Kodi mpya ya majengo imekaaje kisheria?

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
23,547
2,000
Kuna kodi mpya ya majengo imeanzishwa kwa nyumba hata zile ambazo zimejengwa sehemu zisizopimwa.
Hii imekaaje kisheria, maana lazima tutii sheria bila shuruti. Kodi hii iko kisheria? Mpaka sasa bado sheria inataka nyumba zilizojengwa katika sehemu zilizopimwa ndio zilipe.

Naambatanisha barua ya wito wa kulipa toka TRA kwa sehemu ambazo hazijapimwa.

KODI YA MAJENGO-1.jpg
 
Attachments

NAKWEDE

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
28,013
2,000
Kwa wale ambao wamejenga sehemu ambazo hazijapimwa, kwanza inatakiwa kufika tarehe 30/6/2017 wawe tayari wamerasimishwa makazi yao. Sasa kuhusu kodi za majengo wanachaofanya (Kata ya Buswelu - Mwanza) unakwenda ofisi ya Mtendaji wa kata, wanajaza fomu ambayo kwenye hiyo fomu kuna sehemu ya kueleza nyumba yako ilivyo, ukimaliza unacha hiyo fomu hapo ofisi ya kata kusubiria utaratibu mwingine baada ya kurasimishiwa makazi. Sasa kwa kesi yako nakushauri uende ofisi ya mtendaji wa kata yako akupe taratibu.
Taraitora mlangila wange!!
 
msem

JF-Expert Member
Nov 7, 2015
1,788
2,000
Kuna kodi mpya ya majengo imeanzishwa kwa nyumba hata zile ambazo zimejengwa sehemu zisizopimwa.
Hii imekaaje kisheria, maana lazima tutii sheria bila shuruti. Kodi hii iko kisheria? Mpaka sasa nabo sjeria inataka nyumba zilizojengwa katika sehemu zilizopimwa ndiyo zilipe.
Naambatanisha barua ya wito wa kulipa toka TRA kwa sehemu ambazo hazijapimqwa.
Uko sawa mkuu, ila kama kweli tunapenda kutii sheria bila shuruti hata kujenga sehemu ambazo hazijapimwa pia sheria inakataza lakini tunajenga tena bila hata kibali cha ujenzi.

Hakuna namna tulipe kodi tu.
 
Hujaelewa, sehemu ambazo hazijapimwa hakuna kibali cha ujenzi! Na huwa hazilipiwiwi kodi! Sasa haya wanayoyafanya si kinyue cha sheria?
 
msakaa jr

JF-Expert Member
May 18, 2017
3,155
2,000
Hapo ndio huwa naishangaa serikali, inaainisha vitu kuwa vipo kinyume cha sheria lakini bado inaendelea kuzidai kodi.
 
msem

JF-Expert Member
Nov 7, 2015
1,788
2,000
Hujaelewa, sehemu ambazo hazijapimwa hakuna kibali cha ujenzi! Na huwa hazilipiwiwi kodi! Sasa haya wanayoyafanya si kinyue cha sheria?
Hazilipiwi kodi kwa kuwa kisheria haitarajiwi mtu ajenge sehemu hizo, kwa hiyo anapojenga inakuwa ni kinyume cha sheria
 
Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,698
2,000
Ndiyo mkuu. Hiyo kodi ni kwa ajili ya jengo lako. Ipo kisheria na inalipiwa kwa landed properties ambazo ni za kudumu. Nyumba za makuti, kontena na za udongo nadhani ziko excluded kwa kuwa sio permanent landed property...
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
39,643
2,000
Hujaelewa, sehemu ambazo hazijapimwa hakuna kibali cha ujenzi! Na huwa hazilipiwiwi kodi! Sasa haya wanayoyafanya si kinyue cha sheria?
wakiamua kwenda kisheria watabomoa hizo nyumba. Kipi bora ulipe kodi 20,000/-(kwa mantiki hio 'wanarasimisha' nyumba yako) au wavunje nyumba yako kwa mujibu wa sheria.
 
sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,478
2,000
Kuna kodi mpya ya majengo imeanzishwa kwa nyumba hata zile ambazo zimejengwa sehemu zisizopimwa.
Hii imekaaje kisheria, maana lazima tutii sheria bila shuruti. Kodi hii iko kisheria? Mpaka sasa nabo sjeria inataka nyumba zilizojengwa katika sehemu zilizopimwa ndiyo zilipe.
Naambatanisha barua ya wito wa kulipa toka TRA kwa sehemu ambazo hazijapimqwa.
Ktk kikao hiki cha bunge la budget. Waziri mwenye dhamana alifafanua ni nyumba zipi zinazostahili kulipia na zipi hazistahili. Kama nyumba yako ni ya makazi na hujapangisha. Wewe hustahili kulipa. Nyumba za ibada, na zile zinazotoa huruma za serikali nazo hazilipiwi. Lkn nyumba yako unaishi wewe na umepangisha unawajibika kulipia kodi. Au nyumba ya biashara.
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
23,547
2,000
Hazilipiwi kodi kwa kuwa kisheria haitarajiwi mtu ajenge sehemu hizo, kwa hiyo anapojenga inakuwa ni kinyume cha sheria
No please hakuna sheria inayokataza kujenga sehemu isiyopimwa. Hakuna! Huko zinatawala sheria za kimila... customary right of occupancy! ambayo ipo kisheria lakini haina kipengele chas kulipia kodi mpaka uwe na granted right of occupancy
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
23,547
2,000
Ktk kikao hiki cha bunge la budget. Waziri mwenye dhamana alifafanua ni nyumba zipi zinazostahili kulipia na zipi hazistahili. Kama nyumba yako ni ya makazi na hujapangisha. Wewe hustahili kulipa. Nyumba za ibada, na zile zinazotoa huruma za serikali nazo hazilipiwi. Lkn nyumba yako unaishi wewe na umepangisha unawajibika kulipia kodi. Au nyumba ya biashara.
Itakuwa vizuri kama utatuwekea clip hiyo ,
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
23,547
2,000
wakiamua kwenda kisheria watabomoa hizo nyumba. Kipi bora ulipe kodi 20,000/-(kwa mantiki hio 'wanarasimisha' nyumba yako) au wavunje nyumba yako kwa mujibu wa sheria.
Hakuna sheria inayosema sehemu zisizopimwa haziruhusiwi kujenga, haipo! Ila sehemu zilizopimwa lazima uwe na kibali!
 
Johape

Member
Apr 15, 2017
23
75
Mi napenda kulipa kodi ila kuna jambo sijaelewa..mama alijenga nyumba mwaka 2000 ila haijawahi kupimwa walipita kipindi fulan kupima ila hawakufika kwenye eneo letu,sasa nalipa vp kodi na kama bado eneo halijapimwa na zaidi ya hapo kuna taarifa nyumba zilizopo eneo hilo zitabomolewa sabb ziko karibu na mto..sasa nikilipa kodi watafidia wakati wa kuzibomoa..nisaidieni kujibu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom