Kodi ya Uzalendo kwa Wabunge

Paf

JF-Expert Member
May 25, 2021
1,703
3,304
Tuna Wabunge 413 kwa taarifa za leo June 22/2021.

Ili kuondoa utata wa kodi ya uzalendo kwenye simu na LUKU napendekeza Kodi ya Uzalendo kwa Wabunge Tsh. 1,000,000 kila mwezi wakatwe.

Wananchi vyuma bado vimekaza
 
Hujamskia mbunge wa Mbogwe Geita akidai mapato yao kwa ujumla hayatoshi?

Na wabunge wanampigia makofi, ubinafsi ni ugonjwa kama magonjwa mengine.

Wataendelea kujipendelea na hawatatosheka kamwee.
 
Daaaaah!.ongezeni zaidi maana hakika namna.so mpo wenyewe kiharamu.ila mtakuja kuzitapika one day.

Kwa hiyo tukatwe kodi ili mnufaike ninyi wajinga wakubwa.
Ila na watanzania wengi wetu ni majuha wa karne.ukikataa basis Nijue ni hatua gani ulishajaribu kufanya.CCm ni kirusi cha corona ambacho watanzania tulikipata tangu enzi achana na hili cha HUANI CHINA
 
Tuna wabunge 413 kwa taarifa za leo June 22/2021.
Ili kuondoa utata wa kodi ya uzalendo kwenye simu na luku napendekeza kodi ya uzalendo kwa wabunge Tsh 1,000,000 kila mwezi wakatwe.
Wananchi vyuma bado vimekaza

Duu, kumbe hawa jamaa wanalamba hazina ya nchi bila huruma.
 
Eti huko hakuna kitu, wamejazana wanatafuta nini si waache waje kujiajiri
 
Sasa si kama anataka kulipwa kwa dola, si ahamie kwenye nchi wanazolipa kwa dola?
Hao wabunge ni wa kuwatupa tu uchaguzi ujao bila huruma, yaani mtu anakunja TS 200,000/= kwa kikao kimoja na sasa bunge la bajeti wanakaribia mwezi wa nne wako tu huko wanapiga domo kutaka kujiongezea posho. Mshahara TS 11,000,000/= kwa mwezi na mwisho wa mhula wa miaka mitano anapewa mkono wa kwaheri TZ 200,000,000/=

Ubinadamu ni kazi kubwa sana, hakuna hata mmoja hapo ambaye yuko tayari afe yeye ilimradi wananchi anaowawakilisha watatuliwe shida zao.
 
Uchaguzi uhai kwa katiba ipi?
 
Hujamskia mbunge wa Mbogwe Geita akidai mapato yao kwa ujumla hayatoshi?

Kama chama chake hawatatoa tamko kumkosoa huyu mbunge aliyeomba ubunge ili ajipatie pesa za kutosha kuwagawia wananchi wake kama anavyojinasibu wanamsubiri inaonesha hata kupita kura za maoni alihonga maana hajiamini kama hana pesa kama anaweza kushawishi na kuishi ya kutokuwa na ukwasi kuwazidi ili awapiganie kwa moyo wote.

HAFAI HUYU hata kidogo, ajiuzulu haraka na uchaguzi ufanyike kwa yule anayekubaliana na malipo ya ubunge kwa sasa.

Wananchi mtaani wanadai wabunge wanalipwa mishahara na posho kubwa mno kwa gharama za kodi za wananchi ambao kipato chao ni kidogo bado wanataka waongezewa? Wanasema HAPANA
 
Back
Top Bottom