Kodi ya mitandao ya kijamii kuanza kutozwa Uganda

Cowman

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
1,710
3,145
Raia wa Uganda wanaotumia mitandao ya kijamii nchini humo huenda wakalazimika kulipa ndipo waruhusiwe na serikali kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook na WhatsApp. Hii ni baada ya Bunge hilo kuidhinisha mswada huo tata Jumatano.
Chini ya sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kutekelezwa 1 Julai, wanaotumia mitandao ya kijamii watakuwa wanatozwa shilingi 200 za Uganda ambazo ni sawa na $0.05 ( £0.04) kila siku.
Raia pia watalipia kila shughuli ya kibiashara watakayoikamilisha kupitia simu zao, huku kila shughuli ya kibiashara ikitozwa 1% ya thamani yake.

Ni vyema kuweka picha za mwanao mtandaoni?
Rais Yoweri Museveni alikaririwa na vyombo vya habari nchini Uganda mwezi uliopita akisema kuwa mitandao ya kijamii inatumiwa zaidi kwa taarifa za "udaku". Wanaharakati wa haki za binadamu hawakubaliani na madai ya rais. "Ni sehemu tu ya majaribio ya kubana uhuru wa watu kujieleza ," Mwana Blogi Rosebell kagumile aliliambia shirika la habari la Reuters.
Takriban wabunge watatu wamekosoa sheria hizi mpya na kuzitaja kama "utozaji wa kodi mara dufu ", kulinga na gazeti binafsi Daily Monitor.
Mbunge wa jimbo Kyaddondo Mashariki Robert Kyaggulanyi, almaarufu Bobi Wine - pamoja na wenzake Joshua Anywarach na Silas Aogon - wamesema kwa sababu watumiaji wa mtandao wa WhatsApp hupata huduma hiyo kupitia muda salio ambalo wanalipia ushuru, ushuru wa ziada utakuwa unakiuka haki

Mbunge mwingine , Patrick Nsamba wa chama tawala , amesema kuwa ushuru huo utawaumiza maskini zaidi. Ni rahisi sana kwa mbunge kusema asilimia 1% ni kiasi kidogo cha lakini kwa watu wenye kipato cha chini ya dola moja kwa siku itawaumiza sana. Kuna mkanganyiko kuhusu namna ushuru huo mpya kwa mitandao ya kijamii utakavyotekelezwa.

Waganda wanatumia mitandao ya kijamii kusambaza kauli zao za kutoafikiana na ushuru huo mpya ambao umepitishwa kufuatia ombi la rais Yoweri Museveni.
Katika barua yake kwa waziri wa fedha, Bwn. Museveni alisisitiza kuwa ya kijamii inapaswa kulipa kodi kwasababu inachochea taarifa za udaku.
Lakini alidai kuwa huduma ya data za intaneti haipaswi kuwekewa ushuru, kwa sababu manufaa yake ya kielimu.
Wataalam pamoja na mtoaji mmoja wa huduma za Intaneti wameelezea hofu yao juu ya namna ushuru wa mitandao ya kijamii na mamilioni ya Waganda kwa kutumia sim-kadi
Serikali inahangai kuhakikisha simu kadi zote zinasajiliwa.

Chanzo: BBC Swahili.
 
Hivi ni kwanini viongozi wanaona social networks kama wapinzani kwao. Hizi ni zama za sayansi na teknolojia huwezi kuweka ugumu watu wasitumie mitandao ya kijamii, dunia imebadilika na kuwa kijiji kupitia hizo social networks sasa leo kila kiongozi hasa hawa wa Africa wanatumia kila mbinu ili tusiweze kutumia mitandao ya kijamii.
 
Afadhali na TZ tuige ili tuongeze vyanzo vipya vya mapato sio kila siku sigara na pombe tu!!
 
Mkuu kuna watu hii mitandao ndiyo ofisi zao, nimepost nauza TV laki 850,000 lazima nitoe 8,500 kama kodi. This is nonsense!
 
Back
Top Bottom