Nina Hisense soundbar, lakini kusema ukweli, nimejuta kuinunua. Bora ningechukua Sepeano yangu tu, ambayo nimeiacha mkoani. Mimi najua ninachokisema linapokuja suala la mziki. Sound clarity yenyewe si ya kuridhisha, bass nayo hakuna ile ladha unayoitarajia. Kwa kifupi, kwangu imekuwa disappointment kubwa. Ushauri wangu, usiingie mtego wa kununua Hisense soundbar au hivi visoundbar vingine vya kichina kwa kutegemea matangazo na muonekano wake. Bora utafute mfumo wa sauti unaotoa mziki wenye ladha halisi. Mimi nimejifunza kwa uzoefu, na kwa kweli najuta!