri wa wakubwa na kuisaliti "kama huru". Hata hivyo bado alikuwa both "mpenda nchi" na "tumbo lake". Madaraka matamu lakini yana mwisho, mwaka 1995 alibwagwa katika uchaguzi mkuu wa vyama vingi na Maalim Seif, komandoo , kama Mzee Mugabe, alishakubali matokeo, lakini unajua tena wapambe nuksi, amri ikatoka kule machinjioni (dodoma), katika kile kilichoitwa kwa siri "do any thing to save the union from anemies", matokeo yakabadilishwa, jaji Zuberi (mw'kiti wa tume ya uchaguzi wakati ule, saivi anaokota makopo) akamtangaza komandoo kuwa rahisi, kinyume na matakwa ya wachaguzi bali ya wateuzi (dola au SMT).
  Bid yake ya kuongeza muda ilishindikina kwa "kiburi" chake tu kwa waliomteuwa kuwa rais 1995 (yaani bara au smt) kwani kama wangetaka sheria ingebadilishwa na asingetokea nyoko yeyote kupinga, mbona sheria ya kupunguza majimbo ya uchaguzi Pemba ili kupunguza nguvu ya upinzani bungeni na BLW ilipitishwa licha ya kupingwa vikali na wadau mbalimbali visiwani? mbona walipotaka Amani Karume apite bila kupingwa kugombea kwa awamu ya pili walifanikiwa licha ya kuwa Dr. Bilal alikuwa na nafasi kubwa ya kumbwaga kule machinjioni (dodoma)?
  Lakini all ini all,licha ya mapungufu yake mengi makubwa na madogo,komandoo atabaki kuwa rais pekee wa Zanzibar aliekuwa "maarufu" kwa watu wa kawaida na masikini wa Zanzibar, watakumbuka enzi zile huhitaji kusubiri mshahara wa tarehe 35 au 36 ili usavaivu libeneke kali la maisha. Pesa ilikuwapo nje nje, jamaa alikuwa anajua kula na vipofu, biashara zanzibar ilinoga mpaka "makalikiti" kutoka "mrima" walikuwa wakifurika visiwani kuja ku spend.
  Mikakati yake ya kuirejesha zanzibar kuwa "himaya ya kibiashara" katika mwambao wa Afrika Mashariki, ilifuatiwa na vision ambayo pengine ingekuwa kweli kama si kauzibe za Muungano.
   
 13. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  I do like the way u spin Junius. Lakini kwa nini hutaki kueleza ukweli jinsi gani CUF waliiba kura katika uchaguzi huo wa kina Salmin. Kina Salmin walitonywa njama na mikakati ya CUF ya kuuiba kura (na intelligence) wakapuuza wakizubaishwa na vigelele vya katika kiriri. Matokeo yake ni uchafuzi katika uchaguzi ule, but on part of CUF na siyo kina Salmin ambao walikuwa na matumaini. Junius kuwa na courage ya kueleza ukweli.
   
 14. J

  JokaKuu Platinum Member

  #14
  May 27, 2009
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  Junius,Pakacha,

  ..waliomshughulikia Komandoo na Dr.Bilali Dodoma ni wanamtandao.

  ..Komandoo alisaidia kushawishi wajumbe wa ZNZ kumpa kura Mkapa na kumkosesha Uraisi JK mwaka 95 ktk mkutano mkuu wa CCM.
   
 15. P

  Pakacha JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2009
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 816
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Na wanamtandao wasingeweza kupenya , bila ya nguvu ya marehemu Diria (Mungu Amlaze mahala pema). Ambaye aliwabeba "Wanamtandao" na kuwapenyeza huko Zenj kwa kutumia mgongo wa uwana-Mapinduzi.
   
 16. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu kwa anaejua:
  Kwa nini Kikwete aliposhinda 1995 uchaguzi ukarudiwa kwa madai kuwa hakufikisha zaidi ya 50% ya kura zilizopigwa.Huu utaratibu ulikuwepo/upo kwenye katiba ya CCM au ni zengwe tu la Nyerere&co?
   
 17. BUSARA6

  BUSARA6 JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2009
  Joined: Jan 8, 2007
  Messages: 340
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Wakaskazini zbar wana mambo!
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Sheria za CCM ni kuwa mtu kua mgombea wa CCM lazima ashinde kwa zaidi ya 50%(yani majority). Mgombea mmoja asipo pata hizo asilimia zinazo hitajika kuna kua na runoff kati ya wagombea wawili walio pata kura nyingi zaidi. Sasa JK hakupata more than 50% so kukawa kuna runoff(round ya pili) kati ya yeye na bwana Mkapa. Kwenye hiyo roundoff Mkapa akapata asilimia zinazo takiwa. Hicho ni kiashiria kwamba waliokua wana support wagombea wengine baada ya mbio kuwa kati ya JK na Mkapa waka hamia kwa Mkapa. Watu wengine wanavyo dai ni kwamba Nyerere & co wao walikua wanampigia debe Mkapa na kama unavyo jua Mzee wetu alikua very influential. Sidhani kama kulikua na foul play yoyote. Nyerere knew who he wanted & did everything within the party regulations to get his man. Kama kuna mwenye view tofauti sawa ata tueleza.
   
 19. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Pakacha,
  Hebu tuwe wakweli kidooooooooogo tu!
  Pindipo (nasisitiza tena, Pindipo) zanzibar ufanyike uchaguzi (angalau wa majaribio) halafu uchaguzi huo uwe huru na haki, ufanyike kihakkki lillahi. Vyama vyote visifanye haya maigizo wanayofanya saivi wakiyaita uchaguzi. Niagulie matokeo.
   
 20. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Na ile ya Bilali na Amani karume je?
   
Loading...